• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Waziri Ndalichako Asema Kila Kitu Kimekamilika Serikali ya Watu wa China Yatakiwa Kuanza Ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi Mkoani Kagera

Posted on: January 28th, 2019

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako afanya ziara ya siku moja Kagera na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoani Kagera ili kuona ni hatua gani imefikiwa katika ujenzi huo ili vianze au viendelee kutoa huduma fanisi  kwa wananfunzi wanaohitimu Elimu ya Msingi na Kidato cha nne.

Profesa Ndalichako akiwa Mkoani Kagera Januari 26, 2019 alitembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Mkoa wa Kagera katika Kijiji cha Burugo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kilometa chache kutoka Bukoba Mjini.

Profesa Ndalichako  alitembelea Burugo kwenda kujihakikishia kama jukumu la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Serikali ya Mkoa wa Kagera limekamilishwa la kufikisha miundombinu ya Barabara, Maji na Umeme katika eneo hilo ili Serikali ya Watu wa China iweze kuanza ujenzi mara moja.

Mara baada ya kufika katika eneo la Burugo akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera alikagua miundombinu ya Barabara, Maji na Umeme iliyofikishwa katika eneo hilo na Serikali na kusema kuwa sasa jukumu la Serikali limekamilika kwa asilimia 100% na kilichobaki ni Serikali ya Watu wa China kuanza ujenzi mara moja.

“Sisi Serikali ya Tanzania tumekamilisha kila kitu kilichotakiwa kwa upande wetu kilichobaki sasa ni Serikali ya Watu wa China kuanza ujenzi mara moja katika eneo hili ambapo ujenzi huo utagharimu jumla ya Shilingi bilioni 22.4 na chuo hiki kikamilika kitakuwa kinapokea jumla ya wanafunzi 800 wa fani mbalimbali za ufundi stadi kwa wakati mmoja.” Alifafanua Profesa Ndalichako.

Ikumbukwe kuwa Serikali ya Watu wa China mwaka 2015 ilihaidi kutoa shilingi bilioni 22.4 kwa ajili ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Rais Jakaya Kikwete akaagizachuo hicho kijengwe Mkoani Kagera. Ujenzi wa chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Kagera unatarajia kuanza mwezi Mei 2019 mara baada ya taratibu za kusaini mikataba na manunuzi kukamilika.

Katika hatua nyingine Profesa Ndalichako alitembelea ujenzi na ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi Wilayani Karagwe (Karagwe Development Vocational Training Center KDVTC) ambapo Serikali ilitoa Shilingi bilioni 4.6 ili Chuo hicho kiboreshwe miundombinu yake ya majengo na kujenga majengo mapya ili kiweze kukidhi viwango vya kupokea wanafunzi wengi zaidi.

Ujenzi wa Chuo cha KDVTC unaosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na ngazi ya ujenzi ipo katika hatua ya msingi jambao ambalo lilimfanya Profesa Ndalichako kumwagiza Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Kagera Mhandisi Salum Chanzi anayesimamia ujenzi huo kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa wa mwaka mmoja ifikapo Julai 2019.

Aidha, katika hatua nyingine Profesa Ndalichako alitembelea Shule ya Sekondari Bukoba na kukagua majengo yaliyoezuliwa na upepo na upepo mkali usiku wa kuamkia tarehe 17.10.2018 pia majengo hayo yakiwa  yameathiriwa na Tetemeko la Ardhi la Septemba 10, 2016 na kuhaidi kuendelea na ufuatiliajia wa upatikaji wa fedha ili shule hiyo iweze kukarabatiwa na wananafunzi waliohamishiwa Shule za Sekondari Omumwani na Ihungo waweze kurejea na kuendelea na masomo katika Shule hiyo.

Kwa upande wa maendeleo ya Elimu katika Mkoa wa Kagera Profesa Ndalichako mara baada kupokea taarifa ya mkoa ya maendeleo ya elimu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliupongeza uongozi na wananchi wa Mkoa wa Kagera kwa kuendelea kufanya vizuri na kuwa katika nafasi kumi bora za mwanzo katika mitihani mbalimbali.

Pia Profesa Ndalichako alisema kuwa mkoa unatakiwa kuzifanyia kazi haraka changamoto za miundombinu katika shule mfano uhaba wa matundu ya vyoo na mlundikano wa wanafunzi katika madarasa. “Chanagamoto ya vyoo inatakiwa kufanyiwa kazi haraka ukizingatiwa kuwa mkoa huu una mvua nyingi jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha ya watoto wawapo shuleni.” Alisisitiza Profesa Ndalichako.

Mkoa wa Kagera umeendelea kufanya vizuri katika matokeo mbalimbali na kuwa miongoni mwa mikoa kumi bora inayoshika nafasi za juu ambapo kwa miaka mitatu mfurulizo 2016, 2017, na 2018 Mkoa wa Kagera uliongoza kwa kushika nafasi ya kwanza Kitaifa kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara katika Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Nne.

Matokeo ya Darasa la Saba Kitaifa mwaka 2016 Kagera ilishika nafasi ya 5, Mwaka 2017 nafasi ya 3 na mwaka 2018 nafasi ya 5 kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Katika Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili Kitaifa  kwa mwaka 2016 Kagera ilishika nafasi ya 4, Mwaka 2017 nafasi ya 6 na mwaka 2018 nafasi ya 7 kati ya mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani.

Aidha, Katika Matokeo ya Mtihni wa Taifa wa Kidato cha nne Mkoa wa Kagera kwa mwaka 2016 ilishika nafasi ya 3, Mwaka 2017 nafasi ya 9 na mwaka 2018 nafasi ya 8 Kitaifa kati ya mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani. Shule ya Kemebos iliyopo Manispaa ya Bukoba ilishika nafasi ya 2 Kitaifa mwaka 2018.

Pamoja na Mkoa wa Kagera kufanya vizuri katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2018 lakini Shule ya Sekondari Rwemondo iliyopo Wilayani Missenyi ilishika nafasi ya 4 kwa shule kumi za mwisho jambo ambalo linapelekea kengere kulia kwa uongozi wa Wilaya pia na Mkoa kuiangalia shule hiyo kwa jicho la tatu.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.