• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Kituo cha Mafuta Smart Oil Kinachopatikana Manispaa ya Bukoba na Kukidhi Viwango vya EWURA vya Kutoa Huduma kwa Walaji

Imewekwa : October 9th, 2017

EWURA Yawaelimisha Wafanyabiashara wa Mafuta Kagera Ili Kutoa Huduma Bora kwa Walaji

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yatoa elimu kwa watoa huduma ya Mafuta (Wafanyabiashara ya mafuta) Mkoani Kagera lengo kuu likiwa ni kuwaelimsha jinsi ya kutoa huduma zao kwa walaji (Watumiaji wa Mafuta) na kufuata sheria na kanuni katika kufanya biashara zao.

Akitoa mada juu ya Sheria na Kanuni katika udhibiti wa sekta ya Petroli nchini Mhandisi Godwini Samwel Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA alisema kuwa Mamlaka inatoa elimu kwa Wafanyabiashara nchi nzima ili wazielewe sheria na kanuni za kuendesha biashara za mafuta ili Mamlaka isiwatoze faini kwa kukiuka sheria na kanuni  kumbe hawakuelimishwa awali na Mamlaka hiyo.

Aidha, Mhandisi Samweli alisema kuwa Mamlaka inatoa elimu kwa wafanyabiashara wa mafuta wazijue vizuri Sheria na kanuni za kuendesha biashara hiyo  ili kumlinda mlaji ambaye ni mtumiaji wa mafuta naye apate mafuta yenye viwango kwa bei sahihi na katika mazingira yanayokidhi viwango vya kutolea huduma hiyo.

Katika semina hiyo wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera walitoa changamoto zao katika kuendesha biashara za mafuta ikiwa ni pamoja na EWURA na Mamlaka nyingine kuchelewesha  taratibu za utoaji wa vibali vya kuanzisha vituo vya mafuta ambapo vibali hivyo huchukua muda mrefu zaidi ya mwaka tangu mwombaji aombe kupata leseni.

Akitoa majawabu ya changamoto hiyo Mhandisi Samweli alisema kuwa tayari Mamlaka (WEWURA) wamekaa na wadau wengine kama NEMC wanaohusika na usimamizi wa mazingira na kuwekeana mkakati  wa kuhakikisha utoaji wa vibali unakwenda haraka ili kutowakwamisha wafanyabiashara , mfano kwasasa  (EWURA) wanashughulikia  leseni kwa  siku 45 tu kama mwombaji atakuwa ametimiza vigezo vyote.

Wafanya biashara walioshiriki katika semina hiyo waliishukuru Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuwapa elimu juu ya sheria na kanuni za kuendesha biashara zao hasa uanzishwaji wa vituo vya mafuta kwani walikuwa wanapata changamoto hasa maeneo ya kuweka vituo vya mafuta  kwani kabla ya semina walifikiri kuwa vituo havitakiwi kuwekwa karibu na makazi ya wananchi.

Pongezi hizo zilitolwa baada ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godwini Samwel kutoa ufafanuzi kuwa  hakuna sheria inayozuia kituo cha mafuta kujengwa karibu na makazi ya wananchi ispokuwa taratibu zote za usalama zikifuatwa. Pili alisema kuwa Vituo vya mafuta vinajengwa ili kuwahudumia wananchi kwahiyo ni bora vikawa karibu na wananchi ambao wanategemea kupata huduma hiyo.

Akifunga  Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera Oktoba 9, 2017 Afisa Biashara wa Mkoa wa Kagera Bw. Isaya tendega alitoa wito kwa wafanyabiashara wa Kagera kuhudhuria semina kama hizo zinzpoitishwa na kusisitiza kuwa zina manufaa makubwa katika uendsha ji wa biashara ya mafuta na zinawapunguzia faini wafanyabiashra zisizokuwa za lazima.

Aidha, Bw. Tendega aliwashauri wafanyabiashara waliohudhuria wanaporudi makazini kwao wawaelimishe waenzao kwa kuwapatia makabrasha waliopewa katika semina hiyo ili wayasome na kuzijua Sheria na kanuni za uendeshaji wa  biashara za mafuta ili mkoa uwe na wafanyabiasha walio rasmi na kuondokana na biashara zisizorasmi.

Hadi sasa Mkoa wa Kagera una wafanyabiashara au wauzaji wa mafuta ambao ni rasmi wenye vituo 48 na wauzaji wasio rasmi 72. Jumla ya wafanya biashara ya mafuta yaani wauzaji ambao ni rasmi na wasiokuwa rami jumla ni 120.

Kati ya wadau waliopongezwa kwa kufuata sheria, Kanuni na taratibu za kuanziasha na kutoa huduma za biashara  ya   mafuta Mkoani Kagera ni Bw. Remigius Patrick (Maarufu kama Dk Remy) mwenye kituo cha Smart Oil Kibeta Manispaa ya Bukoba wafanyabiashara wameaswa kuiga mfano wake.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa