- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera Katika Kutekeleza Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa Mikoa yenye fursa nyingi na muhimu za uwekezaji kwa maendeleo ya ukuaji wa uchumi na ustawi wa kijamii. Mkoa unayo hali ya hewa nzuri, mvua za kutosha misimu miwili kwa mwaka, ardhi ya kutosha na yenye rutuba, vyanzo vya maji vya kutosha pamoja na fursa ya kijiografia ya kupakana na chini zote za Afrika Mashariki za Uganda, Rwanda, Burundi na Kenya kwa upande za Ziwa Victoria.
Mkoa wa Kagera unavyo viwanda vikubwa tisa (9), ambavyo mchango wake katika uchumi ni mkubwa kwenye ajira ya zaidi ya (1,050), mapato ya Serikali na huduma mbalimbali kijamii. Kagera Sugar ni kiwanda pekee cha Sukari katika Kanda ya Ziwa kilichopo Wilayani Missenyi na kinatoa ajira zaidi ya 5,000. Viwanda vya kuchakata minofu ya samaki vya Supreme Pearch Ltd kinachotoa ajira ya zaidi 300 kipo Nyamukazi Manispaa ya Bukoba, na Kagera Fish Co Ltd kinachotoa ajira ya zaidi 60 na kipo eneo la Kemondo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.
Viwanda vingine ni viwanda vya kusindika kahawa ambavyo ni Amir Hamza (T) Ltd kinachotoa ajira ya zaidi 70 kipo Manispaa ya Bukoba, TANICA kinachotoa ajira ya zaidi 120 kipo Kastamu Manispaa ya Bukoba, Olam (T) Ltd kinachotoa ajira ya zaidi 250 kipo Wilayani Missenyi, BUKOP Ltd kipo Manispaa ya Bukoba, Kiwanda cha Chai Kagera kinachotoa ajira ya zaidi 200 kilichopo Maruku Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, na Kiwanda cha Maji cha Bunena kinachotoa ajira ya zaidi ya 50 na kipo Bunena Manispaa ya Bukoba.
Aidha, viwanda ambavyo ujenzi wake unaendelea ni pamoja na Kiwanda cha Maharage cha KADERES Plc Wilayani Karagwe, Kiwanda cha nyanya cha Victorius Edibles Ltd Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, na Kiwanda cha Maji, Juisi na Mvinyo cha MAYAWA Manispaa ya Bukoba. Viwanda hivi vinatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2018.
Mkoa wa Kagera tayari umeainisha na kutenga maeneo yenye ukubwa wa takribani hekta 57,000 kwa ajili ya uwekezaji na ujenzi wa viwanda. Vilevile, ili kuhakikisha fursa zilizopo zinatumika kikamilifu kwenye kila wilaya, uongozi wa mkoa umejiwekea Mkakati wa Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja ili ndani ya muda mfupi kila wilaya walau iwe imejenga kiwanda kimoja kikubwa kwa kutumia rasirimali na fursa zilizopo kwa kushirikiana na Wadau wa sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya uchumi.
Katika kuendelea kutekeleza Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda mkoa wa Kagera una mikakati ya kuendelea kujenga viwanda ambapo tayari umepata Wawekezaji Wanne (4) walioonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vikubwa kama ifuatavyo;
GESAP Agro Farming Kiwanda cha Maziwa (Missenyi), KADERES Plc kiwanda cha Kahawa na Novath Mzee Kiwanda cha Maji (Muleba), ujenzi umeanza). Ben Build Investment Ltd kiwanda cha vifaa vya ujenzi (Karagwe). Mkoa unazidi kuwahamasisha Wawekezaji wote wa ndani na nje ya Mkoa kuja Kagera kujenga na kuwekeza katika viwanda kwani mazingira ni mazuri na watapata ushirikiano mkubwa kutoka kwenye uongozi wa Mkoa katika ngazi zote.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa