- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Rais Magufuli Azindua Rasmi Barabara ya Kyaka Bugene na Kuhaidi Kumalizia Kipande Kilichobaki Hadi Kasulo Ngara
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezindua rasmi barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa kilometa 59.1 iliyojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi bilioni 81.597 fedha zilizogharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania.
Rais Magufuli kabla ya kuzindua barabara hiyo ya Kyaka Bugene inayoziunganisha Wilaya mbili za Missenyi na Karagwe akiongea na wananchi alisema kuwa Serikali itaendelea kujenga kipande kilichobaki hadi Kasulo Wilayani Ngara na Kukamilisha jumla ya kilometa 183.1
Akitoa Taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Bw.Patrick Mfugale alisema kuwa barabara hiyo imesimamiwa na Watanzania baada ya Kampuni kutoka India iliyokuwa imepewa tenda ya kusimamia kushindwa kazi na na Serikali kuamua kuifukuza kazi.
Aidha, Bw. Mfugale alisema Kampuni hiyo kama ingefanya kazi mpaka mwisho wa kukamilisha barabara hiyo ingelipwa shilingi bilioni 4 lakini baada ya kuisimamishwa kazi na kupewa Watanzania ambao wamesimamia mpaka barabara kukamilika wamelipwa shilingi milioni 500 tu na kuokoa shilingi bilioni 3.5
Katika hatua nyingine Rais Magufuli aliwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Karagwe kuwa Serikali tayari imeiweka kwenye mpango wa ujenzi barabara ya Omugakorongo Mulongo ili ijengwe kwa kiwango cha rami kusudi wananchi waweze kufanya biashara na nchi jiarani ya Uganda.
Rais Magufuli akiongelea kero za wananchi wa Wilaya ya Karagwe alisema anajua kuwa kero ya maji Karagwe ni ya muda mrefu, ambapo alisema kuwa serikali imeainisha miji 17 na Karagwe ikiwemo na tayari Serikali imepata mkopo wa fedha Dola Milioni 500 kutoka nchi ya India na Wilaya ya Karagwe imetengewa Dola milioni 70 kwajili ya ujenzi wa mradi wa maji.
Pia Rais Magufuli alisema kuwa anajua kuwa Karagwe kuna Kero kubwa ya ardhi na kuwataka wananchi wote waliovamia vyanzo vya maji kuondoka mara moja na kuuagiza uongozi wa Mkoa kuhakikisha unasimamia kikamilifu na kuhakikisha unawatafutia maeneo mbadala ya kuishi.
“Jamani najua kuna sheria za mazingira lakini tukiamua kuzisimamia sheria hizo kwa karibu sana wananchi watakosa mahala pa kuishi, kama wananchi wanalima kandokando ya mito pengine wakati wa kiangazi wakitekeleza sera ya hapa kazi tu waacheni walime kwani hawazuii maji yaliyoletwa na Mungu kutirirka.” Alisistiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli alitolea mfano wa kijana mmoja aliyetoa kero yake kwake wakati akisalimia wananchi eneo la Kyaka Wilayani Missenyi akielekea Wilayani Karagwe kuwa kijana huyo alifukuzwa kando kando ya Mto Kagera wakati akilima mahindi yake. Rais Magufuli aliagiza kijana huyo kuendelea kulima na wananchi wengine isipokuwa watakaolima kwenye vyanzo vya maji ndiyo wachukuliwe hatua za kisheria.
Mwisho Rais Magufuli aliwapongeza Waandishi wa Habari kwa kazi kubwa wanayoifanya pia na vyombo vya habari kwa kufanya kazi kubwa ya kuwahaabarisha wananchi. Rais Magufulia ataendelea na ziara yake Wilayani Missenyi katika kiwanda cha Kagera Sukari kesho Novemba 8. 2017.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa