• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Kahawa Ambayo Tayari Imekomaa na Inasubiria Kuvunwa

Imewekwa : May 29th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Avikagua Vyama Vikuu Vya Ushirika Kuona Utayari wa Kukusanya Kahawa ya Wakulima Msimu Unapofunguliwa Juni Mosi 2018

Mkoa wa Kagera ukiwa mzalishaji mkubwa wa zao Kahawa nchini kwa zaidi ya asilimia 50 sasa wafanya maandalizi ya kufungua msimu wa mwaka huu 2018 wa ununuzi wa Kahawa kwa wakulima kupitia Vyama Vikuu  vya Ushirika vya Kagera Cooperative Union 1990 Limited (KCU 1990 LTD) na Karagwe District Co operative Union  Limited (KDCU LTD)

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu katika kuhakikisha agizo la Serikali la Wakulima kuuza Kahawa yao kupita Vyama vya Ushirika linatekelezwa kikamilifu amevitembelea Vyama Vikuu vya Ushirika vya KDCU Ltd  na KCU 1990 LTD kuona maandalizi ya kupokea kahawa hasa maghara ya kuhifadhi kahawa hizo pamajoa na viwnda vya kukoboa kama vipo tayari kufanya kazi msimu unapofunguliwa  Juni 1, 2018.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu alitembelea na kukagua mashine za kukoboa kahawa katika kiwanda  cha BUKOP na maghara ya kuhifadhi kahawa kiwandani hapo na ghara la Kemondo la KCU 1990 Ltd. Katika Mashine ya kukoboa kahawa BUKOP Mkuu wa Mkoa alijonea ukarabati wa mashine zilizomo katika kiwanda hicho zikifanyiwa ukarabati ili kuanza msimu wa ukoboaji

Katika Wilaya ya Karagwe Mkuu wa Mkoa alitembelea maghara ya Chama Kikuu cha KDCU Ltd pamoja na mashine ya kukoboa kahawa iliyokuwa ikifanyiwa ukarabati ambapo alipewa taarifa ya kiwanda hicho kudaiwa fedha za Ankara ya umeme na TANESCO ambapo alisema kuwa tayari Kamati ya Ulinzi na Usalama inalifanyia kazi suala hilo ili msimu ukifunguliwa mashine hiyo iweze kukoboa kahawa.

Katika Wilaya ya Kyewa Mkuu wa Mkoa  alitembelea na kukagua maghara ya vyama vya Msingi vya Iteera na Karongo na kuridhika na maandalizi ya maghara hayo kupokea kahawa kwa msimu huu wa mwaka 2018 unaotarajiwa kufunguliwa Juni 1, 2018.

Akiongea na viongozi wa Vyama hivyo Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera  Mhe. Kijuu alisema kuwa ni lazima mkoa usimamie agizo la Serikali,  na lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha wakulima wa kahawa wananufaika na kilimo chao cha kahawa bila kunyonywa. Aidha, alisistiza kuwa wakulima watapewa malipo ya awali na baada ya kahawa kuuzwa watalipwa malipo ya pili kulingana na bei ya soko la dunia.

“Najua wakulima wengi  wana mashaka na mfumo mpya wa uuzaji wa kahawa kutokana na makovu waliyoyapataa huko miaka ya nyuma lakini Serikali sasa imeamua kuhakikisha wananufaika na kahawa yao kupitia Vyama vya Ushirika na ndiyo maana nimeamua kufuatilia kwa karibu. Hapa namsafishia njia Mhe. Waziri Mkuu ambaye anatarajia kuja Kagera kuhakikisha mkulima ananufaika na Kahawa yake.” Alisistaiza Mhe. Kijuu.

Maagizo; 

Mara baada ya kukagua maghara na viwanda vya kukoboa kahawa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu aliwaagiza Viongozi wa Vyama Vikuu vya Ushirika  vya KCU Ltd na KDU Ltd kwanza  kuhakikisha maghara yanasafishwa kwa kiwango cha kuridhisha ili kupokea kahawa ya wakulima. Pili kuhakikisha mizani yote inafanyiwa uhakiki na Wakala wa Vipimo kabla ya kuanza kukusanya kahawa ili mkulima asipunjwe katika vipimo.

Tatu, kukamilisha ukarabati wa mashine za kukoboa kahawa kwa wakati ili mara kahawa ikianza kukusanywa isikwame kukoborewa na kusababisha kucheleweshwa kwenda katika soko la mnada wa dunia na kuchelewesha malipo ya pili ya mkulima.

Nne, Kamati za Ulinzi na Usalama  za Wilaya kuhakikisha hakuna kahawa inauzwa “Obutura” wala kutoroshwa kwenda nchi jirani kwa wafanyabiashara  wanaonunua kwa njia ya magendo bila kusajilijiwa kihalali kama Vyama vya Ushirika vinavyotambulika.

Chama Kikuu cha KCU 1990 Ltd kinatarajia kukusanya tani 5,000 na zaidi za kahawa maganda katika msimu huu wa mwaka 2018. Aidha, KDU Ltd inatarajia kukusanya kahawa ya wakulima kiasi cha tani 40,000 na asilimia 90 ya kahawa hiyo itakuwa Robusta na Arabika asilimia 10, pia katika kahawa hiyo kutakuwa na kahawa ya masoko maalum (Organic Coffee) tani 4,000.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa