• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Waziri Dkt. Augustine Mahiga Tanzania na Waziri Sam Kutesa Uganda Wakisaini Makubaliano ya Ushirikiano Kati ya Tanzania na Uganda Mjini Bukoba Mkoani Kagera..

Posted on: July 30th, 2017

Tanzania na Uganda Zakubaliana Masuala Makuu Manne ya Ushirikiano Katika Maendeleo na Kutiliana Saini Mkoani Kagera

Hatimaye mkutano wa ujirani mwema kati ya Tanzania na Uganda umemalizika leo Julai 29, 2017 majira ya jioni kwa Mawaziri wa nchi hizo mbili kutiliana saini hati za makubaliano ya utekelezaji wa masuala makuu manne ya ushirikiano katika maendeleo waliyokubaliana kwenye  mkutano huo wa siku moja.

Akitoa Taarifa mara baada ya makubaliano na kutiliana saini katika hati za makubaliano Waziri wa Mambo ya nje wa Uganda Mhe. Sam Kutesa alisema yeye akiongoza jopo la Mawaziri kumi kutoka Uganda pamoja na wataalam wengine wamefurahishwa sana na Mkutano huo kwani umekuwa wa mafanikio kwao.

Aidha Mhe. Kutesa alisema kuwa katika Mkutano huo wamekubaliana masuala makuu manne ambayo yanahusu Kuhakiki mipaka ya kati ya nchi mbili, pili Huduma za maji kutoka Mto Kagera, Tatu Biashara baina ya nchi mbili na nne Kuhusu suala la nishati ya Umeme.

Akitoa ufafanuzi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Afrika Mashariki  Dk.Augustine Mahiga alisema kuwa kuhusu Suala la Mipaka wamekubaliana kuongeza alama za mipaka ili mpaka uonekane vyema kati ya nchi mbili ili kuondoa migongano inyoweza kujitokeza maeneo ya mpakani kwasababu mipaka hiyo iliwekwa na Wakoloni miaka mingi iliyopita.

Pili Dkt. Mahiga lifafanua suala la Huduma ya maji katika Mto Kagera na kusema kuwa nchi ya Uganda wanayo matatizo ya maji kwa baadhi ya sehemu mpakani na Tanzania na maji yanapatika Mto Kagera kwa upande wa Tanzania kwa hiyo katika suala hilo Waganda wameomba na kukubaliana na Tanzania kujenga mabwawa  na malambo kwaajili ya kunywesha mifugo yao.

“Suala hilo tumekubaliana lakini taratibu zote za mazingira zitafuatwa ili kusijekukatokea uharibifu wa mazingira na uvujanjaji wa sheria za mazingiara.” Alisistiza Waziri Dkt. Maiga. Kuhusu suala la Biashara Dkt. Maiga alifafanua kuwa wamekualiana kuimarisha biashara kati ya nchi mbili pamoja na kuwa nchi hizo zote zipo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kuhusu Nishati ya Umeme Waziri Dkt. Maiga alisema kuwa mji wa Bukoba unapata umeme kutoka Uganda kwa hiyo Tanzania imekuwa ikipata nishati hiyo toka Uganda lakini kwa sasa Tanzania pia inatarajia kuzalisha umeme wa kutosha ambapo wamekubaliana pia kuwa mara ya umeme huo kuwa umepatikana Tanzania pia itawauzia Umeme Uganda.

Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya ELCT Bukoba ulihudhuliwa na Mawaziri kutoka Tanzania saba pamoja na wataalam mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Afrika Mashariki  Dk.Augustine Mahiga.  Aidha, kwa upande wa nchi ya Uganda uliongozwa na Waziri wa Mambo ya nje Mhe. Sam Kutesa pamoja na Mawaziri kumi wakiambatana na Wataalamu mbalimbali.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.