• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Waziri Mkuu Awasili Mkoani Kagera na Kutoa Wito Kwa Wakandarasi Wazawa Kukamilisha Miradi Kwa Wakati Wanayopewa na Serikali Bila Visingizio

Posted on: February 20th, 2019

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amewasili Mkoani Kagera leo tarehe 20 Februari, 2019 kwa ziara ya siku mbili ambapo mara baada ya kuwasili Nyakanazi Wilayani Biharamulo akitokea Mkoani Kigoma aliongea na wananchi katika Mkutano wa hadhara na kuwaeleza wananchi jinsi Serikali inavyoendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika Mkoa wa Kagera.

Katika Mkutano wa hadhara Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa wito kwa Sekta binafsi pale zinapoaminiwa na Serikali na kupewa miradi ya kutekeleza kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa na kukamilika kwa wakati. Waziri Mkuu alisikitishwa na Mkandarasi anayeendelea kujenga barabara ya Nyakanazi Kibondo Kilometa 50 (Nyanza Roadworks Ltd) kutomaliza barabara hiyo kwa wakati pamoja na  kuwa Serikali tayari imeilipa Kampuni hiyo ya Kitanzania fedha za kujenga barabara hiyo.

“Sijaridhishwa na kiwango cha ujenzi wa barabara ya Nyakanazi Kigoma, jana nimeongea na Mkandarasi anasingizia hana malori na hana vifaa wakati tayari tumemlipa fedha. Serikali imekuwa ikakaa na Sekta binafsi na kuongea nao na kilio chao kilikuwa ni kuaminiwa na kupewa kazi na Serikali lakini walio wengi hawatekelezi miradi hiyo na kuimaliza kwa wakati mfano hii barabara imeanza tangu mwaka 2014 mpaka sasa bado Mkandarasi anajikongoja tu.” Alieleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa kama Mkandarasi huyo atashindwa kukamilisha barabara hiyo ifikapo mwezi Aprili 2019 Serikali itamfukuza kazi. Barabara ya Nyakanazi Kibondo kilometa 50 ilianza kujengwa mwaka 2014 na kulingana na Mkataba ilitakiwa kuwa imekamilika ifikapo Juni 2016 lakini mpaka sasa bado haijakamilika.  Aidha gharama za ujenzi wa barabara hiyo ni bilioni 45.986 mpaka kukamilika hadi kiwango cha rami.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia aliwaeleza wananchi wa Nyakanazi waliokusanyika kumsikiliza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha inakamilisha kwa asilimia 90% miradi yote ya maendeleo ambayo ilihaidiwa wakati wa uchaguzi mwaka 2015 katika sekta za Elimu, Maji, Afya na Miundombinu ya barabara na umeme kwa wananchi ifikapo mwaka 2020.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaeleza wananchi wa Nyakanazi kuwa Serikali tayari imetabiri eneo la Nyakanazi kuwa litakuwa mji mkubwa hapo baadae kutokana na eneo hilo kukaa kimkakati  ambapo kuna barabara kuu za kwenda nchi jirani za Rwanda , Burundi na Serikali tayari imeamua kupaboresha Nyakanazi kwa kutoa fedha shilingi bilioni tatu  kujenga miundombinu mbalimbali ya kimkakati ili kuliandaa eneo hilo kuwa mji mdogo na wananchi wafanye biashara na na Serikali kuingiza mapato.

“Tayari mkataba umesainiwa kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo na Wizara ya Fedha ili ujenzi uanze na tunatarajia kujenga Kituo kikubwa cha Mabasi, Kituo cha kuegesha magari makubwa, Soko kubwa la kisasa, na Jengo kubwa la maduka na kituo kikubwa cha ukaguzi. Fedha tayari zipo na kinachosubiriwa ni kutangaza tenda. Tunataka Nyakanazi pabadilike kwa kasi kubwa na wananchi wanufaike na eneo hili la kimkakati.” Alisisitiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwakemea viongozi wa Wilaya ya Biharamulo kuacha malumbano na ugomvi kati yao na wawe mfano kwa watumishi na wananchi wanaowaongoza na kushikamana na kushirikiana kuleta maendeleo kwa wananchi. Waziri Mkuu aliwaonya viongozi hao na kusema kuwa kama hawataacha ugomvi wao na malumbano atamshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano aangalie upya uteuzi wao upya.

Mwisho Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa Halmashauri ya Biharamulo kuhakikisha wanasimamia na kukusanya mapato ya Serikali ipasavyo. Pia aliwakumbusha wananchi wa Nyakanazi kuhakikisha wanakuwa wazalendo kwa kutumia mfumo wa nyumba kumi za usalama kuimarisha ulinzi na usalama hasa kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ambao wamekuwa wakija nchini na kufanya vitendo vya uharifu.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.