• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Kama Una Wazo la Kukigawa Chama Kikuu Cha Ushirika KDCU LTD ni Bora Uhame Mkoa wa Kagera Sipo Tayari Kuona Hilo Linatokea – RC Gaguti

Imewekwa : March 5th, 2019

“Kama kuna mwananchi, kundi la watu, baadhi ya wanachama wa Vyama vya Ushirika au kiongozi yeyote ana wazo la kukigawa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Karagwe na Kyerwa Development Co-operative Union Limited (KDCU LTD) ahame mara moja Mkoa wa Kagera au akafanye hivyo nje ya mkoa huu lakini sipo tayari kuona jambo hilo linatokea.” Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akitoa onyo katika Mkutano Mkuu wa 32 wa KDCU LTD Kayanga Wilayani Karagwe.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa onyo hilo Machi 5, 2019 Wilayani Karagwe kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa KDCU LTD katika ukumbi wa CCM akiwa mgeni rasmi wakati akiongea na wajumbe wa Mkutano huo ambapo alisema kuwa tayari ameanza kusikia fununu za baadhi ya watu kutaka kukigawa chama cha KDCU LTD katika vyama viwili ambavyo vitawakilisha Wilaya za Karagwe na Kyerwa na kuonya kuwa jambo hilo haliwezi kutokea na halitakiwi kufikiriwa wala kujadiliwa.

Pia Mkuu wa Mkoa Gaguti alisistiza kuwa kwasasa anatamani Mkoa wa Kagera ungekuwa na Chama Kikuu cha Ushirka kimoja chenye nguvu na kuwahudumia wakulima lakini si kuwa na Vyama vya Ushirika vingi ambavyo vitauingiza mkoa katika migogoro na haviwezi kuwasaidia wakulima kuendeleza kilimo cha kahawa lakini pia kuwanufaisha wakulima na zao la kahawa ambalo linatakiwa kuwainua kiuchumi wananchi  wa Kagera.

“Serikali itaendelea kuweka misingi na mikakati iliyo imara ili kuhakikisha kahawa inapata bei bora na fedha za wakulima kupatikana mapema ili mkulima asihangaike wakati tayari amekusanya kahawa yake katika Chama cha Msingi. Pia Serikali ingependa kuona zao la kahawa linaboreshwa zaidi na kuongeza uzalishaji mkoani Kagera kutoka uzalishaji wa sasa wa kilo milioni 58.9 hadi kilo milioni 100”. Alisistiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Katika hatua nyingine Mbunge wa Kyerwa Innocent Bilakwate akiongea na wajumbe wa Mkutano huo aliwaonya vionozi wa KDCU LTD kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa fedha za wakulima katika Vyama vya Msingi vya chama kikuu hicho kwani ambapo alisema alisema kuwa kwa utafiti wake baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wamehujumu au kutumia vibaya fedha za wakulima katika maeneo yao.

Jambo hilo lilimfanya Mkuu wa Mkoa Gaguti kuagiza Vyama vya Msingi vya  Nyakatuntu, Kaina, na Kamuli kukamatwa mara moja na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa ubadhilifu wa fedha za wakulima na ifikapo Machi 6, 2019 saa 3:00 asubuhi awe amepata taarifa ni hatua gani zimechukuliwa kwa viongozi hao na kutoa rai kwa baadhi ya viongozi ambao wamejipanga kuhujumu mfumo wa ushirika kuwa Serikali itachukua hatua kali sana dhidi yao.

Katika msimu huu wa mwaka 2018/19 ulioanza mwezi Mei Mosi 2018 na utakamilika Aprili 30, 2019 Mkoa wa Kagera umekusanya na kuuza  jumla ya kilo milioni 58.9 za kahawa na Chama Kikuu cha  KDCU LTD kimekusanya asilimia 67%  kahawa zote. Chama cha KDCU LTD kilikuwa kimeotea kukusanya tani elfu 40 na kufanikiwa kukusanya tani elfu 39 sawa na asilimia 98% na tayari chama hicho kimepata faida ya shilingi milioni 260.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa