- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waandishi wa Habari Wakumbushwa Kuzama Chini Kwenye Jamii Kuandika Habari za Wananchi Zenye Vyanzo Sahihi
Waandishi wa Habari Mkoani Kagera wakumbushwa kwenda kwa wnanchi katika ngazi za chini kabisa hasa vijijini kuona matatizo ya wananchi na kuyaibua kwa kuandika habari zao zitakazolenga kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao na kuwatoa sehemu moja na kupiga hatua ya maendeleo kuliko kuandika habari za mijini tu ambazo zimezoeleka.
Hayo yalisemwa na Bibi Restuta Tibalila Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukoba alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo katika ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo huadhimishwa kila mwaka Mei 3 ambapo Waandishi wa Habari Mkoani Kagera walijumuika na wenzao Duniani kuadhimisha siku hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Bukoba Coop Manispaa ya Bukoba .
Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Bukoba iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya alivipongeza vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari Mkoani Kagera kwa kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo ya mkoa kwa kuandika habari ambazo zinaelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayolenga kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na mkoa kwa ujumla.
Vilevile Mkuu wa Wilaya Bukoba katika hotuba yake aliwashukuru wamiliki wa vyombo vya Habari kuendelea kufanya uwekezaji katika Vyombo vya Habari na masuala ya habari kama kuanzisha Redio za Kijamii na magazeti ambapo vinachangia sehemu kubwa kwa wananchi kupata habari mbalimbali zinazohusu mkoa wao na kwa wakati.
Aidha, Mkuu wa Wilaya katika hotuba yake aliwahakikishia Waandishi wa Habari kuwa Serikali Mkoani Kagera itaendelea kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari ili vitimize wajibu wake pia Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili wananchi ambao ni walaji wapate habari sahihi na zenye uhakika.
Katika Maadhimisho hayo yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Kagera pia walialikwa wadau mbalimbali ambao walishirikiana na waandishi wa Habari na Wamiliki wa Vyombo vya Habari kujadili na kuchambua mada isemayo “Uhuru wa Habari ni Chachu ya Uwajibikaji kwa maendeleo ya Mkoa.”
Wadau wakichangia mada hiyo waliwashauri Waandishi wa Habari kuhakikisha wanaandika habari zenye vyanzo vyenye uhakika na zenye maslahi mapana na jamii ili kubadili mtazamo wa jamii kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ya maendeleo.
Pia Waandishi wa Habari walishauriwa kuhakikisha wanazama chini katika jamii kuandika habari za wananchi wa kawaida au kuandaa vipindi ambavyo vinawagusa wananchi wa chini kabisa ambao wangependa kuona mabadiliko chanya katika maisha yao kwa kuelimishwa kupitia vyombo vya habari.
Chanagamoto kubwa waliopewa waandishi wa Habari ni kujiendeleza kielimu ili kuhakikisha wanankuwa na ufahamu wa kutosha na masuala mbalimbali ambayo wanayaandika au kuandaa vipindi juu ya masuala hayo pia kuendana na matakwa ya Sheria ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.
Kwasasa Mkoa wa Kagera unavyo vituo vya redio vipatavyo tisa, Kasibante, Fadeco, Karagwe, Shinuz, KCR, Vision, Kwizera, Bukoba na redio Mbiu. Pamoja na Redio nyingine nyingi ambazo zinasikika katika Mkoa wa Kagera zikirusha matangazo yake kutoka nje ya mkoa.
Pamoja na Redio kuna magazeti, mitandao ya kijamii, Cable TV, ambavyo vinautangaza mkoa wetu wa Kagera na kuwapasha wananchi wake kupitia Waandishi wa habari ambao wametapakaa mkoa mzima wakiandika habari mbalimbali za michezo, kuichumi, kijamii, Elimu, Utalii, Uwekezaji na nyinginezo nyingi.
Siku ya Mei 3 ilitangazwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani. Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani huongeza ufahamu wa umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na kuikumbusha Serikali wajibu wake wa kuheshimu na kuhakikisha haki ya uhuru wa kujieleza inaheshimika chini ya Ibara ya 19 ya Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu la 1948. Pia katika Siku hiyo Hukumbukwa Waandishi waliotangulia Mbele za Haki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa