• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Huduma za Madaktari Bingwa Mkoani Kagera Tayari Zawafikia Wananchi 429 Siku ya Kwanza na Wengi Bado Wafurika Kupata Matibabu

Imewekwa : November 6th, 2018

Huduma za Madaktari Bingwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera zawafanya wananchi wengi wenye matatizo ya kiafya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera kufurika katika Hospitali hiyo ili kupata huduma za Kibingwakutoka kw Madaktari Bingwa.

Katika uzinduzi rasmi wa utoaji wa huduma hizo za Kibingwa Novemba 6, 2018 Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Dk. Felix I. Otieno alitoa taarifa kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhandisi Richard Luyango ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba kuwa tangua zoezi lianze Novemba 5, 2018 siku ya Jumatatu tayari wagonjwa 858 walikuwa wamejiandikisha kuwaona Madaktari Bingwa wa magonjwa mbalimbali.

Aidha, Dk. Felix alisema kuwa tayari Madaktari Bingwa 27 walikuwa wamewasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwaajili ya kutoa huduma za kibingwa  na siku ya kwanza ya Jumatatu Novemba 5, 2018  wagonjwa 429 walikuwa wamepatiwa huduma za Kibingwa katika vitengo vya kuhudumia magonjwa mbalimbali katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kuwaadaa baadhi ya wagonjwa kwajili ya upasuaji.

Akizindua rasmi zoezi la kutoa huduma za Kibingwa Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhandisi Richard Luyango ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango aliwashukuru Madaktari bingwa 27 ambao tayari wamewasili katika Hospitali hiyo na kuanza kutoa huduma za Kibingwa na kusema kuwa huo ni uzalendo mkubwa waliuonesha wa kuwahudumia wananchi wa Kagera.

“Nawapongeza sana Madaktari Bingwa ambao mmefika hapa kuwahudumia wananchi wetu mmekuwa wazalendo kweli kweli kama mnavyowaona wananchi wetu hapa kuwa wanahitaji huduma zenu kwasababu ya matatizo ya kiafya waliyonayo. Wito wangu kwenu ninyi Madaktari Bingwa niwaombe muongeze siku mbili zaidi katika kutoa huduma kwani siku sita (tarehe 5 hadi 11 Novemba, 2018) hazitatosha ukiangalia wananchi waliohudhuria hapa.”  Alisisitiza Mhandisi Luyango.

Pia Mhandisi Luyango aliwaomba wananchi ambao ni wagonjwa waliohudhuria katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kupata huduma za Kibingwa kuwa wavumilivu katika kupata huduma hizo kutokana na wingi wao na pia walitakiwa kusikiliza maelekezo wanayopewa na Wataalamu wa Afya ili kuwafikia Madaktari Bingwa kwajaili ya kupatiwa huduma.

Naye Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Projectus Rutabanzibwa aliwataka watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika kutoa huduma kwenye zoezi hilo na kusisitiza kuwa Serikali imetoa fedha nyingi kugharamia zoezi hilo kwa ajili ya kutoa Huduma za kibingwa kwa Wananchi wa Mkoa wa Kagera.

Kwa upande mwingine Daktari Bingwa Kiongozi wa timu ya Madaktari Bingwa wanaotao huduma za Kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Dk. Samwel Rweyemamu ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo alisema timu yao ya Madaktari Bingwa inaendele vizuri na utoaji wa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera.

Dk. Rweyemamu alisema kuwa kwa upande wa magonjwa ya moyo siku ya kwanza Jumatatu Novemba 5, 2018 walikuwa wamehudumia wagonjwa watu wazima 60 lakini siku ya pili ya Jumanne Novemba 6, 2018 huduma za Kibingwa kwa upande wa magonjwa ya moyo zilikuwa zikitolewa kwa watoto ambao nao ni wengi. Aidha, Dk. Rweyemamu alisema tayari wagojwa 10 walikuwa wameshauriwa kwenda katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kutokana na matatizo yao kuwa makubwa zaidi.

Nao wananchi ambao wamefurika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera walikiri mbele ya Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Mhandisi Richard Luyango ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba kuwa wanaishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma za Kibingwa karibu. Pia krahisisha namna ya kuwaona Madaktari Bingwa ukilinganisha na kuwafuata katika vituo vyao vya kazi pamoja na gharama za malazi na chakula.

Katika kutekeleza zoezi hilo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera wamejipanga vizuri kuhakikisha huduma za Kibingwa zinatolewa kwa uhakika ambapo wananchi wenye kadi za Bima Hawatozwi chochote bali wanalipia gharama zao kupitia kadi hizo lakini mfumo wa kukusanyia mapato unatumika kuhakikisha fedha ya Serikali inakusanywa kwa usahihi ili kukuza mapato ya Hospitali hiyo.

Ikiwa ni mara ya pili zoezi la huduma za Madaktari Bingwa kutolewa Mkoani Kagera mwaka 2017 jumla ya wagonjwa 3,146 walihudumiwa na mwaka huu 2018 huduma hizi zinalenga kuwahudumia wagonjwa 4,000 hadi 5,000 kwa magonjwa ya Uzazi na kizazi kwa wanawake, Magonjwa ya upasuaji kwa Ujumla, Magonjwa ya njia ya mikojo ikiwemo tezi Dume, Magonjwa ya pua, sikio na koromeo.

Magonjwa mengine yatakayoshughulikiwa na Madaktari Bingwa ni pamoja na Magonjwa ya mifupa, Magonjwa ya moyo, Magonjwa ya ndani ikiwemo sukari na figo, Magonjwa ya watoto, Magonjwa ya Afya ya kinywa na meno, Magonjwa ya macho, Magonjwa ya Ngozi, Magonjwa ya afya ya akili, na Saratani ya Mlango wa kizazi.

 

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa