- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera (RCC) katika kikao cha dharura imepitisha kwa kauli moja mapendekezo ya Kamati ya ushauri ya Wilaya ya Missenyi ya kubadili jina la Jimbo la uchaguzi la Nkenge ili liitwe Jimbo la Missenyi jina litakalowagusa wananchi wote katika Wilaya hiyo yenye Jimbo la uchaguzi moja.
Kikao hichokilichofanyika Machi 17, 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera na kuongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Hajjat Fatma Mwassa kilikuwa na ajenda kuu moja ya kugawa Majimbo na kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi katika Mkoa wa Kagera.
Kati ya Majimbo tisa ya uchaguzi yaliyopo mkoani Kagera ni Jimbo moja la Nkenge linalopatikana Wilayani Missenyi lilipendekezwa kubadilishwa jina na kuitwa Jimbo la Missenyi na mapendekezo hayo yaliungwa mkono na wajumbe wote wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kama ilivyopendekezwa na kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Missenyi.
Wakitaja sababu kuu ya kupendekeza kubadilisha jina la Jimbo la uchaguzi la Nkenge Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Missenyi walisema kuwa jina la Nkenge limekuwa likitumika tu kwa Jimbo lakini hakuna taasisi yoyote ya Serikali au binafsi inatumia jina hilo la Nkenge, lakini pia mawasiliano yote ya Kiserikali yamekuwa yakitumia jina la Missenyi na siyo Nkenge.
Aidha, Katika hoja ya kugawa Majimbo ya uchaguzi yaliwasilishwa mapendekezo ya kugawanywa kwa Majimbo ya Uchaguzi ya Biharamulo Magharibi na Jimbo la Ngara lakini kutokana na kutokukidhi vigezo vya kugawanywa Majimbo hayo Wajumbe wa kikao walikubaliana baada kupiga kura mara mbili kuwa mchakato wa kuyagawanywa majimbo hayo usitishwe hadi hapo baadae kwa sababu ya kutokidhi vigezo vilivyo wekwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
Akifafanua vigezo hivyo Mkuu wa Mkoa Hajjat Fatma Mwassa Mwenyekiti wa kikao alisema kuwa vigezo vikuu ni uchumi mkubwa wa Jimbo la Uchaguzi linalotakiwa kugawanywa, Wingi wa watu wasiopungua 400,000 lakini kati ya majimbo hayo mawili ya uchaguzi ya Biharamulo na Ngara yaliyopendekezwa kugawanywa hayakizi vigezo hivyo.
Mkoa wa Kagera unayo Majimbo ya uchaguzi jumla Tisa ya Uchguzi ya Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini, Muleba Kasikazini, Muleba Kusini, Biharamulo Magharibi, Ngara, Karagwe, Kyerwa na Jimbo la Nkenge linalopendekezwa kubadilishwa jina na kuwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa