• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Biharamulo Yaongoza Kwa Vituo Vyake Viwili Kupata Nyota Nne Katika Utoaji wa Huduma Bora za Afya Mkoani Kagera

Imewekwa : July 30th, 2018

Halmashauri za Wilaya nne Mkoani Kagera zikiongozwa na Halmashauri ya Biharamulo zapata vyeti vya utoaji huduma bora za afya kwa wananchi katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kwa kupata nyota kuanzia tatu na kuendelea baada ya tathimini iliyofanywa na  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mwaka 2017.

Vyeti hivyo vya huduma bora ya afya  vilitolewa na Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulie Julai 28, 2018 Wilayani Muleba ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo iliongoza kwa kuwa na nyota nne Katika Hospitali Teule ya Wilaya na Zahanati ya Katoke kwa kupata asilimia 69% pamoja na cheti walipewa ngao ya mshindi wa kwanza. Ngara  ilishika nafasi ya tatu kwa Hospitali ya Murugwanza kupata nyota nne na kupata asilimia 51%.

 Karagwe ilishika nafasi  ya nne kwa Hospitali Teule ya Wilaya Nyakahanga kupata nyota nne na kupata asilimia 51%. Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ilishika nafasi ya tano kwa Zahanati ya Buganguzi kupata nyota tatu na kupata asilimia 17%

Katika tathmini ya mwaka 2017 Biharamulo imeendelea kushika nafasi ya kwanza, Muleba ilikuwa ya mwisho kwa tathmini ya mwaka 2016 kwa kutokuwa na kituo chochote kilichokuwa na nyota tatu lakini kwa mwaka 2017 imeshika nafasi ya pili kimkoa. Aidha, Muleba, Kyerwa, Halmashauri ya Bukoba  na Missenyi kwa tathmini ya mwaka 2016 zilikuwa nafasi ya mwisho ambapo hazikuwa na kituo hata kimoja chenye nyota tatu.

Akitoa vyeti hivyo Naibu Waziri Dkt. Ndugulile alizipongeza Halmashauri zilizopata ushindi na kuzisisitiza kuendelea kufanya vizuri ili zifikie nyota tano. Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa pamoja na ushindi huo lakini hakuna Halmashauri iliyofikia asilimia 80% kwa hiyo mkoa bado una kazi ya kufanya ili kuhakikisha kila Halmashauri inafikia kiwango cha kitaifa cha asilimia 80%.

Katika hautua nyingne Naibu Waziri Dkt. Ndugulile aliagiza Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia Madaktari na Watumishi wa idara ya Afya wanapotoa huduma kwa mgonjwa katika vituo kila mmoja kwa nafasi yake aandike muda aliomhudumia mgonjwa ili kuhakikisha mgonjwa anapata huduma kwa wakati na likitokea tatizo ajulikane ni yupi kafanya uzembe.

Naibu Waziri Dk. Ndugulile alimalizia hotuba yake fupi kwa kuzitaka Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya kuhakikisha zinasimamia dawa za Serikali zenye nembo ya “MSD” na “GOT” haziuzwi kwenye maduka binafsi na zikipatikana katika maduka binafsi wahusika wachukuliwe hatua za kisheria

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi  Richard Luyango kwa niaba ya Serikali alishukuru Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi na kusisitiza kuwa viongozi wote Mkoani Kagera wataendelea kusimamia ili upatikanaji wa huduma bora zinapatikane na wananchi wapate huduma bora na kwa wakati.

Mwisho Mkuu wa Wilaya Luyango aliipongeza Halmashuri ya Wilaya ya Biharamulo kwa kupata ushindi wa kwanza katika mkoa na kuitaka Halmashauri hiyo kuendelea na uboreshaji wa huduma ili kuendelea kushika nafasi ya kwanza pia alizitaka Halmashauri zilizofanya vibaya kwenda kujifunza katika Halmashauri ya Biharamulo ili nazo ziweze kufanya vizuri.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa