• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Awasili Mkoani Kagera Kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Tatu Kukagua Miradi ya Maendeleo ya Sekta ya Afya

Imewekwa : June 10th, 2019

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Inmi Patterson awasili Mkoani Kagera kwa ziara ya  kikazi ya siku tatu kukagua miradi ya maendeleo katika Sekta ya Afya kitengo cha UKIMWI inayotoa huduma kwa wananchi na kufadhiliwa na nchi ya Marekani.

Kaimu Balozi Dk. Patterson akiongea na Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ofisini kwake mara baada ya kuwasili  Juni 10, 2019 mkoani Kagera alitoa pole kwa wananchi wa Manispaa ya Bukoba waliokumbwa na mafuriko Mei 26, 2019  na kusema kuwa aliguswa na tukio hilo lililoleta taflani kwa wananchi aidha aliishukuru Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa kwa hatua zilizochukuliwa haraka kunusuru maisha ya wananchi hao.

Akitaja dhumuni la ziara yake mkoani Kagera Kaimu Balozi Dk. Patterson alisema kuwa amekuja Kagera kuona mafanikio ya  miradi ya maendeleo hasa Sekta ya Afya inayofadhiliwa na Marekani kwani mkoa wa Kagera unaonekana kunafanya vizuri hasa katika upimaji wa watu waliombukizwa na Virusi Vya UKIMWI (VVU) hasa wananume, utoaji wa dawa za kufubaza nguvu za Virusi, pia wananchi kuhamasika kupima katika vituo vya afya.

“Nimefurahi sana kufika hapa kujionea  miradi tunayoifadhili lakini kikubwa na nia yangu ni kuona maambukizi ya VVU yanashuka pia mkoa huu umebarikiwa kuwa na chakula cha kutosha lakini  inaonekana udumavu wa watoto bado ni mkubwa lazima kuangalia mbele kwanikwa takwimu za sasa idadi  ya watu Tanzania ni karibu milioni 60 lakini lazima tufikirie mwaka 2045 wingi huo wa watu utakuwa mara mbili yaani milioni 120 lazima tuanze sasa kujenga kizazi chetu. “ Alisisitiza Kaimu Dk. Balozi Patterson

Naye Mkuu wa Mkoa Gaguti akimweleza Balozi Dk.  Patterson  juu ya namna mkoa unavyopambana na udumavu alisema kuwa kwa Kagera chakula si tatizo bali elimu tu kwa wananchi ambapo alisema kuwa sasa udumavu imekuwa ajenda yake na ya mkoa mzima kwa kutoa elimu juu ya lishe bora kwa wananchi  ili kuhakikisha tatizo la udumavu linaondoka katika mkoa wa Kagera.

Naye Mgagnga Mkuu wa Mkoa Dk. Marco Mbata katika mazungumzo hayo alimhakikishia Kaimu Balozi Dk. Patterson kuwa takwimu za hivi karibuni  za udumavu kwa mkoa wa Kagera umeshuka kutoka asilimia 41.7 hadi asilimia 39.8 na mkoa bado unaendelea na kutoa elimu kwa wananchi lishe bora kwa kutumia vyakula mbalimbali  vilivyomo mkoani Kagera badala ya kula chakua aina moja tu ndizi.

Vilevile Mkuu wa Mkoa Gaguti alimweleza Kaimu Balozi Dk. Patterson juu ya fursa mbaimbali za uwekezaji kama kilimo, ufugaji, utalii na nyinginezo ambapo alisema katika sekta ya kilimo mkoa una eneo la kilimo na kuna fursa kubwa ya kilimo cha Vanila. Aidha, zao la kahawa mkoa wa Kagera unazalisha karibu nusu ya uzalishaji wa nchi nzima ya Tanzania  na alimwomba Kaimu Balozi kuwaleta wawekezaji kuja kuwekeza katika Sekta hizo.

Akiongelea fursa za uwekezaji Kaimu Balozi Dk. Patterson alisema kuwa mkoa wa Kagera ni kitovu cha usafirishaji kwani mkoa huo umepakana na nchi nyingi ambazo ili kufikika lazima upite Kagera pia Balozi huyo wa marekani alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye uwezo  usiokuwa na ushindani kutokana na raslimali ilizonazo kwahiyo wananchi wake hawapaswi kuwa masikini.

Katika Hutua nyingine Mkuu wa Mkoa  Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti alimpokea ofisini kwake Balozi wa Ethiopia nchini Tanzania  Balozi Yonas Yosef Sanbe ambaye naye aliwasili mkoani Kagera Juni 10, 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa