- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
Akiongea na Watumishi wa Idara ya Ardhi Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Wakuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa Mkoa katika ziara ya siku moja Mkoani Kagera Machi 14, 2020 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesisitiza kuwa sasa Wizara yake inahamia Mkoani humo ili kumaliza kero za wananchi kuhusu ardhi.
“Gharama za kupata hati ya ardhi Mkoani Kagera zilikuwa kubwa mno kutokana na gharama ya kusafiri kwenda Mwanza kufuatilia hati ilikuwa kubwa kuliko gharama za kupata hati yenyewe jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma molari wa wananchi kupima ardhi zao ili wapate hati. Mhe. William Lukuvi.
Mhe. Lukuvi alisema kuwa ili kuhakikisha kero zote za ardhi zinakwisha tayari amewateua Kamishna Msaidizi wa Ardhi, Mkurugenzi wa Upimaji wa Ramani, Msajili wa Hati, Mthamini pamoja na Maafisa wao ili kuhakikisha wananchi wanapata hati mkoani Kagera badala ya kusafiri kwenda kuzifuata Mwanza na nyaraka za hati za Wananchi 16,000 ambao wamepima ardhi zao zilizokuwa Mwanza alisema zitahamishiwa Kagera.
Katika Kikao hicho Mhe. Lukuvi alisema kuwa mwishoni mwa mwezi huu Machi 2020 Wizara yake inahamia rasmi Mkoani Kagera ili kumaliza kero za muda mrefu kuhusu upatikanaji wa hati za ardhi za wananchi. “Kuwa na ardhi isiyopimwa hata kama umejenga jengo lenye thamani kubwa unakuwa na mali mfu lazima tupange na kuzipima ardhi za wananchi.” Alisistiza Mhe. Lukuvi
Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwakumbusha Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuwa mamlaka ya upangaji wa ardhi ni jukumu na si jukumu la Waziri. “Pangeni ardhi zenu kwa matumizi sahihi na kuwamilikisha wananchi, nawaletea watendaji haya ni matrekta mapya yatumieni ipasavyo hata maeneo ya vijiji yanayoonekana kukua yapimeni na kuwapa wananchi hati.” Alipigilia msumali Mhe. Lukuvi
MwishoWaziri Lukuvi alisistiza juu ya wananchi kupata hati katika Halimashauri zao bila kusafiri kufuatilia hati hizo ambapo aisema kuwa kama ni mwananchi wa Wilaya ya Ngara atapata hati yake hukohuko Ngara .
Pia upatikanaji wa hati katika mkoa utapunguza na kero kwa taasisi za kibenki kwa wateja wao wanaokopa kutumia hati hizo kwani walikuwa wanalazimika kusafiri kwenda Mwanza kuthibitisha. Ofisi za Wataalam wote wa Idara ya ardhi zitakuwa katika majengo ya ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.