- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Marburg ulio ripotiwa Mkoa wa Kagera katikati ya mwezi Machi, 2023 na kupelekea vifo vya watu sita. Leo tarehe 02.06.2023 Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ametoa taarifa kuwa Tanzania imepambana kuudhibiti ugonjwa huo na sasa Mkoa wa Kagera na Nchi ya Tanzania ni salama.
Amesema hayo wakati akizungumza na viongozi na wadau mbalimbali wa afya wakati wa hitimisho la mapambano dhidi ya ugonjwa huo, ameeleza kuwa ni zaidi ya siku 42 toka mgonjwa wa mwisho kupona ugonjwa wa Marburg hivyo Nchi imekidhi vigezo vya Shirika la Afya na kutangaza mwisho wa ugonjwa huo.
“Kutokana na ushirikiano wa wananchi, Serikali, Watumishi wa Idara ya Afya na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya Nchi, umepelekea kumalizika kwa ugonjwa huu, hivyo natangaza kuwa leo tarehe 02.06.2023 ugonjwa wa Marburg umeisha rasmi Mkoa wa Kagera,” ameeleza Mhe. Ummy
Aidha,amewashukuru wadau mbalimbali wa Afya wakiongozwa na Shirika la Afya Duniani kwa ushirikiano mkubwa walioutoa na kuhakikisha Watanzania na Dunia inalindwa dhidi ya ugonjwa wa Marburg.Na kuisisisitiza jamii kuendelea kuchukua tahadhari na kutoa taarifa pale kuna jambo la tofauti.
Akiwasilisha taarifa ya kitaalam, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ameeleza kuwa hadi kufikia tarehe 31.05.2023 watu waliopata maambukizi ya ugonjwa huo ni watu tisa, kati ya hao wagonjwa watatu walipona akiwemo daktari wa kituo cha Afya cha Maruku na wagonjwa sita walipoteza maisha akiwemo mtaalamu wa maabara wa kituo cha Afya cha Maruku
Ameendelea kueleza kuwa ufuatiliaji ufuatiliaji wa watu waliotangamana na wagonjwa wa Marburg ulifanyika kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Manispaa ya Bukoba,ambapo jumla ya watu 212 walibainika na kufanyiwa ufuatiliaji wa siku 21 kati yao ni watu wawili pekee ndio waliyoonesha dalili na baada ya kupimwa walibainika na maambukizi
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Ndg.Toba Nguvila ametoa ombi la kujengwa kwa kituo maalum cha kuwahudumia wagonjwa wa magonjwa ya mlipuko na kutokana na Mkoa wa Kagera kuwa mpakani hivyo kupelekea kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ameomba Serikali kujenga vituo vya kutoa huduma ya dharura mipakani
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa