- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kuzindua rasmi Wiki ya Uwekezaji Kagera Agosti 14, 2019 akizindua pia Kongamano la Uwekezaji na kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera leo Agosti 15, 219 wadau mbalimbali wa uwekezaji na wafanyabiashara katika kongamano walijadili fursa mbalimbali za uwekezaji kwa kuzichambua kwa undani zaidi.
Katika Kongamano hilo la Wiki ya Uwekezaji Kagera jumla ya mada nane ziliwasilishwa na wataalam kutoka Sekta mbalimbali za umma na Sekta binafsi kwa kuzichambua na kujadili kwa kina kupata mwelekeo wa uwekezaji hasa majadiliano yakilenga namna bora ya kuondoa vikwazo na kusonga mbele katika kuinua uchumi wa mkoa wa Kagera
Mada nane zilizowasilishwa na wasomi wabobezi na wajasiliamali wenye uzoefu mkubwa katika ujasiliamali na kuzichambua kwa undani kuonesha fursa zilipo na zinaweza kufikikaje ni pamoja na mada ya Ujue Mkoa wa Kagera iliyowasilishwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Method Kilaini ambaye ni mbobezi katika masuala ya historia ambapo aliuchambua mkoa wa Kagera kihistoria miaka ya nyuma na kwa sasa mkoa ulipo.
Mada nyinginezo ni; Mazingira ya jumla ya kibiashara na jukumu la mamlaka za kisheria katika kusaidia uwekezaji, Tatu; Mkoa wa kagera kama kitovu cha biashara katika nchi za Afrika Mashariki na Kati (Biashara za Mipakani), Nne, Kutumia fursa za uwekezaji Kagera katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na Viwanda, Tano; Ni namna gani changamoto ya lishe katika mkoa wa Kagera inaweza kutumika kama fursa ya uwekezaji.
Aidha, mada nyingine zilizojadiliwa ni pamoja na; Ni namna gani fursa za utalii ambazo hazijatumika ipasavyo zinaweza kutumika katika uwekezaji kwenye mkoa wa Kagera, Saba; Nafasi ya huduma za kijamii kwa ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Kagera. Mada ya mwisho ilikuwa ni huduma za kifedha kama kichocheo cha uwekezaji na ukuaji wa uchumi.
Mara baada ya mawasilisho ya mada tajwa hapo juu ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa hali ya juu kuhusu mada hizo na washiriki kuchangia kwa kuonesha ni fursa gani zinapatika na zinafikikaje katika mkoa wa Kagera Wafanyabiasha kutoka nchi za Rwanda na Burundi walipata nafasi ya kukutana Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera na kuwa na mazungumzo ya kibiashara (B2B Discution) kulingana na mtu kavutiwaje.
Baada ya Wiki ya Uwekezaji Kagera kufika mwisho uongozi wa Mkoa wa Kagera utakuwa na orodha ya jumla ya biashara ambazo wafanyabiashara kutoka nje ya nchi watakuwa wameingia makubaliano na wenzao kutoka nchi jirani ili kufanya ufuatiliaji na kuhakikisha fursa hizo zinafikika na kutumika.
Wiki ya Uwekezaji Kagera inatarajiwa Kufungwa rasmi tarehe 16/08/2019 lakini maoonesho ya bidhaa mbalimbali yatakuwa yanaendelea katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba hadi tarehe 18/08/2019 na Wadau mbalimbali wa uwekezaji watapata fursa za kwenda kutembelea vivutio mbalimbali vya uwekezaji katika mkoa wa Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa