- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
Mkoa wa Kagera wafungua fursa za maendeleo katika kipindi cha pili cha Awamu ya Tano ya Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni baada ya kuwa mkoa wa kwanza nchini kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ziara ya kikazi tangu uchaguzi mkuu kukamilika Oktoba 28, 2020.
Ziara ya kikazi ya siku mbili (Januari 18 hadi 19, 2021) ya Rais Magufuli imeuacha Mkoa wa Kagera katika hali ya matamanio ya wananchi wake kuendelea kuchapa kazi ili kuifikisha Kagera kwenye ngazi ya juu ya kiuchumi na hayo yanatokana na kusikia na kuona kwa macho nini Serikali ya Awamu ya Tano inafanya, na inatarajia kufanya nini ili Kagera ipae kiuchumi.
Rais Magufuli Kutelea Nini Kagera?
Katika ziara yake Mkoani hapa Rais Magufuli alizindua shule ya Sekondari Ihungo ambayo imejengwa upya na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 10.9 baada ya majengo ya shule hiyo kuharibiwa kwa kiwango kikubwa na Tetemeko la Ardhi Septemba 10, 2016 sasa shule hiyo yenye majengo yenye viwango vya hadhi ya Chuo Kikuu inahudumia wanafunzi kutoka Kagera na nchi nzima.
Pili, Rais Magufuli aliweka jiwe la Msingi katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Kagera kinachojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 22. Chuo hicho kikamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wa kozi ndefu 800 na kozi fupi za ufundi stadi 1600 jumla ya wanafunzi 2400 kwa mwaka.
Hii ni fursa kubwa ya kiuchumi ukiachana na Ujenzi wa Chuo hicho cha Ufundi Stadi VETA Kagera lakini manufaa kwa wananchi wa Kijiji cha Burugo pale kinapojengwa chuo hicho watanufaika kiuchumi kutokana mwingiliano mkubwa wa watu, tayari Rais Magufuli ameagiza wananchi hao wapatiwe huduma za maji, umeme, na kupimiwa ardhi zao. Ajira tayari wananufaika nazo katika ujenzi unaoendelea katika eneo lao.
Tatu, kutokana na madini ya nickel kuwa na uhitaji mkubwa duniani kwa sasa na madini hayo yenye kiwango cha ubora duniani yanapatikana mkoani Kagera Kabanga Wilayani Ngara, Rais Magufuli aliona ni muhimu mkataba wa uchimbaji wa madini hayo wenye thamani ya Dolla za Kimarekani Milioni 664 sawa na Shilingi Trioni 1.5 ambayo utafiti wake ulianza mwaka 1976 usainiwe ndani ya mkoa wa Kagera Bukoba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya LZ NICKEL LIMITED.
Pamoja na kuwa Taifa la Tanzania litanufaika na uchimbaji wa madini ya Nickel lakini kipaumbele cha Serikali ni kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera hasa wanaopakana na mgodi wa Kabanga Nickel Wilayani Ngara ambao watapata manufaa mengi ikiwemo ajira katika mgodi huo, tenda mbalimbali, uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbali vitapata soko aidha, Rasi Magufuli aliwasisitiza wananchi hao kuzalisha chakula kwa wingi kwani neema inakuja.
Nne, Katika kuhakikisha wafugaji wanapata soko la maziwa wanayoyazalisha kutokana na mifugo yao Rais Maguli aliweka jiwe la msingi katika Kiwanda cha kusindika maziwa na vyakula vya mifugo chenye thamani ya shilingi bilioni 8.9 Kiyanga Wilayani Karagwe ambapo kiwanda hicho kikikamilika kitakawa na uwezo kusindika lita 10,000 za maziwa kwa siku na tani 20 za vyakula vya mifugo ambapo kinategemewa kuzalisha ajira za watu zaidi ya 400.
Je Rais Magufuli Ktuachaje Kagera?
Rais Magufuli kabla hajaondok Kagera katuachia miradi itakayoendelea kuchochea ukuaji wa kiuchumi katika Mkoa, katika sekta ya usafiri na usafirishaji Rais Magufuli katuachai kilomita 213 za barabara kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami. Barabara ya Rusahunga- Rusumo Km 92 kujengwa upya, Barabara ya Bugene- Kasulo Kilometa 120 kujengwa kwa kiwango cha lami Kilometa 60 kati ya Kilometa 120.
Zingine ni barabra ya kutoka Kyerwa kuelekea Wilayani karagwe Kilometa 110 itajengwa kwa kiwango cha lami kwa kilometa 50 kutokea Wilayani Kyerwa. Barabara inayoelekea katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Kagera Kilometa 10 kujengwa kwa kiwango cha lami na Barabara inayoelekea Katika Shule ya Sekondari Ihungo Kilometa moja kujengwa kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Bukoba. Aidha, daraja la Kitengurelitakamilika ifikapo Juni 2021 kuziunganisha Wilaya za Karagwe na Missenyi kuendelea kuchochea ukuaji wa uchumi.
Rais Magufuli kauacha ujumbe kwa wananchi Kagera wakiongozwa na watendaji wa Serikali yake kuhakikisha wanachapa kazi kwa kujituma ili kuleta maendeleo ya haraka katika mkoa wa Kagera . Vile vile kuhakikisha huduma za kijamii kwa wananchi zinapatikana kwa wakati nazo ni kama maji, umeme, na huduma za afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.