• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Katika Ufunguzi wa Wiki ya Uwekezaji Kagera Mabalozi Watano Kutoka Nchi Tano Watoa Vifurushi Vya Fursa Kwa Wafanyabiashara Tanzania

Imewekwa : August 12th, 2019

Wiki ya Uwekezaji Kagera sasa yaanza rasmi mkoani Kagera Agosti 12, 2019 kwa Mabalozi wa nchi tano zinazopakana na mkoa wa huo kuwasilisha fursa zinazopatikana katika nchi walizotoka na fursa hizo  zinaweza kuchangamkiwa kwa namna gani na wafanyabiashara wa Kagera na Kanda ya Ziwa .

Mabalozi hao watano waliwasilisha fursa mbalimbali kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Kagera waliohudhuria kongamano ili kuwaonesha na kuwafungua macho waweze kufanya biashara na nchi hizo. Mabalozi waliowasili mkoani Kagera ni Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya, Uganda na Congo DRC.

Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda Inspekta Jenerali Mstaafu  Ernest Mangu akiwasilisha fursa zinazopatikana nchini Rwanda alisema kuwa Mkoa wa Kagera unahitaji sana kuwa au kujenga masoko ya mipakani ili kusogeza bidhaa mbalimbali karibu na nchi jirani ili kuyafikia masoko kwa haraka badala ya wafanyabiashara kutoka nchi za nje kuingia ndani na kujitafutia bidhaa wenyewe..

Balozi Tanzania nchini Uganda Mhe. Dk. Aziz P. Mlima akiwasilisha fursa zinazopatikana nchini Uganda aliwashauri wananchi wa mkoa wa Kagera pamoja na wafanyabiashara kulima zao la parachichi ambalo sasa lina soko kubwa nchi za nje. “Badala ya kupanda miti ya mbao sasa ni wakati wa kulima parachichi kwa wingi.” Balozi Dk. Azizi

Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dk. Pindi Chana pamoja na kuwasilisha fursa za biashara zinazopatikana nchini Kenya lakini alisema kuwa wafanyabiashara wa Kagera na Tanzania bado wanahitaji Elimu kubwa juu ya biashara za kimataifa kwa kuelimishwa kutumia teknolojia za mitandao badala ya kubeba bidhaa na kwenda kutafuta soko watumie teknolojia ya mitandao kupata masoko .

Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  Lt. Jen. (mst) Paul I.  Mella alisema kuwa nchi ya Kongo ina soko kubwa la biashara na si mkoa wa Kagera tu bali Kanda ya ziwa kutokana na ukubwa nchi ya Kongo ikiwa ni pamoja na wingi wa watu wanaopatikana katika nchi hiyo.

Naye Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dr. Edmund Kitokezi alisema kuwa Burundi kuna fursa za biashara lakini akasisitiza kuwa nchi ya Burundi isiangaliwe kwa udogo wake bali fursa za kibiashara ni kubwa kuliko mtu yeyeto anavyodhania.

Akiifungua Kongamano la wafanyabiashara Mwenyekiti Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. gaguti alisistiza kuona wafanayabiashara wa Kagera na mikoa ya jirani wanaamka na kuchangamkia fursa na kuwa wasumbufu kwa viongozi wa ngazi zote katika kuhakikisha fursa za biashara zinachangamkiwa kwa kiwango kikubwa.

“Hapa tunaongelea fursa ya kitaifa na si mkoa wa Kagera tu kwani kati ya nchi nane zinazopakana na Tanzania nchi nne zote zinapakana na Mkoa wa Kagera kwa hiyo mkoa huu ni kitovu cha uchumi wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati nataka kuona hamasa ya wafanya biashara wetu hapa wakitumia fursa hiyo.” Alisistiza MKuu wa Mkoa Gaguti

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju alisema Mkoa wa Kagera sasa ni wakati wake wa kuinuka kiuchumi katika Awamu ya Tano na uongozi wa Mkoa usiruhusu malumbano ya kiasiasa kukwamisha maendeleo pia usiruhusu wafanyabiashara wabinafsi kuhodhi biashara wao peke yao.

Mwisho Mbunge wa Bukoba Mjini Wilfred Lwakatare aliwashukuru Mabalozi kwa kuja katika kongamano hilo na kutoa elimu hasa ya fursa zinazopatikana katika nchi walizotoka na kusema kuwa Mabalozi hao wametoa cheki ya fedha iliyowazi ili mtu kuandiaka kiasi chochote cha fedha anachohitaji akimaanisha kuwa baada ya Mabalozi kutoa elimu juu ya  fursa, sasa wafanyabiashara wachague wao ni biashara gani wafanye na nchi gani.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa