• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Washiriki wa Mafunzo ya PS3 Juu ya Utoaji Motisha kwa Watumishi Mkoani Kagera.

Posted on: November 4th, 2017

PS3 Yazinoa Halmashauri Mkoani Kagera Juu ya Motisha Kwa Watumishi Ili Kuboresha Utoaji Huduma Kwa Wananchi

Mradi wa kuimarisha Mifumo katika Sekta ya Umma Tanzania (PS3) wawanoa watendaji na Waajiri Mkoani Kagera namna bora ya kuwamotisha watumishi wao katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili watumishi hao waweze kufikia malengo na matarajio ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mafunzo hayo ya siku sita Mkoani Kagera yamewahusisha Wenyeviti, Wakurugenzi na  Wakuu wa Idara wa Halmashauri za Wilaya mbili za Biharamulo na Kyerwa ambazo zipo katika awamu ya kwanza ya Mradi wa PS3 pamoja na Wakuu wa Idara katika idara za Utawala na Raslimali Watu kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Kagera Kagera.

Mafunzo hayo yamelenga kuboresha utendaji na utoaji wa huduma bora kutoka kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenda kwa wananchi ambapo mtumishi akipewa motisha mbalimbali anazozistahili hutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na mwananchi hupata huduma anayostahili kupata na kwa wakati.

Mafunzo hayo yamelenga kuwakumbusha Waajiri na Wakuu wa Idara hasa Idara za Utawala na Raslimali Watu kutoa motisha kwa watumishi wao jambo ambalo litawafanya watumishi hao kufanya kazi katika eneo lolote hata kama kuna changamoto za baadhi ya huduma za jamii mfano vijijini ambako huduma za maji na umeme hazijawafikia wananchi.

Akitoa ufafanuzi juu ya ufanisi wa mafunzo hayo Bw. Aloyce Msigwa kutoka PS3 Makao Makuu Dodoma alisema Mradi unalenga kuwakumbusha waajiri na wakuu wa idara juu ya utoaji wa motisha ili huduma kwa wananchi ziweze kuboreka lakini pia na kupunguza msongo wa mawazo kwa watumishi wakati wakitekeleza majukumu yao.

Akifunga mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Nesphory Bwana aliwakumbusha washiriki wa mafunzo hayo kuwa Serikali ilishatoa mwongozo wa namna ya kuwahamasisha watumishi ili waweze kutoa huduma bora kupitia utoaji wa motisha.

“Mwongozo huo ulitolewa kupitia Sera ya Malipo na Motisha ya mwaka 2010 na upo muda mrefu lakini kwa sababu mbalimbali waajiri na hasa Mamlaka za Serikali za Mitaa wamekuwa wazito katika kubuni mbinu za kuutekeleza. Wakati mwingine jambo hili halitekelezwi siyo kwa sababu ya uwezo mdogo wa Halmashauri bali kwa sababu ya Uongozi husika kutokuona umuhimu wake na hivyo kutolipa kipaumbele.” Alisistiza Bw. Nesphory 

Aidha, Bw. Nesphory alitoa wito kwa viongozi wote, watendaji na wanasiasa kubadilika na kulipa umuhimu jambo hilo kwa kuanza kulitengea bajeti kila mwaka kwa yale ambayo Halmashauri ina uwezo nayo.

Katika hatua nyingine Halmashauri za Wilaya za Biharamulo na Kyerwa ziliweza kupata fursa ya  kuandaa mipango ya motisha kwa watumishi wao na pia mikakati ya kuitekeleza mipango hiyo. Ambapo pia Halmashauri hizo mbili ziliweza kubadilishana mipango hiyo ya motisha kwaajili ya ufanisi zaidi.

Mafunzo hayo yalifunguliwa Oktoba 30, 2017 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Kamishna Diwani Athumani na yamefungwa leo Novemba 4, 2017.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 Kupitia Miradi Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 23.8

    September 07, 2025
  • Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 Kupitia Miradi Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 23.8

    September 07, 2025
  • Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera Yafungu Dawati Maalu la Uwezeshaji Wafanyabiashara

    September 03, 2025
  • Nsekela Stadium Yazinduliwa Rasmi Kyerwa - Kagera

    August 29, 2025
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.