• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Waziri Luhaga Mpina (Wa tatu Kutoka Kushoto) Akikagua Sehemu ya Kunyweshea Maji Ng'ombe Katika Ranchi ya Kagoma

Posted on: December 6th, 2017

Waziri Mpina Amutimua Mwekezaji Mbabaishaji Agri Ranch Katika Ranchi ya Taifa ya Kagoma Mkoani Kagera

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ampa  siku saba mwekezaji wa Ranchi za Kagoma, Mabale na Kikurula AGRI RANCHI  kuwa ameondoa  mifugo yake katika Ranchi hizo baada ya kukiuka masharti ya mkataba wake na Kampuni ya Huria (Ranchi)  za Taifa (NARCO) na kuendelea kutumia Ranchi hizo kwa miaka mitano bila kutimiza masharti ya Mkataba.

Waziri Mpina akiwa Mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 5 hadi 6 Desemba 2017 alitembelea Huria (Ranchi) ya Kagoma Wilayani Muleba na kukutana na Mwekezaji AGRI RANCH ambaye anawekeza katika Ranchi tatu za Kagoma, Mabale na Kikurula na kutembelea  mifugo yake,  kukagua miundombinu aliyowekeza katika Ranchi  ya Kagoma  pia na Kuongea na mwekeza ji huyo.

Baada ya kutembelea miundombinu katika Ranchi hiyo na kupata maelezo ya AGRI RANCH pamoja na Meneja Mkuu wa NARCO Profesa Philemon Wambura Waziri Mpina alitoa uamuzi kuwa anakubaliana na maamuzi ya NARCO ya kuvunja Mkataba na AGRI RANCH kwasababu Kampuni hiyo ilikiuka masharti ya Mkataba huo tangu mwaka 2012 ilipopewa Ranchi hizo tatu kuwekeza.

“Kuanzia sasa nakubaliana na maamuzi ya NARCO ya kuvunja Mkata ba na Kampuni hii kwani wamekiuka Mkataba tangu mwaka 2012 walipopewa Ranchi zetu kuwekeza. katika Mkataba huo AGRI RANCH ilitakiwa kujenga kiwanda cha kusindika nyama na machinjio ya kisasa lakini hadi sasa kwa miaka mitano hawajawahi kufanya lolote ,” alisisitiza Waziri Mpina.

Vilevile Waziri Mpina alisema kuwa AGRI RANCHI ilitakiwa kuilipa Serikali kiasi cha Shilingi bilioni tatu kila mwaka lakini hadi sasa haijawahi kulipa fedha hizo bali wamelipa kiasi kidogo sana katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba , kwahiyo kwa miaka mitano wanadaiwa kiasi cha shilingi bilioni 15 pia Kampuni hii  ilitakiwa kuwa na ng’ombe zaidi 25,000 katika Ranchi zetu lakini hadi sasa ng’ombe waliopo ni  4500 tu.

Aidha, Meneja Mkuu wa NARCO  Profesa Philemon Wambura alisema Kampuni ya AGRI RANCH imekiuka mashariti yote ya mkataba na tayari NARCO wameionya mara nyingi kampuni hiyo na kukaa nao kwa majadiliano mara kwa mara laikini AGRI RANCH hawakutekeleza chochote ambapo NARCO ikaamua kuvunja Mkatana kutoa “notice” ya mwekeza huyo kuondkoa tangu mwaka 2014 lakini bado ameendelea kukaidi hadi sasa.

Baada ya maelezo hayo Waziri Mpina alisema kuwa Serikali haiwezi kuendelea kwavumilia wawekezaji waongo ambao hawana mitaji lakini wanaidanganya Serikali na kutumia Raslimali za wananchi isivyopaswa  ambapo aliwaagiza NARCO kufanya tathimini ya kina juu ya hasara iliyosababishwa na Kampuni hiyo na kuilipa Serikali ikiwa ni pamoja na Bilioni 15 walizokwepa kulipa awali.

Katika hatua nyingine Waziri Mpina alimwagiza Meneja Mkuu wa NARCO Profesa Philemon Wambura kuhakikisha kuwa ndani ya Siku sana awe amepeleka Meneja Katika Ranchi ya Kagoma na walinzi wa kuilinda Ranchi hiyo isivamiwe wakati mwekezaji anaendelea kuondoa mifugo yake katika Ranchi hiyo.

Pia kuendelea kuweka mazingira mazuri  kwa wawekezaji  wa  Vitalu vya ufugaji Mkoani kagera Waziri Mpina alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango kwa kushirikiana na NARCO kubaini mipaka halisi ya vitalu na kutoa mapendekezo juu ya wananchi waliovamia vitalu hivyo ili kuondoa kabisa tatizo la uvamizi wa vitalu vya wawekezaji.

Akijitetea mbele ya Waziri Mpina Meneja wa Kampuni ya AGRI RANCH Bw. Rutagwelela Mbelwa alisema hawakujenga kiwanda cha nyama kutokana na ng’ombe aina ya ankole kutokuwa na nyama inayokidhi viwango kwahiyo kampuni hiyo ilijikita katika ufugaji wa ng’ombe aina ya borani ili kupata nyama inayokidhi viwango vya kimataifa ndipo kiwanda kingejengwa.

Pili  Bw. Mbelwa alisema kuwa Kampuni yake AGRI RANCH inaomba kubaki na na Ranchi moja ya Kagoma lakini Mabale na Kikurula Serikari inaweza kuzitaifisha ambapo maelezo hayo hayakubatilisha msimamo wa Waziri Mpina na kusisitiza kuwa waondoe mifugo yao mara moja katika Ranchi za Serikali.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.