• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Kuishi Mipakani ni Fursa Kubwa ya Kiuchumi Kwa Wananchi Wetu Watumishi wa Umma Tusiwe Kikwazo Kwa Wafanyabiashara – Profesa Kamuzora

Imewekwa : January 25th, 2019

“Mipaka kati ya nchi moja na nyingine ni fursa ya kiuchumi kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo wakifanya biashara kulingana na masoko yaliyopo katika nchi hizo. Wananchi wanaoishi katika mipaka wanatakiwa kutumia mipaka kufanya biashara na kutajirika kwa kufuata sheria za nchi na jukumu letu Serikali ni kuhakikisha wananchi hawa wananufaika na siyo kuwa kikwazo kwao na mipaka kuonekana si mahala pazuri pa kuishi.”

Msistizo huo ulitolewa na Profesa Faustine Kamuzora Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera wakati akitembelea mipaka ya Tanzania na Uganda iliyopo Mkoani Kagera Wilayani Missenyi (Kabindi- Kashenye, Mtukula na Bugango) pia Murongo Wilayani Kyerwa Januari 22 hadi 23, 2019 alipokutana na wananchi na watumishi katika mipaka hiyo ili kuona namna bora ya wananchi wanaoishi mipakani wanavyoweza kunufaika na mipaka hiyo huku Serikali ikiwawekea mazingira mazuri ya kibiashara.

Hii ni kutokana na uongozi wa Mkoa wa Kagera kuweka azma ya mwaka 2019 kuwa mwaka wa kodi kwa wafanyabiashara wote wakubwa na wadogo kuhakikisha wanalipa kodi stahiki na rafiki ambayo itawafanya kuendelea kufanya biashara zao na kunufaika. Katika hali hyo Profesa Kamuzora anasema lazima Serikali  kuyajua matatizo wanayokumbana nayo wafanyabiashara na kuyafanyia kazi ili wananchi wanufaike na fursa zilizopo katika mazingira yao.

Mara baada ya kutembelea Mwalo wa Kabindi Kashenye Wilayani Missenyi mpakani mwa Tanzania na Uganda upande wa Ziwa Victoria na kuongea na wananchi wa Mwalo huo ambao ni wavuvi walimweleza Profesa Kamuzora kuwa kuna shida ya soko la samaki wakati mwingine viwanda vilivyopo Bukoba vinapata samaki wa kutosha na havinunui samaki wao jambo ambalo linawatia hasara au kulazimika kuuza samaki kwa bei ndogo wakati katika nchi jirani ya Uganda kuna soko zuri la samaki na kwa bei nzuri lakini hawaruhusiwi kuuza huko.

Profesa Kamuzora baada ya kusikilza kilio chao aliwaeleza kuwa ndiyo maana alimua kutembelea mipaka ili aone changamoto zilizopo ili Serikali iweze kuzifanyia kazi ambapo alisisitiza kuwa maana ya kuwa mpakani unatakiwa kucheza na fursa za nchi zote mbili ili utajirike. Profesa Kamuzora aliwaeleza wavuvi hao kuwa Serikali itaangalia namna bora ya kuona nchi jirani Uganda kama kuna bei nzuri ya samaki wavuvi waruhusiwe kuuza huko kwa kufuata sheria na kulipa ushuru wa Serikali lakini pia kutoa  changamoto katika viwanda vya ndani ili vitoe bei nzuri kwa wavuvi.

Pia Profesa Kamuzora alisisitiza kuwa wananchi wanaokaa mipakani wanatakiwa kunufaika na mipaka hiyo kwani likitokea jambo baya mfano vita au magonjwa wao ndiyo wa kwanza kudhurika tofauti na katikati mwa nchi kwa hiyo ni vizuri hata fursa za biashara ziwanufaishe kwani wananchi hao ni ndugu bali mipaka iliwekwa tu Wakoloni lakini bado wao wana mahusiano makubwa.

Katika hatua nyingine Profesa Kamuzora alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kupima viwanja haraka iwezekanavyo katika eneo la Kabindi Kashenye ili kuwe na mji uliopangika na wananchi hasa wanaojihusisha na uvuvi katika eneo hilo waweze kuwa na makazi bora lakini pia na wawekezaji ambao wangependa kuwekeza katika eneo hilo wakute viwanja vilivyopimwa ili paweze kuchangamka kama upande wa pili wa nchi jirani Kasensero.

Profesa Kamuzora akiwa katika mpaka wa Mtukula ambapo alipata fursa kuongea na watumishi wa idara zote za Serikali zinaotoa huduma katika mpaka huo aliwaeleza watumishi hao kuwa wanatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wananchi wanaojishughulisha na biashara katika mpaka huo bali wawe wabunifu katika kazi zao na kutekeleza sheria lakini wakiongozwa na busara kubwa katika kutatua changamoto mbalimbali za kuwasaidia wananchi kutumia fursa ya mpaka kufanya biashara.

“Sisi watumishi wa umma tusiwe kikwazo kwa watu wetu kuwa mpakani ni fursa kubwa ya wananchi wetu kutajirika, ukienda nchi nyingine wananchi wa mipakani ndiyo matajiri kwasababu wamepewa fursa ya kufanya biashara katika pande zote mbili lakini kwa kuzingatia matakwa ya sheria. Sisi tuwe mwangaza na njia kwao badala ya kuwa vikwazo ili tuinue uchumi wao.” Aliwaasa watumishi wa Mtukula Profesa Kamuzora

Aidha, Profesa Kamuzora alisema kuwa baada ya kutembelea mipaka hasa Mtukula, Bugango na Murongo changamoto kubwa aliyoiona ni upande wa pili wa nchi jirani Uganda wafanyabiashara kuchangamkia fursa karibu na mipaka kwa kuanzisha miji na vituo vya biashara wakati huku upande wa Tanzania kukiwa hakuna kilichoendelezwa na kupelekea Watanzania kunufaisha wenzao wa nchi jirani kwa kununua bidhaa huko.

Profesa Kamuzora anasema kuwa kunatakiwa kufanyanyika upembuzi wa kina kuona kwanini nchi jirani wanatambua fursa za mipaka lakini sisi upande wa Tanzania bado.  Mfano Mtukula maduka ya bidhaa mbalimbali yapo upande wa pili wakati huku Tanzania hakuna, hivyo hivyo Bugango Waganda wana maduka makubwa ya bidhaa lakini Tanzania hakuna na Murongo upande wa Uganda Kikagati kuna mji wa kibiashara lakini Tanzania hakuna, mipaka yote Watanzania wanavuka kutafuta manunuzi nchi jirani.

Profesa Kamzora akiongea na watumishi na Viongozi mbalimbali katika Wilaya hizo mbili za Missenyi na Kyerwa alisema kuwa kuna haja ya Serikali kuangalia upya mifumo ya kodi pia kufanya utafiti kwanini wenzetu wanapata fursa ya kufungua biashara mipakani lakini Watanzania hawafanyi hivyo wakati mwingine wanakwenda kufungua biashara upande wa nchi jirani lakini si upande wa Tanzania.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mipakani aliokutana nao Profesa Kamuzora walimweleza kuwa upande wa nchi jirani Uganda kodi zao ni nafuu katika kufungua biashara ukilinganisha na Tanzania na ndiyo maana maduka na biashara zianaanzishwa upande wa pili kuliko upande wa Tanzania. Pia walimweleza kuwa katika upande wa Tanzania mipakani Miundombinu kama umeme maji na pengine barabara nzuri za rami zilicheleweshwa kufika katika mipaka hiyo jambo ambalo linakwamisha sana kibiashara.

Vilevile wafanyabisaha walimweleza Profesa kamuzora kuwa upande Tanzania kuna mamlaka nyingi ambazo zinasimamia sheria zinazofanana na kuleta usumbufu mkubwa kwao mfano TFDA, TBS na nyinginezo ambazo kama zingepunguzwa au kuunganishwa majukumu yake ingeweza kuondoa usumbufu na Watanzania wakaweza kufungua au kuwekeza  kibiashara katika upande wa Tanzania.

Profesa Kamuzora aliwashauri viongozi na Watendaji wa Halmashauri za Wilaya zilizopo mipakani  kuona namna bora ya kuzibaini na kuzichambua chanagamoto mbalimbali zilizopo mipakani na kuishauri Serikali kwani wao ndiyo wanaishi katika maeneo husika kuliko viongozi waliopo Dodoma na Dar es Saam ili changamoto hizo zifanyiwe kazi kulingana na uhalisia.

“Mimi nashauri Mkuu wa Wilaya Pamoja na Wakurugenzi mliopo mipakani kukaa chini na kuzichambua changamoto hizi na kutuletea Mkoani ili nasi tuzipeke mahali panapohusika Serikali ni sikivu itazifanyia kazi. Mfano huwezi kuelewa mpaka ufike huku hata mimi nikiwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu nilikuwa napokea mengi lakini baada ya kufika huku na kujionea ndiyo nimeelewa zaidi. Ibueni nyinyi tuleteeni mkoani ili tuyasukume ili sheria zifanye kazi kulingana uhalisia.” Profesa Kamuzora alisistiza

Profesa Faustine Kamuzora aliyeteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera tarehe 8 Januari, 2019 na kuapishwa Januari 9, 2019 aidha, aliripoti Mkoani Kagera tarehe 10, Januari, 2019 anasema baada ya kukabidhi ofisi sasa ameanza kazi rasmi Mkoani Kagera lakini akianza na kujifunza kwa kupitia mipaka na kuona changamoto zake na kuona namna bora ya kuweka ustawi wa wananchi katika kufanya biashara zao bila bughudha.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa