- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti azindua rasmi Kampeini ya siku tatu ya Msaada wa Kisheria kwa wananachi wenye kero au migogogro ya Ardhi, Mirathi, Kunyanyaswa kijinsia na kutelekezewa watoto kwa kusikilizwa na kutatuliwa kero zao.
Akizindua Kampeini hiyo Julai 1, 2019 Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya kutemblea ofisi za Wataalam kutoka idara mbalimbali zilizohamishiwa katika Viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba alisema aliamua kufanya utatuzi wa kero za wananchi kwa pamoja kutokana na kero nyingi katika maeneo yaliyotajwa kufika mara kwa mara ofisini kwake kulalamika lakini ufumbuzi wa kero hizo unahitaji idara zaidi ya moja.
“Katika utatuzi huu wa kero za wananchi tukishirikiana na Shirika la MHOLA tumeamua kuleta msaada wa kisheria kwa wananchi kutatua kero za muda mrefu. Pia hapa tunao Wanasheria zaidi ya 15, tunao Maafisa wa Dawati la Jinsia na Upelelezi kutoka Jeshi la Polisi, Maafisa Kutoka TAKUKURU, Ustawi wa Jamii, Idara za Ardhi pia Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri za Bukoba na Manispaa ili kuhakikisha kero zote zinatatuliwa.” Alieleza Mhe. Gaguti
Aidha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pia ilihamishiwa katika viwanja hivyo vya Gymkhana ili kero zinazoshindikana kwa watendaji wa ngazi mbalimbali na kutakiwa kusikilizwa moja kwa moja na Mkuu wa Mkoa mwenyewe ambapo Mhe. Gaguti alizisikiliza papo kwa hapo na kuzitolea ufumbuzi au kuelekeza utatuzi wake kwa mamlaka husika.
Hadi kufikia muda wa saa 7:00 mchana wakati Mkuu wa Mkoa Gaguti akiongea na Vyombo vya Habari tayari wananchi 140 walikuwa wamehudumiwa wanaume wakiwa 72, wanawake 68 na kati ya hao 140 wananchi 69 sawa na asilimia 49% walikuwa na kero za ardhi. Wananchi 46 sawa na asilimia 33% walikuwa na kero za Unyanyasaji wa kijinsia na kero nyingizo. Pia kwa upande wa malalamiko ya Mirathi wallijitokeza wananchi 25 sawa na asilimia 18%
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gerazius Byakanwa alifika katika Viwanja vya Gymkhana kuona wananchi wa Mkoa wa Kagera wanavyopatiwa huduma za Msaada wa Kisheria chini ya uratibu wa Mkuu wa Mkoa na alitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera namna kero za wananchi zinavyotatuliwa kwa mfumo wa kisasa na wenye ubunifu mkubwa kuliko ilivyokuwa zamani.
“Mtwara tunasikiliza kero za wananchi na kuzitatua lakini si kwa mfumo huu wa kukusanya idara zote husika na kuletwa pamoja kwa siku maalum ili kutatua kero hizo, siwezi kusema kuwa nitamuiga Mkuu wa Mkoa ila nimejifunza jambo kwake. Pia huko nyuma kero za wananchi zilikuwa hazisikilizwi ila kwasasa Serikali ipo karibu na wananchi wake ambao ni jambo jema.” Alipongeza Mhe. Byakanwa.
Kampeini ya Msaada wa Kisheria kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera imeanza Julai Mosi, 2019 na ni Kampeini ya siku tatu mfulrilizo ambapo wananchi zaidi ya 2000 wanatarajiwa kuhudumiwa pia Mkuu wa Mkoa Gaguti anaendelea kutoa wito kwa wananchi ambao wana kero wafike katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba ili watatuliwe kero zao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa