• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Wakuu wa Mikoa Kumi na Moja ya Kanda ya Magharibi na Kanda ya Ziwa Wakiwa Katika Mkutano wa Ujirani Mwema Mkoani Kagera

Posted on: December 15th, 2017

Mikoa Kumi na Moja Yakutana Kagera Kuweka Mikakati ya Kuimarisha Ulinzi na Usalama na Kukuza Uchumi wa Wananchi Katika Mikoa Hiyo

Wakuu wa Mikoa kumi na moja pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama kutoka Kanda ya Magharibi na Kanda ya Ziwa wakutana Mkoani Kagera Manispaa ya Bukoba kufanya mkutano wa pamoja wa ujirani mwema ili kujadili kwa pamoja changamoto za Ulinzi na Usalama na jinsi ya kukabiliana na vitendo vya uharifu vilevile kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ikiwa ni apmoja na fursa za uwekezaji katika mikoa hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye ni Mwenyekiti  wa mkutano huo Mhe. Aggrey Mwanri akifungua mkutano alisema kuwa lengo kuu la kukutana mikoa kumi na moja ni kuweka mkakati wa pamoja katika masuala ya Ulinzi na Usalama na kubadilashana uzoefu wa kudhibiti vitendo vya kihalifu  katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi.

“Hii mikoa kumi na moja ndiyo mikoa ambayo ipo karibu na Makao Makuu ya nchi Dodoma, kama sisi hatutaweka vizuri mikoa yetu uhalifu ukaanzia kwetu Dodoma hakuwezi kuwa salama. Pili, sisi mnatuona hapa tulipewa jukumu kubwa na Waziri Mkuu wa Jamhauri ya Muungano wa Tanzania kusimamia zao la pamba na kuhakikisha hii mikoa inakuwa wazalishaji wakubwa  ambapo sasa tutajadili kwa kina na kuweka mikakati ya pamoja ya kuinua zao la pamba,” Alisisitiza Mhe. Mwanri.

Naye Makamu Mwenyekiti ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akiwakaribisha wajumbe wa Mkutanao huo alisema kuwa Mikutano ya ujirani mwema imesaidia sana kwani kabla ya mikutano hiyo kufanyika operesheni mabalimbali zilikuwa zikifanyika ambapowaharifu walikuwa wakitoka mkoa mmoja na kuhamia mkoa mwingine na na kuweka ugumu wa kuudhibiti uharifu huo.

“Kutokana na umuhimu wa mikutano hii sisi Mkoa wa kagera tumeweza kufanya operesheni  na kufanikiwa kuiondoa mifugo katika Mapori yetu ya Akiba na Hifadhi za Misitu na sasa wanyamapori wamerejea kwa kasi na kuanza kuzaliana sana. Katika mapori hayo waharifu walikuwa wakijificha kwenye mwavuli wa ufugaji lakini tumefanikiwa kuwatokomeza na sasa tunawakaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza katika mahoteli ya kitalii ili kuwavutia watalii katika Maporui hayo.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Kigoma Malima ambaye ni mjumbe wa mkutano huo alisema kuwa mkutano wa ujirani mwema ni muhimu sana kwani kunakuwa na  mada mbalimbali zajinsi ya kukuza na kuinua uchumi wa wananchi katika mikoa husika. Alitoa mfano kuwa katika mkutano wa Kagera kuna mada ya zao la Vanilla ambalo linalimwa Kagera pekee na lina bei kubwa ambapo alisema kuwa amekuja kujifunza ili akaipeleke fursa hiyo katika Mkoa wa Mara.

Akiongea kwa niaba ya Makamanda wa Jeshi la Polisi wenzake  Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanaza Ahmed Msangi alisema kuwa kufanya mikutano ya ujirani mwema,  kupeana na kubadilishana mbinu za kiusalama wameweza kuwadhibiti wahalifu ambapo alisisitiza kuwa wahalifu walikuwa wakifanya uhalifu kwa kuhama kutoka mkoa mmoja na kwenda mkoa mwingine lakini kwasasa hawawezi kutokana na mikakati ya pamoja.

Mkutano huo wa ujirani mwema umefanyika Desemba 15, 2017 katika Manispaa ya Bukoba katika Hoteli ya ELCT Bukoba Mkoani Kagera na mikoa iliyoshiriki mkutano huo ni Kagera,  Tabora, Shinyanga, Mara, Mwanza, Katavi, Geita, Simiyu, Singida, Rukwa na Kigoma. Wakuu wa Mikoa waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti Mhe. Aggrey Mwanri na Makamu Mwenyekiti Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu.

Wengine ni Mhe Adam Kigoma Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita, Wakuu wa mikoa wengine waliwakilishwa  katika Mkutano huo. Aidha, Makatibu Tawala wa Mikoa na wajumbe wa  Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa yote kumi na moja walihudhuria katika mkutano huo wa ujirani mwema .

Mkutano huu wa ujirani mwema ni mkutano wa nne kufanyika ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika Mkoani Tabora mwezi Januari 2017, Mkutano wa pili ulifanyika mwezi Machi 2017 Mkoani Kigoma, Mkutano wa tatu ulifanyika Mkoani Singida mwezi Juni 2017 na Mwezi huu Desemba 2017 Mkutano wa Ujirani Mwema umefanyika Mkoani Kagera.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.