• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Afanya Ziara ya Siku Mbili Mkoani Kagera Kukagua Miradi ya Maendeleo Inayofadhiliwa ya Nchi Yake

Imewekwa : July 3rd, 2018

Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Jeroen Verheul  afanya ziara ya siku mbili Mkoani Kagera kukagua  miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na nchi ya Uholanzi katika kuinua uchumi na kipato cha wananchi ambao ni wakulima na wafugaji ili kuboresha maisha yao.

Mara baada ya kuwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera  Balozi Jeroem Verheul   alisema kuwa lengo la ziara yake Mkoani Kagera ni kuja kuona fursa za uwekezaji katika biashara ya bidhaa za kilimo na mifugo kati ya nchi yake na Tanzania hasa bidhaa zinazoweza kupatikana ili zikauzwe nchini Uholanzi kutoka Mkoani Kagera.

“Lengo kuu la kuja Mkoani Kagera ni kuona  fursa za uwekezaji na miradi ya maendeleo ambayo nchi yangu ya Uholanzi imekuwa ikiifadhili kama kilimo na ufugaji na  kuona namna bora ya kuboresha miradi hiyo ambayo inaweza kuwa kiunganishi kizuri kwa kufanya biashara ya kati ya nchi zetu mbili za Uholanzi na Tanzania hasa Mkoa wa Kagera. “Alieleza Balozi Jeroen Verheul 

Pia Balozi Jeroen alisema kuwa pamoja na kufadhili miradi ya Kilimo na Ufugaji katika Mkoa wa Kagera lakini pia nchi yake imefadhili na kujenga mradi wa kituo cha kufua umeme Wilayani Biharamulo  pamoja na mradi wa kujenga barabara kwa teknolojia iliyotengenezwa nchini kwao yenye unafuu wa gaharama za matengenezo ya barabara za vijijini ukilinganisha na matengenezo  ya kawaida.

Balozi Jeroen alisema teknolojia hiyo imetengenezwa nchini  Uholanzi na Wilaya ya Biharamulo ilichaguliwa kama sehemu ya majaribio ambapo imetengenezwa barabara ya kilometa moja kwa teknolojia hiyo ya kuchanganya maji, udongo na vifaa vingine ambapo barabara hiyo inaweza kudumu kuanzia miaka kumi na kuendelea bila matengenezo makubwa.

Ziara ya Balozi Jeroen Verheul  Mkoani Kagera na Wilayani Biharamulo ni pamoja na kutembelea na kukagua barabara iliyotengenezwa kwa teknolojia kutoka nchini Uholanzi ili kuona ufanisi wake, changamoto zilizopo na kuona namna bora ya kuboresha  teknolojia hiyo ili itumike katika kutengeneza barabara nyingi katika Halmashauri za Wilaya nchini.

Aidha, akimkaribisha Mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa  Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu alimshukuru Balozi Jeroen kwa kuamua kuutembelea Mkoa wa Kageara pia na ufadhili wa nchi yake wa kufadhili miradi mablimbali katka Sekta za Kilimo, Ufugaji, Nishati na Miundombinu inayolenga kuinua uchumi wa Wananchi wa Mkoa wa Kagera

Mkuu wa Mkoa Kijuu aliitaja baadhi ya miradi ambayo nchi ya Uholanzi imekuwa ikiifadhi Mkoani Kagera kuwa ni Mradi wa Kuendeleza Wafugaji Kagera (Kagera Livestock Development Programme - KALIDEP) pamoja na mradi wa kuendeleza wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa  vijijini.

Miradi mingine ikiwa ni pamoja na utoaji wa mbegu bora za ng’ombe wa kisasa wenye tija katika ufuaji wanaotoa maziwa kwa wingi  pamoja na kutoa madawa mbalimbali ya kupambana na magonjwa ya mifugo ili ufugaji katika mkoa wa uwe wa tija.

Mkuu wa Mkoa Kijuu alisema kuwa ni matarajio ya Serikali ya Mkoa kuwa siku moja maendeleo ya wakulima na wafugaji  katika Sekta za Kilimo na Mifugo Mkoani  Kagera polepole yatafikia maendeleo ya Waholanzi katika sekta hizo kutokana na ufadhili wa nchi hiyo katika kuhakikisha Wananchi wa Kagera wanapiga hatua ya maendeleo.

Balozi Jeroen katika siku yake ya kwanza Julai 2, 2018 Mkoani Kagera alitembelea Manispaa ya Bukoba kuona ufugaji wa Samaki katika mabwawa mradi uliopo chini ya Cartas Tanzania pia alitembelea mradi wa Wafugaji wadogo wa Ng’ombe wa Maziwa Wilayani Missenyi. Katika Siku yake ya pili Julai 3, alitarajiwa kutembelea Wilaya ya Biharamulo kukagua mradi wa kituo cha kufua umeme na mradi wa utengenezaji wa barabara za vijijini kwa teknolojia kutoka Uholanzi.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa