- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala awasili Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani hapa ambapo ziara yake itazihusisha Wilaya zote saba za Mkoa huo huku akishughulikia masuala mbaimbali yahusuyo Uhamiaji.
Akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kupokelewa na Mkuu wa Mkoa ofisini kwake Dkt. Makakala alisema kuwa uwepo wa nchi jirani zinazopakana na Mkoa wa Kagera ni fursa kubwa ya wananchi kufanya biashara na nchi hizo mipakani lakini si fursa za uhamiaji haramu usiofuata sheria.
Dkt. Makakala akielezea namna Idara ya Uhamiaji walivyojipanga katika kipindi hiki cha uchaguzi hasa raia wasiokuwa Watanzania kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa alisema kuwa kama ilivyo kwenye sheria ya uchaguzi pia uhamiaji wanayo sheria ya uraia kwajili ya kutoa elimu kwa wananchi ambao ni wapigakura na wagombea kuhusu madhara ya wananchi wasio raia kupiga kura au kuchaguliwa na wanaendelea kutoa elimu hiyo kwa wananchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akielezea ujio wa Dkt. Makakala alisema amekuja kuongeza nguvu katika kazi ambayo imekuwa ikifanywa na uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji kuondoa wahamiaji haramu pia kutoa elimu kwa wananchi kushirikiana na Serikali katika suala zima la uzalendo wa nchi yao.
“Katika kuhakikisha tunakomesha uhamiaji haramu sisi tumefanya kazi kubwa na Idara ya Uhamiaji imekuwa ya msaada mkubwa kwetu tumewabaini wengi na tumewarudisha makwao kwa kufauata sheria, vilevile tulianzisha Mfumo wa Nyumba Kumi Bora za Usalama ili kuwajengea uwezo wananchi wenyewe kuhakikisha katika maeneo yao hakuna wahamiaji haramu nahatua zinatakiwa kuchukuliwa kuanzia ngazi ya kaya. Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti.
Ikumbukwe kuwa Novemba 8, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti akiwa katika Kijiji na Kata ya Rutoro Wilayani Muleba alitoa onyo kali kwa wahamiaji haramu na wananchi Watanzania wanaowakaribisha wahamiaji hao kwa kuwasaidia kupata vibali vya kuishi nchini kuwa mkono wa sheria utawafikia mahali popote watakapokuwa na watarudishwa kwao kama walivyoingia hata kama watakuwa wamechuma mali wataziacha zote hapa nchini.
Wito kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera ni kutumia fursa za mipaka ya nchi jirani kufanya biashara ili kukuza uchumi wa mkoa wao lakini pia kuhakikisha kuwa hawawakaribishi watu wasiokuwa raia ambao hafuati sheria kutaka kuishi nchini, lakini pia kama kuna raia asiyekuwa Mtanzania na angependa kuishi nchini afuate taratibu na sheria za nchi ili aweze kuishi kisheria hapa Tanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa