- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha 2022/2023, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa amewasihi Waheshimiwa Madiwani na Menejimenti kufanya utafiti katika vyanzo vinavyokusanya mapato makubwa ili kujiridhisha makusanyo yanayopatikana kama ni halisi huku akiweka nia ya kuinua pato la wananchi kwani Mkoa wa Kagera unazo fursa nyingi zinazowezesha kukuza uchumi.
Akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika leo Juni 9, 2023 katika ukumbi wa ofisi za Halmashauri, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwa kupata Hati Safi na kueleza kuwa Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa iliyopata hoja chache za ukaguzi hali inayoonyesha kuwa kazi kubwa imefanyika katika kuondoa hoja hizo.
“Kikao hiki ni mwendelezo wa agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia wakati akipokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 tarehe 29, Machi, 2023 ambapo alielekeza kila Taasisi ifanyie kazi hoja hizo na kuhakikisha hoja zote zinafungwa,” ameeleza Mhe. Mwassa
Ameendelea kueleza kuwa Serikali ilitoa agizo kwa kila Halmashauri kuhakikisha inakusanya si chini ya asilimia 85 kwa mwaka. Na kuelekeza kupitia vikao waje na mikakati itakayofanikisha mapato ya ndani yaongezeke. Sambamba na juhudi za makusudi ili mapato yote ya Halmashauri yakusanywe kwa njia ya kieletroniki.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mhe. Privatus Mwoleka ameeleza juu ya uhaba wa watumishi na kumuomba Katibu Tawala Mkoa kusimamia suala hilo na kuweka jitihada za makusudi za ufuatiliaji kwenye mamlaka husika. Jambo ambalo Katibu Tawala Mkoa Ndg. Toba Nguvila amelipokea na kueleza kuwa suala hili linafanyiwa kazi kadri watumishi wanavyoajiriwa.
Akisoma taarifa fupi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Fatina Laay ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba imeendelea kuweka jitihada za dhati katika kuzuia na kupunguza hoja za ukaguzi kwa miaka mitano kutoka hoja 108 mwaka 2018/19 hadi hoja 18 mwaka 2022/23.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa