• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Watendaji wa Kata na Vijiji Mnayo Mamlaka Makubwa Mnavaa Kofia Zote za Ulinzi na Usalama Katika Maeneo Yenu

Posted on: September 17th, 2019

Watendaji  wa Kata na Vijiji mnavaa kofia zote za vyombo vya Ulinzi na Usalama wa nchi, nyinyi watendaji ni Askari Polisi, Uhamiaji, Usalama wa Taifa na ni askari Jeshi wa ulinzi wetu katika maeneo yenu ya kazi, simamieni majukumu yenu kwa nguvu zote bila kupepesa macho hakuna wa kuwababaisha.

Maneno hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti  Septemba 16, 2019 wakati akizungumza na Watendaji wa Kata na Vijiji katika Halamashauri ya Wilaya ya Missenyi alipokuwa akiwakumbusha wajibu wao wa utendaji wa kazi katika maeneo yao.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti  aliwakumbusha watendaji hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ni Serikali ya ugatuzi wa madaraka kuwa wanao wajibu wa kuhakikisha suala la ulinzi na usalama linamarishwa na mtu wa kwanza kuwajibika ni Mtendaji wa Kijiji akifuatiwa na Mtendaji wa Kata kuzuia uhamiaji haramu na vitendo vya uvunjifu wa amani.

“Mimi kama Mkuu wa Mkoa sitegemei kupokea kero yoyote katika ofisi yangu ambayo Mtendaji hajashughulika nayo, ninyi mnatakiwa kuhusika na kila jambo la mwananchi hakuna jambo lolote ambalo Mtendaji anatakiwa asilijue katika kijiji chake au Kata yake hata kama ni jambo la kifamilia.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Pia Mhe. Gaguti aliwakumbusha Watendaji hao kusimamia miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kujihusisha na kero za wananchi akitolea mfano wa Vyama vya Msingi katika maeneo yao kuwa wakulima wakati wakihangaika kulipwa fedha zao Watendaji wanakaa pembeni kama jambo hilo haliwahusu kumbe wao wanatakiwa kufanya ufuatiliaji kuhakikisha kila mkulima amelipwa au apewe  majibu sahihi kwanini hajalipwa.

Mwisho Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwakumbusha Watendaji hao kutoa utumishi uliotukuka kwa wananchi, kuwapokea, kuwasikiliza na kutatua kero zao tena kwa kuwapa maandishi si maneno tu. Pia aliwakumbusha kuwa wasiwe miungu watu bali wawe watu wa chini kabisa na kutoa huduma iliyotukuka kwa wananchi ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele vile vile Watendaji hao wawe mstari wa mbele katika kukusanya kodi ya Serikali

Katika hatua nyingine Watendaji hao wa Kata na Vijiji walimweleza Mkuu wa Mkoa  kuwa changamoto kubwa kwao ni migogoro ya ardhi kwa maeneo wanayoyaongoza ambapo aliwaelekeza wakae na wahusika na kuimaliza migogoro hiyo na kuwashauri wananchi wanaomiliki ardhi hizo kuzipima ili kuondoa migogoro ya kesho.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.