- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Shughuli za Biashara Namba 14 ya mwaka 2007 (Business Activities Registration Act - BARA No 14 of 2007) ya biashara inatakiwa kusajiliwa na kupewa cheti cha kudumu ili kutambulika kuwa ni biashara rasmi. Usajili wa jina la biashara umekuwa ukifanywa na Wakala wa Usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara Tanzania ambaye ni BRELA. Wakala huyu ndiye mtekelezaji Mkuu wa Sheria ya BARA na 14 ya mwaka 2007.
Usajili wa MAKAMPUNI hufanywa na BRELA chini ya sheria ya makampuni namba 12 ya mwaka 2002 (Company Act No 12 of 2002). Ili kusajili kampuni ya aina yeyote ile unashauriwa kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kitengo cha Biashara ili uweze kushauriwa namna bora ya kufanikisha usajili kwa wakati. Mahitaji muhimu ya usajili wa kampuni ni kama ifuatavyo:-
• Kuandaa/Kufikiria jina la kampuni;
• Kuandaa “Memorundam and Artcles of Association”;
• Kujaza fomu za usajili namba 14a na 14b;
• Kuandaa ada ya usajili wa kampuni inayotegemea mtaji wa kampuni;
• Kuwasilisha nyaraka husika kwa Msajili na Kupata cheti cha usajili wa kampuni.
Kumbuka, BRELA iko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Mamlaka nyingine zilizoko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ni SIDO, TBS na Wakala wa Vipimo (WMA-Weights and Measure Agency) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE).
Ada ya usajili wa Jina la Biashara ni shilingi za Kitanzania elfu sita tu 6,000/=. Kuna fomu maalum za kujaza ili kuweza kujisajili kama biasharar ya mtu binafsi au kama biashara ya ubia (watu zaidi ya mmoja mpaka 20). Fomu za maombi ya usajili wa Jina la Biashara zinapatikana katika tovuti ya Mkoa wa Kagera, na kwa maelezo zaidi ya msaada namna ya kusajili jina la biashara wasiliana na Ofisi ya Biashara Mkoa wa Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa