- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Asherehekea Siku ya Wazee Duniani na Wazee wa Kituo Cha Kiilima-Bukoba
Kila tarehe Mosi Oktoba kila mwaka huwa ni Maadhimisho ya siku wa Wazee Duniani ambapo wazee hukumbukwa kwa michango yao mbalimbali hasa kwa kuyatumikia mataifa yao katika Nyanja mbalimbali wakati wa ujana wao.
Mkoa wa Kagera mwaka huu Octoba Mosi, 2017 uliadhimisha siku ya Wazee Duniani kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo kuwatembelea Wazee wanaotunzwa katika Kituo cha Wazee Kiilima na kuwazawadia mchele kilo 50 mafuta lita 10 na mbuzi kwaajili kuadhimisha siku hiyo.
Mkuu wa Wilaya Kinawilo akiongea na wazee hao wa Kiilima aliwaasa vijana kuiga ubunifu kutoka kwa wazee hao ambao walilitumikia Taifa la Tanzania kwa moyo mmoja na kuazisha viwanda mbalimbali nchini ili kuinua uchumi wa nchi.
Wazee hawa walianzisha mashamba ya kahawa,chai pia na kuanziasha viwanda vya aina mbalimbali nchini na kuviendesha lakini vijana wa siiku hizi hawafanyi kazi bali wanakaa vijiweni na kucheza mchezo wa pool . Nawaasa vijana mje katika kituo hiki mkakae na wazee na muwaulize mbinu walizokuwa wanazitumia katika kufanya kazi kama hizo. Alisistiza Mkuu wa Wilaya kinawilo.
Mara baada ya kupokea zawadi hizo kwa niaba ya Wazee wenzake Mzee Kaburi wazi aliishukuru Serikali kwa kuwakumbuka katika siku hiyo na kuwapa huduma za mara kwa mara. “Kwanza sisi wazee tuliopo hapa tulikuwa hatujui kama leo ni siku yetu Duniani lakini kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wetu Mhe. Kijuu ametukumbuka nasi tumefurahi sana tumeona tunavyothaminiwa. Alishukuru Mzee Kaburiwazi
Aidha, Mzee Kaburi wazi aliishukuru Serikali kwa kuwapatia Bajaji ya kuwasafirisha kwenda Hospitali kutibiwa ambapo hapo awali walikuwa wakipata tabu ya kwenda kutibiwa Hospitali kwasababu ya kukosa usafiri. Katika kituo cha Wazee Kiilima kuna jumla ya wazee 17 ambao watunzwa na Serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa