- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenge wa Uhuru Wapokelewa Mkoani Kagera na Umeanza Kuzindua Miradi Yenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Bilioni 20
Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo Agosti 1, 2017 Mkoani Kagera na Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Emanuel Maganga katika Kijiji cha Kalenge mpakani mwa Kigoma na Kagera ambapo katika Mkoa wa Kagera Mwenge wa Uhuru unatarajia kupitia jumla ya miradi 66 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 20.
Katika miradi hiyo 66 Mwenge wa Uhuru utazindua miradi 36, utakagua miradi 10, utaweka mawe ya msingi katika miradi 20 aidha, mchanganuo wa gharama za miradi hiyo 66 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru Serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi 5,054,041,775 sawa asilimia 25%.
Halmashauri za Wilaya zimechangia kiasi cha shilingi 499,782,895 sawa na asilimia 3% Aidha wananchi wamechangia shilingi 8,441,593,693 sawa na asilimia 46% Wahisani wamechangia shilingi 5,178,273,867 sawa na asilimia 26%.
Mwenge wa Uhuru mwaka huu umebeba kaulimbiu isemayo “Shiriki Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi yetu.” Kauli mbiu hii inawahamasisha wananchi hususani wa Mkoa wa Kagera kushiriki kikamilifu katika shughuli za kuichumi ambazo zinatoa fursa za kuanzisha na kutumia viwanda katika kusindika mazao na bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wetu ili kukuza uchumi wetu kwa maendeleo ya Mkoa na Taifa letu kwa ujumla.
Mara baada ya kupokea Mwenge huo wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Saada Malunde na Mwenge wa Uhuru ukaanza mara moja mbio zake wilayani humo za kukagua miradi ya maendelo ambapo moja ya miradi iliyokaguliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge Amour Hamad Amour ni kituo cha Afya cha Nemba chenye thamani ya shilingi milioni 66.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Kagera Agosti 2, 2017 unatarajia kukabidhiwa Wilayani Ngara na kuendelea mbio zake Wilayani humo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa