- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa Kagera Aagiza Mkandarasi Kukamatwa na Kufikishwa Ofisini Kwake Akiwa na Pingu Mikononi Baada ya Kuitia Serikali Hasara
Mkuu wa Mkoa wa Kagera aagiza Mkandarasi wa Kampuni ya MECCO aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa barabara zenye thamani ya shilingi bilioni saba na kukataa kusaini mkataba wa kuanza ujenzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kukamatwa na kufikishwa Ofisini kwake akiwa na pingu mikononi ili kutoa sababu za kuitia Serikali hasara.
Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu alitoa agizo hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika Mkoani Kagera Machi 8, 2018 ambapo katika kuwasilisha hoja Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Chief Karumuna kumuomba Mkuu Mkoa kumchukulia hatua Mkandarasi huyo baada ya kugoma kusaini mkataba wakati alishinda zabuni ya ujenzi wa barabara hizo.
Chief Karumuna alisema kuwa Manispaa ya Bukoba imepata hasara baada ya Mkandarasi kukataa kusaini mkataba wa kuanza ujenzi wa barabara zenye thamani ya shilingi bilioni saba na zabuni kutangazwa tena upya, pia alisistiza kuwa fedha hizo zilitolewa na Benki ya Dunia na utekelezaji wa miradi yake ni wa kipindi maalumu kwa hiyo Mkandarasi huyo amechelewesha muda wa utekelezaji.
Katika kikao hicho ambacho Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti aliwasistiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatengeneza barabara za mipakani ili kuimarsha ulinzi na usalaama wa mkoa na na chi kwa ujmla. Barabara hizo ni Bubale-Missenyi Runch- Kakunyu Kilomita 32.5, Bubale – Kamwema Kilomita 17.8 Wilayani missenyi na barabara ya Nyabishenge-Nyakanoni-Ibanda Game Reserve kilomita 15 Wilayani Kyerwa.
Vilevile Meneja wa Wakala wa Umeme na Ufundi (TEMESA) Mkoa wa Kagera ameagizwa na kikao hicho kusitisha mara moja tozo ya shilingi 80,000/= ya ukaguzi wa magari ya Serikali pale yanapotakiwa kukaguliwa ili yakatengenezwe baada ya wajumbe kuwasilisha sheria kikaoni inayoelekeza kuwa magari ya Serikali yanatakiwa kukaguliwa bure. Hadi Mkuu wa mkoa atakapopata walaka unaoruhusu kutoza magari ya Serikali.
Mkoa wa Kagera unahudumia barabara zenye mtandao wenye jumla ya kilomita 7,505.42 kati ya hizo, kilometa 675.46 ni barabara za lami, kilometa 2,791.56 barabara za changarawe na kilometa 4,038.96 zikiwa in barabara za udongo.
Mkoa wa Kagera kwa mwaka wa fedha 2017/18 uliidhinishiwa shilingi Bilioni 10,710.05 kwajili ya matengenezo ya kazi za barabara na ujenzi wa madaraja. Pia mkoa umeidhinishiwa shilingi bilioni 14,180.937 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara Kuu na Barabara za Mkoa kwa mwaka wa fedha 2017/18
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa wa Kagera amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka kumkamata na kumpeleka ofisini kwake kijana anayemtesa mama yake mzazi kwa kutaka kumnyanganya shamba lake na mama huyo ameshinda kijana huyo mara mbili Mahakamani.
“Mtafute kijana huyo na kumleta kwangu nijue ana matatizo gani ili tumsaidie maana atamuua mama yake, hana uchungu na mama yake mzazi. Mama huyoaliwasilisha kilio chake katika mkutano wa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. Lukuvi Wilayani Karagwe lakini kijana huyo bado anaendelea kumsumbua mama yake mzazi.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Kijuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa