• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Bodaboda Alimaarufu Asekdo Mkoani Kagera Mshindwe Wenyewe Lakini Mkuu wa Mkoa Tayari Kawasafishia Njia Kazi Kwenu

Imewekwa : April 3rd, 2019

Badala ya kuwasukuma ndani kuwakimbiza kwasababu ya kutofuata sheria mbalimbali za usalama barabarani, kuwaona ni wahuni na kuwanyanganya vyombo vyao vya moto vya kutafutia riziki na kujipatia kipato waelimishe juu ya sheria zinazohusu kazi yao, wape elimu ya ujasiliamali, itambue kazi yao iwe rasmi ili kushirikiana nao katika kusukuma maendeleo ya mkoa mbele.

Hilo ni kundi kubwa ambalo limejiajili katika sekta ya usafirishaji wa abiria kwa njia ya pikipiki maarufu kama bodaboda au Asekdo mkoani Kagera ambapo vijana hawa hapo awali walikuwa wakitekeleza kazi yao ya kubeba abiria kwa tabu kweli kutokana na baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi kuwasumbua kwa kuwakamata hovyo kuwanyanganya bodaboda zao na kuwatoza faini kila mara zisizokuwa na mpangilio.

Baada ya kilio chao Bodaboda  kumfikia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti na kufanya nao kikao kwanza aliamua kuwa mlezi wa vijana hao na kuwaagiza Jeshi la Polisi Mkoani Kagera badala ya kuwabughudhi liwasimamie wafanye kazi zao kwa amani ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo ya sheria za usalama barabarani ili vijana watekeleze ajira yao kwa amani na utulivu.

Nia ya Mkuu wa Mkoa Gaguti ni kuwaona bodaboda wakifanya kazi zao na kujiingizia kipato bila kusumbuliwa na mtu yeyote. Ili kulitekeza hilo chini ya usimamizi wake Mkuu wa Mkoa aliwaagiza bodaboda wote kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wasajili vijiwe vyao ikiwa ni pamoja na kujisajili majina yao katika vijiwe hivyo ili kutambulika rasmi na Serikali ya mkoa.

Pili, ili wananchi ambao ni wateja wawaamini bodaboda Mkuu wa Mkoa alitoa viaksi mwanga  (Reflectors) zenye namba mgogoni ili kila bodaboda atambulike kwa namba yake. Tatu Mkuu wa Mkoa Gaguti ili kuwaunganisha bodaboda ambalo ni kundi kubwa lililojiajili aliamua kuanzisha ligi ijulikanayo kama JPM BODABODA CUP KAGERA 2019 iliyoanza rasmi tarehe 30 Machi, 2019.

Ligi ya JPM BODABODA CUP KAGERA 2019 inahusisha timu za mpira wa miguu 16 (Timu za vijiwe 16) zilizoundwa na kupendekezwa na Bodaboda wenyewe ambapo mshindi wa kwanza anatarajiwa kuzawadiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera shilingi milioni 3, Mshindi wa pili Milioni 2, na mshindi wa tatu Milioni 1 ikiwa ni pamoja na makombe kwa mshindi wa kwanza wapili na watatu.

Lengo kuu la ligi JPM BODABODA CUP KAGERA 2019 anasema Mkuu wa Mkoa Gaguti kuwa ni kuimarisha vikundi vya Bodaboda ili viweze kuwa na uwezo wa kuwa ujasiliamali tofauti na kazi ya bodaboda ili ikitokea kijana anapata matatizo mfano ajali na kukaa mda mrefu bila kuendesha bodaboda awe na kipato ambacho hakitahitaji kuendesha bodaboda. Lakini pia kuinua vipaji kwa makundi yaliyosaulika na kuwa na timu ya mpira yenye vipaji kutoka katika kundi hilo.

Katika kuboresha hilo Mkuu wa Mkoa Gaguti tayari ametenga Bodaboda mpya tano kwa vikundi vitakavyoonekana ni  bora zaidi katika kufuata sheria za usalama barabarani chini ya usimamizi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani na bodaboda hiyo itakuwa mali ya kikundi au kijiwe hicho. Vikundi hivyo vitapatiwa bodaboda kila kimoja ili bodaboda hiyo iwe ya kikundi na kukiingizia mapato.

Manispaa ya Bukoba tayari imetenga shilingi milioni 20 kwaajili ya mkopo usiokuwa na riba kwa vijana hao ili wakakope na kuimarisha vikundi vyao na maisha yao kwa ujumla. Lengo kuu la kuliangalia kundi hili la bodaboda mkoani Kagera kuhakikisha kuwa vijana wanajiajili bila bughudha lakini pia watekeleze ajira yao kwa kufauata sheria za nchi kwa kuwajibishana wao wenyewe kwa wale ambao hawatafuata sheria za usalama barabarani badala ya Jeshi la Polisi kuwawajibisha.

Mwisho kama kiongozi wa Mkoa Mhe. Gaguti anasema nia yake ni kuona vijana wanashamiri katika kazi zao kwa kutekeleza sheria na kuzitii bila shuruti lakini pia Bodaboda wa Kagera kuwa mfano kwa nchi nzima kama usafirishaji huo ulivyoanzia mkoani Kagera.

Tayari hamasa ni kubwa mno kwa wakazi wa Bukoba kushuhudia mechi za mpambano wa bodaboda kila siku wakishuhudia JPM BODABODA CUP KAGERA 2019 Je nani anatanyakua milioni 3? Je ni kijiwe gani kitanyakua bodaboda mpya? Kazi kwenu ASEKDO BUKOBA

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa