• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Waziri Kalemani Afurahishwa na Utayari wa Wadau Mkoani Kagera Kuchangamkia Fursa Zitakazopatika Kutokana Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi

Posted on: June 1st, 2019

Waziri wa Nishati Medard Kalemani afurahishwa na utayari wa wadau na wananchi wa mkoa wa Kagera katika kuchangamkia fursa na ajira wakati mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga kilometa 1445 pale utakapokuwa umeanza ujenzi wake.

Waziri Kalemani aliyasema hayo Juni Mosi 2019 katika Ukumbi wa Hoteli ya ELCT Bukoba akifungua na kuongoza kongamano la wadau wa mkoa wa Kagera kuhusu mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanga Tanzania ambapo aliwaeleza wadau hao fursa mbalimbali za mradi huo na ni hatua gani mradi umefikia kabla ya kuanza kwasasa.

Waziri Kalemani alisema kwa kuwa Mkoa wa Kagera ndipo bomba la mafuta kutoka nchini Uganda litaaingilia Tanzania Wizara pamoja na wadau wa ujenzi wa mradi huo kwapamoja walipanga na kuamua kuleta kongamano la wadau Kagera ili wananchi waelewe vizuri ni namna gani watanufaika na kwasasa mradi upo katika hatua gani ili elimu iwafikie wananchi kule bomba litakapopita.

“Nimefurahishwa na utayari wa mkoa kwa namna mlivyochangia mawazo yenu unaweza kuona utayari wa kushiriki katika mradi huu mkubwa wa kimataifa, mradi huu unatarajia kuajiri watu 10,000 wakati wa ujenzi na watu 20,000 wakati ukikamilika lakini naona Kagera tayari mmeulewa mradi vizuri na kati ya ajira hizo lazima mhakikishe ajira na fursa za wazabuni mbalimbali zinabaki hapa.” Alisistiza Waziri Kalemani

Mradi wa Bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania utakuwa na urefu wa kilometa 1445 na asilimia 80% ya kilometa hizo zitakuwa upande wa Tanzania ambazo ni kilometa 1147 na asilimia 20% zinazobaki zitakuwa upande wa Uganda ambapo bomba hilo litapita katika mikoa minane ya Tanzania, Wilaya 24 na Kata 134.

Mikoa hiyo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma Manyara na Tanga aidha, katika Mkoa wa Kagera bomba litapita katika Wilaya za Missenyi, Bukoba (vijijini), Muleba na Biharamulo. Pia litapita katika Kata 20 za Mkoa wa Kagera, Vijiji 34, na Vitongoji 117.

Mafuta ghafi yaligunduliwa Ziwa Albert nchini Uganda na kuonekana kuna mapipa bilioni 6.5 na inatarajiwa mapipa bilioni 1.7 kuuzwa nchi za nje kupitia bomba litakalopita nchini Tanzania na  gharama ya ujenzi wa mradi mzima wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Chongoleani  mpaka kukamilika utagharimu jumla ya Dola bilioni 3.5 za Kimarekani (3.5 billion USD).

Bomba la mafuta ghafi litakuwa linasafirisha mapipa ya mafuta 216,000 kwa siku na kila pipa moja litakuwa linalipiwa kodi ya dola 12.5 za Kimarekani ukiachilia mbali na kodi nyinginezo zitakazokuwa zinalipwa kwa nchi nchi ya Tanzania. Makampuni makubwa matatu ndiyo yatateleza mradi huo nayo ni TOTAL kutoka Uingereza, TULLOW kutoka Ufaransa na CNOOC kutoka nchini China.

Katika mradi mzima wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi vitajengwa vituo sita vya kusukuma mafuta viwili upande wa Uganda na vinne upande wa Tanzania na  katika vituo vinne vitakavyojengwa Tanzania kituo kimoja kitajengwa Kyaka Wilayani Missenyi Mkoani Kagera, kingine kitajengwa mkoani Singida na viwili vitajengwa mkoani Tanga.

Pia katika mradi huo zitajengwa kambi 12 za wafanyakazi na yadi 10 za kuhifadhia mabomba, kati ya  kambi 12 zitakazojengwa kambi 2 zitajengwa mkoani Kagera katika Wilaya za Missenyi na Muleba ambapo wananchi watakaokuwa karibu na kambi hizo watanufaika na upimiwa wa ardhi katika maeneo yao, kuwekewa umeme kwa vijiji ambavyo vitakuwa havijapata umeme pia na fursa mbalimbali kama kufanya biashara.

Waziri Kalemani aliwahakikishia wadau wa kongamano la bomba la mafuta mkoani Kagera kuwa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uganda zimefikia asilimia 80% ya majadiliano ya utekelezaji wa mradi tangu kusainiwa mkataba wa makubaliano Mei 26, 2017 na mara baada ya majadiliano hayo kukamilika kwa asilimia 100% ujenzi wa bomba unatarajia kuanza Septemba 2019 na utekelezaji wadi hadi kukamilika utakuwa wa miaka mitatu.

Vilevile Wazir Kalemani alisema kuwa wananchi waliotathminiwa mali zao kupisha bomba la mafuta  wataanza kupatiwa taarifa za tathmini zao watalipwa kiasi gani kuanzia wiki ya pili ya mwezi huu wa Juni 2019. Jumla ya wananchi 10,000 walitathminiwa  katika mikoa minane na kwa mkoa wa Kagera ni wananchi 2017 ndiyo watapisha bomba la mafuta ghafi.

Katika hatua nyingine wadau wa kongamano walimshauri Waziri Kalemani mradi kuzingatia kutoa kipaumbele kwa wazawa (Local Content) ili waweze kunufaika na mradi huo ambapo Profesa Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini alimshauri Waziri kuangalia namna ya kupata ufadhili wa elimu ili Watanzania wakasome masuala ya mafuta kuliko kuendelea kuwa walinzi tu bali na wataalam wapatikae ukizingatia mradi ni wa muda mrefu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akifunga kongamano la wadau wa bomba la mafuta alimshukuru Waziri Kalemani kwa kuleta kongamnao hilo mkoani Kagera kwani ndiyo mkoa ambako bomba linapoingilia nchini Tanzania. Pia alitoa ushauri kwa wadau kuwa tayari kwa vigezo katika ajira na kujipanga kimtaji ili fursa zitakapotangazwa wasishindwe kutokana na ushindani kutoka nje ya mkoa.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.