• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Mhe. Pinda Akizungumza na Wanafunzi na Watumishi wa Chuo Hicho Mkoani Kagera.

Posted on: February 26th, 2018

Waziri Mkuu Mstaafu Aagiza Chuo Kikuu Huria Tanzania Kuanzisha Kozi Fupi Kwa Watumishi Ili Kuendana na Sera ya Viwanda

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania aagiza chuo hicho kuandaa kozi fupi kwa kada mbalimbali ili kuwawezesha watumishi wa umma kuendana na utekelezaji wa Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Serikali ya Viwanda.

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda aliyasema Hayo alipofanya ziara Mkaoni Kagera Februari 23, 2018 ili kukagua miundombinu na maendeleo ya Chuo Kikuu Huria Tanzania Tawi la Kagera ambapo alipongeza juhudi za zinazoendelea kuchukuliwa  kukiendeleza chuo hicho Tawi la Kagera.

Akiongea na wanafunzi, watumishi , uongozi wa chuo hicho na uongozi wa Mkoa wa Kagera katika viwanja vya Chuo Kikuu Huria Tawi la kagera  Migera Manispaa ya Bukoba  Waziri mkuu Mstaafu Pinda alisema chuo hicho ni Chuo cha wananchi na kinawafuata wananchi badala ya wananchi kukifuata chuo.

“Chuo hiki ni chuo cha wananchi kwani hakimlazimishi mwananchi kuacha familia yake au mtumishi kuacha majukumu yake ya kazi kwenda kusoma mbali bali mwananchi yeyote atasoma mahali popote alipo kwan i Chuo chetu kina matawi kila Mkoa na kwa sasa kila Wilaya.” Alifafanua Mhe, Pinda.

Mhe. Pinda alisema pia kuwa tayari amemwagiza Makamu Mkuu wa Chuo  Profesa Elphazi Bisanda na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Profesa Rwekaza Mkandara kuhakikisha wanaangalia uwezekano wa kuandaa kozi fupi kwa watumishi wa umma kama Watendaji wa kata juu ya kusimamia sera ya viwanda pia kozi hizo zitawafanya watumishi waendane na wakati wa Sayansi na Teknolojia.

Mhe. Pinda alitoa mfano wa Nchi ya Korea Kusini kuwa Vyuo Vikuu Huria nchini humo vilisaidia sana katika kuwanoa watumishi ambao  baadae walikuja kutoa mchango mkubwa katika mapinduzi ya kiuchumi na nchi hiyo kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika Sayansi na Teknolojia .

Katika Kuhitimisha Mhe. Pinda alimwomba Mkuu wa Mkoa Kagera kuhakikisha watumishi wa umma wanaruhusiwa kutumia fursa ya chuo hicho kujiendeleza kielimu, pili aliwaomba wanafunzi wa chuo hichio kusoma kwa bidii ili kupambana na ushindani wa vyuo vingine na ikiwezekana wasome kwa muda muafaka kama vyuo vingine pia mfano badala ya kusoma shahada ya kwaza kwa zaidi ya miaka mitatu iwe mitatu tu.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Huria Tanzania Prof. Elphazi Bisanda alisema kuwa Mkoa wa Kagera una mwitikio mzuri wa wanafunzi wanaojiandikisha kusoma katika chuo hicho. Ambapo alihaidi kuwa matawi zaidi yatazidi kufunguliwa ili chuo kiwafutae wananchi. Tawi jipya linalotarajiwa kufunguliwa ni Katika Wilaya ya Biharamulo.

Prof. Bisanda alihaidi kuwa uongozi unaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya Chuo Kikuu Huria Tawi la Kagera ili miundombinu hiyo iwe na hadhi ya chuo Kikuu. “ Tunaendelea kuboresha miundombinu ya hapa kadri tunavyopata fedha na nina uhakika kuwa tutaweza kufika tunapopataka. Alifafanua Prof, Bisanda

Naye mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akimshukuru Mhe. Pinda kwa kuja Kagera kutembelea Chuo Kiku Huria Tawi la Kagera alisema Mkoa wa Kagera ni wa tatu kutoka mwisho kwa umasikini lakini kwa sasa kuna juhudi kubwa zinafanyika ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujiendeleza ili kuutoa Mkoa kwenye nafasi hiyo ya tatu toka mwisho.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.