• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Watumishi wa Sekta ya Afya Toeni Huduma Bora Kwa Wananchi Kama Ubora wa Majengo Unavyoonekana – RC Gaguti

Posted on: August 24th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti awataka watumishi wa Sekta ya Afya Mkoani Kagera kutoa huduma bora kwa wananchi kulingana na hadhi na ubora wa majengo yaliyojengwa ama kuboreshwa kwa fedha za Serikali kwa kiwango cha kuridhisha katika Vituo mbalimbali vya Afya  ili kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana katika vituo hivyo hasa huduma za upasuaji kwa mama wajawazito.

“Nimeridhika na ubora wa majengo yaliyojengwa katika kituo hiki pamoja na thamani ya fedha inaonekana katika majengo haya, rai yangu kwenu watumishi wa Kituo hiki cha Afya na vituo vyote vilivyoboreshwa Mkoani Kagera ni kutoa huduma zinazofanana na majengo yalivyo, huduma safi kwa wananchi zenye kuwafariji wanapokuja kupata huduma za afya hapa.” Alisisitiza Mhe. Gaguti

Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa rai hiyo Augusti 24, 2018 katika Kituo cha Afya Kimeya Wilayani Muleba alipofanya ziara ya kujitambulisha katika Wilaya hiyo na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo alitembelea na kukagua ujenzi wa majengo matano yaliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 456 zilizotolewa na Serikali pamoja na wananchi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 11.7

Majengo yaliyojengwa ni pamoja na jengo la Mama na Mtoto, Jengo la Maabara, Nyumba moja ya Mtumishi, Jengo la upasuaji, na Jengo la kuhifadhi maiti. Mhe. Gaguti aliwashukuru wananchi kuchangia miradi ya maendeleo na kuwataka kuendelea kuchangia miradi mbalimbali ili kujiletea maendeleo na kuitunza pia miradi hiyo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alitembelea shamba la kahawa lenye ekari 45 la Mkulima Bw. Shakiru Yahya lililoko Kijijini Karutanga kata ya Magata Karutanga na kujionea kilimo cha Kahawa cha kisasa na chenye tija ambapo shamba hilo ni la mfano kwa wakulima wengine ambao wanajishughulisha na kilimo hasa zao la Kahawa.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Mkulima wa shamba hilo Bw. Shakiru Yahya alisema kuwa alihamasishwa kulima kahawa na baba yake mzazi wakati akiwa mdogo baada ya baba yake kuwa analima Kahawa na kuuza na kupata fedha za kuendesha familia ikiwa ni pamoja na kuwapatia matumizi mbalimbali ya kifamilia na karo za shule.

Baada ya kujitegemea Bw. Shakiru mwaka 2000 alianza kulima kidogo kidogo na mpaka sasa amefikisha ekari 45 za shamba la mibuni aina ya Arabika na Robusta na amepata mafanikio makubwa kwani kwa msimu uliopita aliweza kuvuna tani 40 za kahawa  na kupata fedha za kitanzania shilingi milioni 60, anasomesha watoto wake, ameajili zaidi wafanyakazi 50, amenunua magari ya kusafirisha mizigo, amenazisha kiwanda cha kusindika kahawa chenye gaharama ya milioni 650.

Mara baada ya kutembelea na kukagua shamba hilo . Gaguti aliwataka wananchi wa Wilaya ya Muleba hasa wanaozunguka shamba hilo kwenda kwa Bw. Shakiru kujifunza kilimo cha Kahawa badala ya kuendelea kumtazama tu. Aidha, Mhe. Gaguti alimshukuru mkulima huyo kwa kuwekeza katika Sekta ya Kilimo na sasa kuanzisha kiwanda ambapo alimhakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana naye ili kuhakikisha lengo alilokusudia linatimia.

Katika Ziara hiyo pia Mkuu wa Mkoa aliweza kuongea na Watumishi wa Serikali, Wazee na Wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Wilaya ya Muleba ambapo aliwakumbusha watumishi wa umma kuhakikisha wanatatua kero za wananchi kila  Mtumishi katika nafasi yake ili kupunguza migogoro mbalimbali katika jamii na kuwafanya wananchi waiamini Serikali yao.

Mwisho Mhe. Gaguti alitoa msisitizo wa kulipa kodi ya Serikali kwa wadau mbalimbali na wafanyabiasha ambapo alisema kuwa bado hajaridhishwa na kiwango cha ulipaji kodi katika Mkoa wa Kagera. Mhe. Gaguti alisema suala hilo ni kipaumbele chake katika Mkoa na anataka kuona Kagera inaongoza katikaulipaji wa kodi bila shuruti.

Mkuu wa Mkoa Gaguti anaendelea na ziara ya kujitambulisha katika Wilaya za Mkoa wa Kagera ili kuufahamu vizuri mkoa wake na maeneo yake ya utawala  lakini paia anaendelea na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri za Wilaya.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.