• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Wanunuzi Binafsi Hawajazuiliwa Kununua Kahawa Nia ya Serikali ni Kuona Mkulima Ananufaika na Kahawa Yake Kwa Kulipwa Vizuri

Posted on: July 12th, 2019

Kuhusu ununuzi wa Kahawa Mkoani Kagera lengo kuu la Serikali ni kuona wakulima wanapata bei nzuri wananufaika na zao lao la kiuchumi la kahawa tena wanalipwa kwa wakati ili kukidhi mahitaji yao mbalimbali ya kuwasomesha watoto na kujikimu kifamilia.

Ndiyo maana tangu msimu uliopita wa mwaka jana 2018 Serikali iliamua kuanzisha mfumo mpya wa kuhakikisha Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera havinunui kahawa bali vinakusanya kahawa ya Wakulima na baadae kuiuza kahawa hiyo kwaniaba ya wakulima na siyo vyama hivyo vikuu kufanya biashara.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti wakati akizindua rasmi msimu wa ukusanyaji wa kahawa kwa Vyama Vikuu vya Ushirika vya KCU 1990 LTD na KDCU LTD mwaka huu Juni 29, 2019 Nkwenda Wilayani Kyerwa alieleza wazi kuwa mwaka huu 2019 atahakikisha wakulima wanapata malipo yao ya awali ya shilingi 1100/= kwa kila kilo ndani ya siku kumi baada ya mkulima kupeleka kahawa zake katika chama cha Msingi.

Pili, aliwaomba wakulima kuhakikisha wanafungua akaunti benki ili walipwe fedha zao kupitia Benki ili kupunguza mianya ya fedha ya mkulima kutumika isivyopangwa hasa kwa viongozi wa Vyama vya Msingi ambapo Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini Bw. Japhet Justine aliweka wazi kuwa faida ya mkulima kulipiwa benki itamsaidia kuaminika kukopesheka kwasababu taarifa zake za kibenki zitaonesha mapato yake anayoyapata kwa msimu.

Tatu, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwataka wanunuzi binafsi kuweka wazi bei zao za kahawa ili kama wapo tayari na kutoa bei inayomnufaisha mkulima wawasiliane na ofisi yake wapatiwe kahawa na siyo kwenda kwa wakulima mashambani kununua kahawa huko, hapo Serikali sasa inataka Mkulima asidhurumiwe wala kulipwa fedha kiduchu.

Julai 11, 2019 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli akitokea Wilayani Karagwe pia alipigilia msumari kuwa Serikali iliamua kuanzisha mfumo wa kuvipa Vyama Vikuu vya Ushirika Fedha ili vikusanye kahawa ya wakulima na kuiuza kwa kulenga kumunufaisha mkulima. Pia alitoa wito kwa wanunuzi binafsi kama wanataka kununua kahawa watoe bei nzuri na wamuone Mkuu wa Mkoa watanunua kahawa.

Kiukweli  maoni mengi yamekuwa yakitolewa kutoka Wilaya zinazolima kahawa kwa wingi za Karagwe na Kyerwa kuwa wanunuzi binafsi waruhusiwe kutoka nchi jirani lakini ukiwauliza walalamikaji hao kwanini wanunuzi hao wanunue kahawa usiku tena kutoka kwa mkulima moja kwa moja na kupitisha kahawa hizo njia za panya  na si kununua mchana  na kupita mipaka halali hawatoi majibu.

Nakumbuka Mkuu wa Mkoa Gaguti akiwa anakagua mipaka Wilayani Kyerwa Juni 13, 2019 Mzee Johakhim John alilalamika kuwa wanunuzi binafsi waruhusiwe kutoka nchi jirani na Mhe. Gaguti alimweleza kuwa kama anaye mnunuzi ambaye yupo tayari kununua kahawa mchana amlete na aseme anataka tani ngapi na aseme bei yake lakini Mzee John alibaki kimya na alipoelezwa faida za mfumo mpya alibaki kuipongeza Serikali na kuomba iongeze Vyama vya Msingi vya kukusanyia Kahawa kutokana na umbali wa kuvifikia vilivyopo.

Katika suala hili la kahawa Serikali haijapiga marufuku wanunuzi binafsi bali utaratibu ufuatwe kodi ya Seriakli ilipwe tena stahiki mkulima alipwe vizuri kwa wakati na kwa kahawa yake ipimwe kwa kipimo sahihi ambacho ni mzani na si (visado) ambavyo ukijaza unaambiwa kilo moja kumbe kilo mbili nanusu hadi tatu, au (Rumbesa) unaambiwa kilo sitini kumbe kilo mia na zaidi.

Wakulima tufunguke macho Serikali nia yake ni nzuri kwani kuna mnunuzi atakwambia mwaka huu bei ya kahawa ni kiasi fulani jambo ambalo si kweli bali bei hotulewa na soko la dunia na ndiyo maana unapolipwa mwanzoni unaambiwa hayo ni malipo ya mwanzo ili kahawa ikishauzwa katika soko la dunia nyongeza ikipatikana mkulima anaongezewa.

Katika picha zifuatazo hapo chini unaweza kuona Wakuu wa Mkoa huu wa Kagera kwa vipindi tofauti wanavyoangaika na vipimo vya kupimia kahawa za Wakulima kama vipo sawa. Aliyewahi kuwa Mkoa wa Kagera  Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu unamuona akihakiki mzani kwa kuhakiki uzito wake mwenyewe. Pili Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa sasa  Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti unamuona akihakiki mzani hadi nukta (Point) za mkulima zisomwe katika mzani ili mkulima asiibiwe au kupunjwa

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.