- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wednesday 11th, September 2024
@Kagera
Katika kikao cha Mamlaka ya Vizazi na Vifo RITA Kagera yajiwekea malengo ya usajili wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wenye stahiki za msingi na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kupitia mpango maalumu wa usajili wa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.
Akiitoa taarifa fupi Mariam Nkubwa, mratibu wa mkakati wa usajili wa watoto walio chini ya miaka mitano kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati akiongea na viongozi mbalimbali katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa, Manispaa ya Bukoba amesema kuwa zoezi hilo linalenga kuwasajili watoto hao kwa kuwafuata katika maeneo yao huku akisisitiza kuwa mpaka sasa ni asilimia 14.2 tu ya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano waliosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa mkoani Kagera.
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Ndg. Toba Nguvila amewataka viongozi mkoani humo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa wa RITA ili kuhakikisha kuhakikisha watoto wote waliokidhi vigezo wanasajiliwa.
Sambamba na hilo, amewaonya viongozi kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuepuka kulitumia zoezi hilo kama sehemu ya kujipatia kipato kwani zoezi hilo litatolewa la bure na atakayebainika kutoza pesa katika zoezi hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
"Sitegemei kiongozi yeyote mkoani Kagera kukwamisha zoezi hili kwa namna yoyote hile, tuhakikishe kila mtoto mwenye vigezo anapata haki yake ya kusajiliwa na kupewa cheti lakini pia nasisistiza suala la uahamiaji haramu lisiwekikwazo cha kukwamisha zoezi hili"ameeleza Ndg Nguvila
Ndg. Brenda Joshua Kileo, meneja wa usajili na utambuzi kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), alisema kuwa katika zoezi hilo watakuwa sambamba na maafisa wa RITA kuendelea kufanya utambuzi uhusani kwa ambao watakuwa hawajapata namba ya NIDA ili kuhakikisha wote wanaostahili wanapata namba hizo na ambao hawatakidhi vigezo watapewa fomu maalumu na wataalamu wa RITA itakayoenda uhamiaji ili kusaidia wazazi hao kusajili watoto wao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa