• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Wananchi wa Kisiwa Cha Ikuza Waondokana na Adha ya Huduma za Afya Baada ya TANAPA Kukabidhi Zahanati Kwa Serikali Tayari Kwa Huduma

Posted on: April 16th, 2019

Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) yaikabidhi Serikali mradi wa ujenzi wa Zahanati uliojengwa kwa ushirikiano kati ya TANAPA, Halmashauri ya Wilaya ya Muleba na Wananchi wa Kijiji cha Ikuza kilichopo Kisiwani Ikuza ambapo mradi huo uligharimu kiasi cha shilingi milioni 280,953,625/= hadi kukamilika kwa hatua ya kwanza ya ujenzi wa vyumba kumi na moja vya vyakutolea huduma.

Akikabidhi Zahati hiyo Aprili 16, 2019 Naibu Kamishina Mkuu wa TANAPA Bw. Martin Leboki aiyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu TANAPA Taifa Bw. Alani Kijazi alimweleza Mkuu wa Mkoa wa Kagera na wananchi waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano kuwa zahanati hiyo imejengwa na kukamilika kwa ushirikiano mkubwa kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba na wananchi wa kijiji cha Ikuza kutokana na ujirani mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.

Bw. Leboki alisema kuwa TANAPA ilitoa jumla ya shilingi milioni 144,725,675/= katika ujenzi wa zahanati hiyo yenye vyumba kumi na moja na kununua vifaa tiba kama vitanda vya wagonjwa, vitanda vya akinamama wajawazito kujifungulia pamoja na samani nyingine zitakazotumika katika zahanati hiyo. Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ilichangia jumla ya shilingi milioni 124,392,340/= na wananchi walichangia jumla ya shilingi milioni 14,535,000/=

Pamoja na kukamilika kwa zahanati hiyo ya Kijiji Ikuza lakini wananchi walibainisha kuwa bado kuna changamoto ya kutokuwa na shimo la kutupia kondo la nyuma, upatikanaji wa umeme na maji katika zahanati hiyo. Pamoja na changamoto hizo lakini wananchi wa Kijiji Ikuza waliishukuru TANAPA kwa kukubali kushirikiana nao kuwajengea zahanati ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya afya katika kisiwa hicho na visiwa vya jirani.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akipokea zahanati ya Kijiji Ikuza kwa niaba ya Serikali aliishukuru TANAPA kwa kushirikiana na wananchi wa Ikuza na kuwajengea Zahanati ya kuwahudumia na kuwaondolea changamoto ya upatikanaji wa huduma ya afya katika kisiwani humo pamoja na visiwa vya jirani.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa pamoja na Serikali kuwa imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kasi kubwa tangu mwaka 2015/16 lakini bado kuna uhitaji mkubwa hasa katika vijiji ambapo alisema kuwa mwaka 2015/16 mkoa wa Kagera ulikuwa unapokea fedha za afya shilingi milioni 800/= lakini hadi sasa mkoa unapokea shilingi bilioni 5 kwa mwaka, Wilaya ya Muleba ilikuwa inapokea shilingi milioni 400 lakini sasa inapokea shilingi bilioni 1 kwa mwaka.

Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano katika mkoa wa Kagera imejenga Vituo vya Afya 14 kwa gharama ya shilingi bilioni 6.9 na tayari imeto shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya .  “Pamoja na juhudi hizo zote kufanyika lakini uhuhitaji katika vijiji ni mkubwa na kama hatutajenga zahanati kama hizi mlundikano katika Vituo vya Afya utakuwa mkubwa mno.” Alisisitiza Mhe. Gaguti

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa maagizo kuwa zahanati hiyo inatakiwa kuanza kutoa huduma mara moja isikae tena mwaka bila kutoa huduma kwa wananchi. Kuhusu changamoto za wananchi juu ya shimo la kondo la nyuma alitoa mifuko 50 ya saruji ili shimo hilo lianze kujengwa kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Ikuza.

Kuhusu umeme, Mkuu wa Mkoa Gaguti alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bw. Emannuel Shelembi kufunga mara moja solar ambayo tayari ipo katika ofisi za Halmashauri pia kuhakikisha Mkurugenzi huyo anaandaa watumishi wa kwenda kutoa huduma katika zahanati hiyo. Na kuhusu suala la maji aliwahakikishia wananchi kuwa atatoa Sim tank ya lita 5000 na wao wachimbe mtaro kutokea ziwani ili maji yapatikane kwa haraka.

Mwisho, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwashukuru TANAPA kwa kuendelea kudumisha ujirani mwema na wananchi wanaopakana na Hifadhi za Taifa ambapo alimshukuru tena Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Taifa kwa kumkubalia kushirikiana naye kujenga Zahanati katika vijiji vinavyopakana na Mapori yaliypandishwa hadhi na kuwa hifadhi za Taifa za Biharamulo Burigi na Kimisi, Ibanda na Rumanyika.

Naye diwani wa Kata ya Ikuza Mhe. Fortunatus Wazia Matta aliishukuru TANAPA na Serikali kwa kuwasogezea karibu wananchi huduma ya afya kwani alisema kuwa tangu alipochaguliwa kuwa diwani wa kata ya Ikuza mwaka 2010 hadi sasa wakina mama wajawazito wanne tayari wamepoteza maisha yao kutokana na changamoto ya afya katika kata hiyo iliyopo visiwani.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 Kupitia Miradi Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 23.8

    September 07, 2025
  • Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 Kupitia Miradi Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 23.8

    September 07, 2025
  • Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera Yafungu Dawati Maalu la Uwezeshaji Wafanyabiashara

    September 03, 2025
  • Nsekela Stadium Yazinduliwa Rasmi Kyerwa - Kagera

    August 29, 2025
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.