- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kuna makundi mawili ya leseni za biashara kwa mujibu wa sheria za leseni ya leseni za biashara namba 25 ya mwaka 1972 iliyofanyiwa maboresho mwaka 1982. Makundi hayo ni:
i) kundi la leseni zinazotolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri za Wilaya na Manispaa)
ii) kundi la pili ni leseni zinazotolewa na Wizara ya Viwanda na Bisahara mfano leseni za kufungua na kuendesha Klabu za Muziki za Usiku (Night Clubs) na leseni za kununua na kuuza nje ya nchi (Import and Export License).
Masharti ya kuomba leseni za biashara kwa makundi yote mawili ni kama ifuatavyo:-
• Cheti cha usajili wa Kampuni au jina la biashara (Certificate of registration/incorporation)
• Kama ni kampuni “memorandum and article of Association''.
• Cheti cha urai (Passport ya Tanzania) au cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo (affidavit).
• Mkataba wa jengo analofanyia biashara husika au hati ya umiliki endapo jengo ni lake.
• Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (TIN)
• Endapo wana hisa wa kampuni wapo nje ya nchi maombi yaambatane na hati ya kiwakili.
Pamoja na kukamilisha masharti hayo, ili kupata leseni siku za nyuma mwombaji alitakiwa kupitisha fomu ya maombi iliyojazwa katika Ofisi za mipango miji, ofisi za afya na hatimaye Ofisi za biashara tayari kwa kupata leseni husika baada ya kuwa wote wamekagua maeneo yao kitaalam na kujiridhisha. Hatua hiyo ilionekana kuwa na urasimu mwingi na kufanya ucheleweshaji wa kutoa leseni hatimaye biashara nyingi zilikuwa zikichelewa kuanzishwa. Ikiwa ni hatua za kurahisisha uanzishaji na uendeshaji wa biashara, sharti la kupitisha fomu ya maombi ya leseni katika ofisi za afya na mipango miji limeondolewa. Aidha, baada ya kukamilisha taratibu zote pamoja na nyaraka zote zinazohusika mwombaji itamchukua muda wa siku moja hadi tatu tu kuwa amepata leseni yake kutoka katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa alipoombea leseni yake.
Kwa kipindi kirefu ada za leseni kwa mujibu wa sheria zilikuwa kati ya shilingi 10,000 hadi 2,000,000 kutokana na aina ya leseni, eneo la biashara na aina ya biashara inayoombewa leseni. Wakati fulani ada hizo ziliondolewa na kwa kipindi kirefu leseni zilikuwa zikitolewa bure ili kurahisisha watu wengi zaidi kuhamasika na kuanzisha biashara ili kuiongezea serikali mapato kwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato.
Hata hivyo serikali katika bunge la bajeti la mwaka 2011/2012 imerudisha utaratibu wa ada za leseni za biashara na utaratibu huu utaanza kutumika rasmi Januari Mosi, 2012. Umetolewa muda wa kutosha kuzipa Halmashauri za Wilaya muda wa kujiandaa na kuweka miundombinu vizuri ili zoezi hili litakapoanza liende kwa kasi inayotarajiwa na kuleta matunda kwa serikali za mitaa ili kupunguza utegemezi kutoka serikali kuu.
Hivyo ni muhimu kwa kila mfanyabiashara kuhamasika na kusajili biashara yake ikiwa ni pamoja na kuikatia leseni ya biashara husika ili kufanya biashara kwa haki, uhuru na amani na kuchangia kikamilifu ujenzi na uimarishaji wa uchumi wa Mkoa wa Kagera na Taifa kwa ujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa