• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Bw. Isaya Tendega Akijiandaa Kupanda Mche wa Mti wa Parachichi Shule ya Msingi Kayanga Karagwe Katika Kilele cha Wiki ya Upandaji Miti Kagera.

Imewekwa : April 3rd, 2018

Ukijani wa Mkoa wa Kagera Sasa Waelekezwa Katika Matunda Kuboresha Afya za Wananchi na Kulisha Viwanda

Mkoa wa Kagera waadhimisha kilele cha wiki ya upandaji miti Wilayani Karagwe kwa kupanda miche zaidi ya 600 ya miti ya matunda aina mbalimbali ili kuboresha afya za wananchi wa Kagera na kuondokana na matatizo ya utapiamlo na udumavu  hasa watoto wadogo.

Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka alisema  katika hotuba yake kuwa wananchi wa  mkoa wa Kagaera wana tatizo la kutokula matunda wakati kilimo cha matunda kinakubali katika ardhi ya Kagera.

Mkuu wa Mkoa alisistiza juu ya Kampeini yak e aliyoizindua mwezi Janauari 26, 2018 ya kupanda miti ya matunda kwa wingi ili kuhamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kula matunda mara kwa mara ili kumaliza tatizo la udumavu pamoja na utapiamlo magonjwa yanayosababishwa na kutokula matunda kwa wingi.

Mkuu wa Mkoa Kijuu alisisitiza tena  kila kaya kuhakikisha inapanda angalau miche mitano ya matunda kuzunguka katika nyumba  yao na Halmashauri za Wilaya kuhakikisha zinaanzisha vitalu vya matunda ili kurahisisha upatikanaji wa miche hiyo ya matunda kwa wananchi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa inasema “Tanzania ya Kijani Inawezekana, Panda Miti kwa Manufaa ya Viwanda” katika kufanikisha kaulimbiu hiyo mkoa wa Kagera umekuwa ukipanda miti kwa wingi ili kulinda mazingira na mwaka wa fedha 2016/17 ulifanikiwa kupanda jumla ya miti milioni 14 na miti milioni 12 ilifanikiwa kuota na kukua.

Aidha kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 mkoa chini ya kampeini ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera unaendelea kuhamasisha wananchi kupanda zaidi miti ya matunda kuliko miti ya mbao ili kuboresha afya ambapo kila Halmashauri imeagizwa kupanda miti hasa ya matunda na kufikia lengo la miche milioni moja na nusu.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Kayanga Mkuu wa Wilaya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Kagera alijumuika na wananchi, wanafunzi  pamoja na walimu na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya  ya Karagwe kupanda miche ya miti ya matunda  katika viwanja vya Shule hiyo na maeneo yanayozunguka Shule ya Msingi Kayanga.

Bw. Isaya Tendega Kaimu Katibu Tawala Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji kwaniaba ya Katibu Tawala wa Mkoa aliwasisitiza walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi kayangia kuitunza miche hiyo ya matunda ili ikue ili wanafunzi na walimu waweze kunufaika na matunda yatakayopatikana kutokana na miti hiyo.

Katika hatua nyingine  Bw. Tendega aliwashukuru wadau mbalimbali katika Mkoa wa Kagera wanaounga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira kwa kutoa miche ya matunda na miti katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera . Wadau hao ni pamoja na Tanzania Agricultural Modernization Association, Kanisa Katoliki, Vi Agroforestry, KKKT Dayosisi ya Karagwe na wengineo.

Mwaka huu maadhimisho ya wiki ya upandaji miti kitaifa ilifanyika Mkoani Shinyanga  Wilayani Kishapu na Mkoa wa Kagera uliadhimisha kilele hicho  Wilayani Karagwe  na huadhimishwa kila mwaka Aprili Mosi.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa