• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Ijue Mitazamo ya Viongozi Wetu Kuelekea Wiki ya Uwekezaji Kagera Agosti 12 Hadi 17, 2019 Gymkhana Manispaa ya Bukoba

Imewekwa : July 12th, 2019

Tunapoelekea katika Wiki ya Uwekezaji Mkoani Kagera sasa tunakuleta makala fupi fupi ili ujue malengo ya wiki hiyo na mtazamo wa viongozi wa Mkoa wa Kagera kuelekea Wiki hiyo Agosti 12 hadi 17, 2019 wiki ambayo ni fursa kubwa kwa Wanakagera na wadau mbalimbali wa maendeleo kuzijua fursa zinazopatka Kagera na kuzichangamkia.

Kaulimbiu ya Wiki ya Uwekezaji Kagera ni “Kagera Eneo la Kimkakati kwa Uchumi Wetu na Afrika Mashariki” kaulimbiu hii inamaanisha kuwa Mkoa wa Kagera unapakana na nchi tano za Kenya, Uganda, Burundi, Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchi hizo ni fursa ya biashara kutokea Kagera.

Katika kuelekea Wiki ya Uwekezaji Kagera Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti tayari amefanya mawasilianao na Balozi wa Nchi ya Kongo ambaye tayari amethibitisha kushiriki wiki hiyo jambo ambalo kwa wadau wa biashara wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo ya kufanya biashara na nchi ya Kongo (DRC) mfano biashara ya  Samaki, Dagaa, mbogamboga, mahindi na ndizi.

Pili,  Mhe. Gaguti tayari Julai 7, 2019 amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Ernest Mangu ili kuweka mazingira sawa kati ya wafanyabiashara wa Rwanda na Tanzania na Wanankagera kutumia fursa ya mpaka wa Rusumo kufanya biashara nchini Rwanda kwa kutumia fursa ya ukaribu na kuwa na mpaka mrefu katika wa Kagera.

Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Ernest Mangu katika kikao hicho cha Julai 7, 2019 kilichofanyika Wilayani Ngara alihaidi kuwaleta wafanyabiashara wa Rwanda kuja kushiriki katika Wiki ya Kagera kuona fursa za uwekezaji pamoja na biashara mbalimbali wanazoweza kufanya kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera au Watanzania, hiyo ni fursa inakuja.

Naye katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera akiwa Mwenyekiti wa kikao cha kupitia andiko la uwekezaji Mkoani Kagera kilichofanyika Julai 11, 2019 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa alisema kuwa ni bahati kubwa ambayo haijawahi kutokea tangu uhuru mkoa kuwa na andiko la uwekezaji ambalo litazinduliwa rasmi Agosti 14, 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye atakuwa mgeni Rasmi katika Wiki ya Uwekezaji Kagera.

Naye Sheikh Haruna kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera akitoa neno katika uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka mitano wa maendeleo wa Baraza la Waislamu Tanzania Mkoa wa Kagera Juni 22, 2019 katika Shule ya Nyanshenye Manispaa ya Bukoba alitoa wito kwa Waislamu wenzake kuiona Wiki ya Kagera kama fursa na wasibaki nyuma bali washiriki kikamilifu mkoa wa kagera usonge mbele kwa kuzitumia fursa uliobarikiwa nazo

Askofu Dk. Abednego Keshomshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Magharibi akitoa neno katika mkutano wa SINODE wa mwaka Kiizi Halmashauri ya Bukoba aliwakumbusha wachungaji Maaskofu na viongozi wote waliokuwepo katika mkutano huo kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera anataka Kagera ifunguke na anatakiwa kuungwa mkono kwa dhati katika Wiki ya Uwekezaji Kagera.

Katika Wiki ya Uwekezaji Kagera pamoja na fursa nyingi zitakazokuwepo lakini fursa ya utamaduni katika mkoa wa Kagera pia itaangaliwa kwa karibu hasa utamaduni wa watu wanaoishi katika mkoa huu ambapo tamaduni hizo zinaweza kuwa kivutio kikubwa na kuleta watalii na kuacha fedha za kigeni ili kukuza zaidi uchumi wa mkoa.

Jipange kushiriki Wiki ya Uwekezaji Kagera na kuzitumia fursa za Kagera kujenga uchumi wako binafsi, uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla “Kagera Eneo la Kimkakati kwa Uchumi Wetu na Afrika Mashariki” Kagera Kazi, Amani na Maendeleo.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa