• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Auagiza Uongozi na Jeshi la Polisi Mkoani Kagera Kukomesha Magendo ya Kahawa Mara Moja Wilayani Kyerwa

Posted on: October 7th, 2018

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa aendelea na ziara yake Mkoani Kagera Wilayani Kyerwa na Karagwe ambapo Kyerwa alitembelea Chama cha Msingi Nkwenda na Kumuagiza Mkuu wa Mkoa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanachukua hatua mara moja kukomesha magendo ya Kahawa Wilayani Kyerwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa onyo kali kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kyerwa kuhakikisha anakomesha magendo ya Kahawa na kuacha tabia ya kushiriki kusindikiza kahawa za magendo kutoroshwa kuelekea nchi jirani wakati jukumu la Jeshi la Polisi ni kudhibiti magendoi ya kahawa.

“OCD (Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kyerwa) wewe na baadhi ya Maafisa wenzako mnalichafua Jeshi la Polisi kwa kusindikiza kahawa za magendo, acha tabia hiyo mara moja tutakuvua vyeo na kusimamisha kazi wakati bado familia yako inakutegemea. OCD simamia kahawa, OCD simamia Kahawa, OCD simamia Kahawa.” Alimuonya Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kyerwa Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa.

Aidha, katika hatua nyingine alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kwa kushirikiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustine Olomi kuhakikisha wanashughulika na Wilaya ya Kyerwa kwa kukomesha Magendo ya Kahawa katika Wilaya ya Kyerwa ili kahawa iuuzwe kwa mfumo halali wa Ushirika na kumnufaisha mkulima moja kwa moja.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alirudia kauli ya Serikali alaiyoitoa Oktoba 6, 2018 akiwa Manispaa ya Bukoba  ya kuuboresha mfumo mpya wa kunuanua kahawa Mkoani Kagera na kusema kuwa  kuanzia msimu ujao wa mwaka 2019/2020 Mnada wa Kahawa utafanyika Mkoani Kagera ili kupunguza gharama za makato kwenye fedha za Wakulima.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwahakikishia wananchi ambao tayari wamekusanya kahawa yao kwenye Chama Kikuu cha Ushirika KDCU Limited na hawajalipwa fedha zao kuwa  watalipwa kwani  Benki ya Maendeleo ya Kilimo tayari imetoa fedha kwa chama hicho ili kuwalipa wakulima hao. Pia alikiagiza Chama cha Msingi Nkwenda ambacho alitembelea kiwanda chake cha Kukoboa kahawa kuwa kitangaze mara moja mnada wa kahawa ambayo tayari wameikusanya ili kuwalipa Wakulima.

Vile vile Mbunge wa Kyerwa Innocent Bilakwate na Mbunge wa Viti Maalum Oliver Semguruka waliwasilisha kero za wananchi katika Sekta za Maji, Afya, Elimu na Ardhi ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi katika maeneo mbalimbali nchini mfano kwa kuongeza ujenzi wa vituo vya afya, madawa na watumishi.

Aidha, katika Sekta za Maji na Ardhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwahidi wananchi wa Wilaya ya Kyerwa kuwa atawatuma Mawaziri wa Sekta hizo kwenda Wilayani Kerwa  kusikiliza kero hizo kuzitatua na kuchukau hatua kama kutakuwa na uzembe uliofanyika kwa kusababishwa na Watendaji  wa Serikali.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alitembelea kiwanda cha KADERES cha kukoboa kahawa chenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.5 kinachomilikiwa na Mwekezaji Leonard Kachebonaho Wilayani Karagwe na kupongeza juhudi za mwekezaji huyo za kuajili wananchi wenzake na kupunguza uhuhitaji wa ajira kwa vijana nchini.

Kiwanda hicho cha KADERES kinakoboa kahawa na kuzipanga kwa madaraja, pia kinaajili wananchi wazawa 30 hadi 200 na kinawahudumia wakulima 1800 ambapo kwa msimu huu wa mwaka 2018/2019 kitaanza kulipa wakulima waliokusanya kahawa yao kwa kiasi cha shilingi 1,700/=  kwa kilo na baadae wakulima hao watalipwa shilingi 100/= na kukamilisha jumala ya shilingi 1,800/=.

Mara baada ya kukitembelea kiwanda hicho Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuunga Mkono wawekezaji katika Sekta ya Viwanda kwa kusema kuwa viwanda vina mambo makuu muhimu matatu. Kwanza kuboresha mazao mbalimbali ya kilimo na biashara kwa kuyaongezea thamani, Pili viwanda vinpunguza sana tatizo la ajira kwa kuajili wananchi wengi kwa wakati mmoja.

Tatu, ni kutoa fursa kwa wananchi wazawa Watanzania kujifunza teknolojia na ujuzi wa kuendesha viwanda wazawa wenyewe bila kutegemea wataalam kutoka nje ya nchi. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimalizia kuwa Viwanda vimeondoa vijiwe vya vijana kwa kutoa ajira nyingi kwa vijana nchini. Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa alimalizia ziara yake Wilayani Karagwe kwa kuongea na wananchi katika Mkutano wa hadhara Uwanja wa Changarawe Kayanga.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.