• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Kagera Mmevunja Rekodi Kwa Mkakati wa Kutangaza Fursa za Uwekezaji Mmejipanga Vizuri Mtafanikiwa – Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Imewekwa : August 14th, 2019
  • Azindua Rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 

Nimehudhuria makongamano ya uwekezaji katika mikoa sita lakini kwa mkoa wa Kagera kweli mmejipanga kuhamasisha uwekezaji maandalizi yenu si ya michezo mnaye mkuu wa mkoa mbunifu na mfatiliaji, nimepita kwenye mabanda nimejionea bidhaa mbalimbali zinazosindikwa hapa Kagera kweli Kagera  kwa mkakati huu mtafanikiwa.

Maneno hayo yalisemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kagera Agosti 14, 2019 katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba alipokuwa mgeni rasmi na kuzindua rasmi Wiki ya Uwekezaji Kagera.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kagera alisema kama mkakati wa Wiki ya Uwekezaji Kagera utatumika vizuri utaupandiusha uwezo wa kiuchumi wa mwananchi mmoja mmoja, uwezo wa mkoa pia na Taifa kwa ujumla.

“Kama tutachangamkia fursa ya uwekezaji Kagera tutaweza kuinua zaidi pato la sasa la mwananchi ambapo kwasasa ni shilingi 1,370,000/=  kwa mwaka na pato la mkoa la sasa la shilingi bilioni 4.98 aidha, mkoa wa Kagera utachangia zaidi pato la taifa badala ya asilimia 3.9 unavyochangia sas.” Alifafanua Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi pamoja na wageni mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara kutoka nchi za Burundi na  Rwanda alisema kuwa kuna sababu za kuwekeza katika mkoa wa Kagera  kwa sasa na alizitaja sababu hizo kama ifuatavyo:

Kwanza Mkoa wa Kagera una amani na utulivu na usalama wa kutosha ambapo alisema kuwa mwekezaji yeyeyote anapenda sana kuwekeza sehemu na mahala penye utulivu. Pili ni fursa za masoko katika mkoa wa Kagera  ambapo alisema kuwa mkoa unapakana na nchi nne za Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda lakini pia upo karibu na nchi za Kongo (DRC) na Sudani ya Kusini na kwa ujumla nchi hizo kuna soko la watu zaidi ya milioni 190.

Sababu ya tatu mkoa wa Kagera una hali nzuri ya hewa, ukiwa na rutuba ya kutosha kuotesha na kustawisha mazao yote, ukipata mvua nyingi mara mbili kwa mwaka kuanzia kwa kiwango cha  milimita 600 hadi 2000 kwa mwaka. Kutokana na hali hiyo mkoa wa Kagera unaongoza kwa uzalishaji wa kahawa yenye ubora na pendwa sana duniani ya robusta na arabika.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliwasistiza wafanyabiashara kuja kuwekeza Kagera kwani viwanda vya kuchakata kahawa bado ni vichache sana lakini pia aliwakumbusha wananchi  kuanza kuwekeza katika viwanda vidogo na vya kati kusindika mazao mbalimbali na kutolea mfano wa mjasiliamali wa anayetengeneza  sabuni kwa mafuta ya mawese kutoka Wilayani Biharamulo anayezalisha boksi 2000 kwa mwaka. 

Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliwasisitiza wafanyabiashara kutoka nchi jirani kuja Kagera kuwekeza katika kilimo cha zao la Vanilla ambalo linalipa sana na maka jana 2018 kilo moja ilikuwa inauzwa kwa shilingi 150,000/=.

Aidha,  alisema kuwa Mkoa wa Kagera ni mkoa wenye neema kwani kuna fursa za kuwekeza katika uvuvi, maeneo ya kufugia katika ranchi za taifa ambako kuna zaidi ya hekta  120,000 za kufugia , vile vile alitoa wito kwa Wanankagera pamoja na Watanzania kuchangamkia fursa ya utalii hasa kujenga Mahoteli na kuanzisha makampuni ya utalii ili kuchangamkia fursa ya mbuga za Hifadhi za Taifa za Brigi Chato, Ibanda, na Rumanyika.

Naye Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti wakati akitoa neno kabla ya Waziri Mkuu kuwahutubia wananchi  alisema kuwa Kagera inawakalisha ukanda wa Kasikazini Magharibi kwa fursa ulizonazo na  kuwa kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Pia alimweleza Waziri Mkuu kuwa mara baada ya kukutana na Mabalozi wa nchi tano  mkoa umejipangia kwenda katika nchi hizo kuhakikisha fursa zilizowasilishwa na Mabalozi hao zinafanyiwa kazi ili kuufungua uchumi wa ukanda wa Kasikazini Magharibi.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akikamilisha hotuba yake aliwataka Wakuu wa mikoa wengine kuiga katika mkoa wa Kagera namna ya kutangaza fursa za uwekezaji na kuwahamasisha wawekezaji kuja Kagera kuwekeza kwani panafikika kwa njia zote za anga, barabara, na majini.

Mara baada ya hotuba yake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alizindua rasmi Wiki ya Uwekezaji Kagera , pili alizindua Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera na alizindua rasmi Kongamano la kujadili na kudadavua fursa za uwekezaji Kagera ambalo litaanza rasmi Agosti 15, 2019 wakati wote huo maonesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa