• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Vitambulisho vya Wafanyabiashara Wadogo Awamu ya Pili Mkoani Kagera Vyakabidhiwa Kwa Wakuu wa Wilaya Watendaji Waonywa

Posted on: February 1st, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti agawa vitambulisho 35,000 vya awamu ya pili vya Wafanyabiashara Wadogo katika Mkoa wa Kagera na kuwaagiza Watendaji wa Serikali chini ya usimsmizi wa Wakuu wa Wilaya kuendelea na zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo na kuhakikisha ifikapo Februari 28, 2019 vitambulisho vyote view vimegawiwa kwa Wafanyabiashara Wadogo.

Katika hafla fupi ya kukabidhi vitambulisho hivyo 35,000 vya awamu ya pili kwa Wakuu wa Wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Februari 1, 2019 Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa katika tahimini iliyowakutanisha Wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara Mkoa wa Kagera haukufanya vizuri sana wa vibaya katika ugawaji wa vitambulisho vya awamu ya kwanza 25,000 kwani ulishika nafasi ya sita kwa ugawaji wa asilimia 65%.

Mkuu wa Mkoa Gaguti katika hafla hiyo fupi aliziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinakusanya takwimu za Wafanyabiashara wote Wakubwa, wa Kati na wale Wadogo ifikapo Februari 15, 2019 takwimu hizo ziwe zimewasilishwa ofisini kwake lengo likiwa ni kuhakikisha kila mwananchi anayetoa bidhaa yoyote na kupokea fedha anatambuliwa na kulipa kodi au tozo stahiki za Serikali.

Hafla hiyo fupi iliyowashirikisha Wakuu wa Wilaya saba za Mkoa wa Kagera, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa, Wenyeviti wa Halmashauri na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Watendaji wa Kata wa Manispaa ya Bukoba waliowawakilisha Watendaji wenzao katika mkoa ambao walitakiwa kutoa changamoto zinazowakumba katika ugawaji wa vitambulisho vya Wafanyabiashara Wadogo katika maeneno yao.

Wakitoa changamoto mbalimbali  kuhusu ugawaji wa vitambulisho Watendaji wa Kata walisema kuwa changamoto kubwa ni Elimu kwa wananchi kutojua ni mfanyabiashara yupi anatakiwa kupata kitambulisho na ni yupi hastahili kupata na changamoto hiyo inatokana na suala la mauzo ghafi kutoeleweka vizuri kwao wao wenyewe Watendaji  kama wahusuika wa ugawaji lakini pia wafanyabiashara jambo ambalo waliitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa uelewa kwao.

Changamoto nyingine iliyotajwa na Watendaji wa Kata waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhi  vitambulisho kwa Wakuu wa Wilaya  ni suala la Mfanyabiashara Mdogo kuwa na namba ya utambuzi ya mlipa kodi ya TRA (TIN) wakati biashara yake ni ndogo na hastahili kupata kitambulisho cha mfanyabiashara mdogo wakati mtaji wake ni mdogo haufikii kiwango cha shilingi milioni 4,000,000/= kwa mwaka.

Akitoa majibu ya  changamoto zilizowasilishwa na Watendaji wa Kata Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera Bw. Adam Ntoga alisema kuwa Mfanyabiashara Mdogo anayestahili kupata kitambulisho ni yule ambaye mauzo yake kwa siku hayafikii shilingi 11,000/= kwa siku. Kama Mfanyabiashara anauza bidhaa zake na kupata kiwango cha fedha chini ya shilingi 11,000/= huyo anastahili kupata kitambulisho cha Mfanyabiashara Mdogo.

“Hata kama Mfanyabiashara ana mtaji wa shilingi 5,000/= lakini anauza bidhaa zake kwa siku na kupata shilingi 11,000/= au zaidi kwa siku huyo hastahili kupata kitambulisho, kinachoangaliwa hapa si mtaji wa mfanyabiashara alionao bali ni mauzo yake kila siku kama anapata kiasi cha shilingi 11,000/= au chini ya kiwango hicho.” Alifafanua Bw. Adamu Ntoga

Katika huatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa onyo kwa Wafanyabiashara ambao walidanganya na kupokea vitambulisho wakiwa tayari wametambuliwa na mfumo wa ulipaji kodi wa TRA kuwa tayari anayo amajina sita hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwao mara moja. Pia aliwaonya Watendaji wa Kata ambao wanaandika barua kuwatambulisha wafanyabiashara kuwa mtaji wao ni mdogo kuwa waache mara moja.

“Watendaji wa Kata acheni hizo tabia zenu za kuwaandikia barua wafanyabiashara na kuwatambulisha kuwa biashara zao ni ndogo, kama kuna Mfanyabiashara alipita TRA na kujisajiliwa mwacheni apite huko huko na kufanyiwa tathimini upya na TRA wao ndiyo watoe barua hizo vinginevyo mkiendelea hatua zitachukuliwa kwenu.” Alionya Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa ufafanuzi juu ya Wafanyabiashara Wadogo wanaopata vitambulisho kuendelea kuto tozo ndogo ndogo za Halmashauri husika katika maeneo wanayofanyia biashara mfano tozo za kukusanya taka au huduma za vyoo na usafi na kuwataka kutotumia kigezo cha vitambulisho na kuacha kulipa tozo hizo. Pia Wafanyabiashara ambao tayari wanatakiwa kulipa kodi katika Halmashauri wanatakiwa kuendelea kulipa kodi hizo baada ya kufanyiwa tathimini na TRA.

Mkoa wa Kagera katika awamu ya kwanza ulipatiwa vitambulisho vya Wafanyabiashara Wadogo 25,000 na Wilaya ya Bukoba ilipatiwa jumla ya vitambulisho 3,580. Wilaya za Missenyi, Karagwe, Kyerwa, Ngara, Muleba, na Biharamulo zilipatiwa vitambulisho 3,570 kila moja. Hadi tarehe 1 Februari,2019 vilikuwa vimegawiwa vitambulisho 16,369  sawa na asilimia 65% kwa Wilaya zote na kiasi cha shilingi milioni 327,380,000/= zilikuwa zimekusanywa na kupelekwa benki.

Vitambulisho vya awamu ya pili Mkoa wa Kagera ulipatiwa vitambulisho 35,000 na vitambulisho hivyo vimegawiwa katika Wilaya kulingana na Jiografia ya Wilaya, wingi wa watu na hali ya kiuchumi tofauti na awamu ya kwanza ambapo katika awamu ya pili Wilaya Bukoba iligawiwa vitambulisho 7,000 Biharamulo na Ngara kila moja iligawiwa vitambulisho 4,200. Kyerwa na Missenyi kila moja vitambulisho 4,400 na Wilaya za Karagwe na Muleba ziligawiwa vitambulisho 5,400.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.