• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Waziri Luhaga Mpina Aliyeshika Mtumbwi Akikagua Mitumbwi Zaidi ya 50 Iliyokamatwa na Katika Doria za Kudhibiti Uvuvi Haramu Mkoani Kagera

Posted on: December 6th, 2017

Waziri Mpina Amsimamisha Kazi Mtumishi Aliyeruhusu Samaki Kutoroshewa Nchini Burundi Bila Kufuata Sheria Za Nchi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amtumbua Afisa wa Kitengo cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi mpakani Bw. Ayoub Ngoma ambaye aliruhusu gari lililokuwa limebeba samaki wasioruhusiwa kuvuliwa zaidi ya tani mbili ambapo samaki hao walikuwa wakitoroshwa kuelekea nchini Burundi kupitia mpaka wa Murusagamba Wilayani Ngara.

Waziri Mpina alimwagiza Katibu mkuu wa Wizara  yake Dk. Yohana Budeba kuhakikisha anamsimamisha kazi mara moja mtumishi huyo kabla ya saa 6:00 mchana na kupewa taarifa pia na taratibu za kumfukuza kazi zianze mara moja  baada ya kuonekana anashirikiana na waharifu kuihujumu Serikali.

Agizo hilo lilitolewa na Waziri Mpina akiwa katika siku yake ya pili ziarani Mkoani Kagera tarehe 6.12.2017 alipofanya ziara katika Idara ya Maendeleao ya Uvuvi Mkoa wa Kagera na kupokea taarifa kutoka kwa Kaimu Afisa Mfawidhi Usimamizi wa Raslimali zaUvuvi Kagera Bw. Gabriel Mgeni ambapo alitolea taarifa tukio hilo lililotokea Murusagamba Wilayani Ngara Desemba 3, 2017.

Bw. Mgeni alisema kuwa  tarehe 3.12.2017 majira ya saa 9:00 asubuhi Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya  Ngara walikamata gari lenye namba za usajili T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter ikiwa imepakia samaki wenye uzito wa zaidi ya kilo 2,000 aina ya Sangara kilo 530 Samaki  aina ya Sato.

Kwa mujibu wa sheria namba 22 ya mwaka 2003 watuhumiwa waliokamatwa wanasafirisha samaki hao walikuwa wamekiuka   taratibu zifuatazo ; kuvua  samaki wenye ukubwa zaidi ya sentimita 85 na wadogo chini ya sentimita 50, kutokuwa na kibali cha kusafirisha mazao ya uvuvi, kutolipa mrahaba wa Serikali, kutokuwa na cheti cha afya pamoja na leseni ya kuuza mazao ya uvuvi nje ya nchi.

Bw. Mgeni alisema kuwa samaki hao baada ya kukamatwa Mahakama ilitoa kibali maalum na kugawa samaki hao kwenye taasisi za Serikali na wananchi. Waziri Mpina alizishukuru Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera kwa juhudi kubwa za kupambana na vitendo haramu vya kutorosha maliasili za nchi nje ya nchi.

Waziri Mpina pia alitoa rai kwa watumishi ambao wapo chini ya Mamlaka yake kuwa kwa yeyote ambaye atagundulika kujihusisha na vitendo vya kuihujumu Serikali hawezi kubaki  kazini  kwani akibainika tu lazima achukuliwe hatua kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi moja kwa moja. Vilevile alimwagiza Mwanasheria wa Wizara yake kuhakikisha anaharakisha mchakato wa kuitaifisha gari lililokamatwa na samaki likiekea nchini Burundi.

Aidha, katika hatua nyingine Waziri Mpina alijionea mafurushi 6 ya samaki aina ya migebuka kilo 240 yaliyokamatwa katika kituo Kikuu cha Mabasi Bukoba yakisafirishwa kwenda nchini Uganda, Mabondo kilo 100 ambapo mtuhumiwa wake alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi, Majora 200 yenye thamani ya shilingi milioni 20 na mitumbwi zaidi ya 50 iliyokamtwa katika doria .

Waziri mpina aliiagiza Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Kagera kuhakikisha inaendelea na juhudi za kukamata wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu na utoroshaji wa samki nje ya nchi ambapo tani 100 hutoroshwa kila wiki kuelekea nchi jirani.  Waziri Mpina amehitisha Ziara yake ya Siku mbili Mkoani Kagera leo tarehe 6.12.2017 na kuelekea Mkoani Kigoma.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.