• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Maafisa wa Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Kutoka Nchi Kumi na Moja Wanafunzi wa Chuo Cha Ulinzi Cha Taifa Waja Kagera Kupata Somo

Imewekwa : January 7th, 2019

Ujumbe wa Kitaifa wa Maafisa wa Vyombo Mbalimbali vya  Ulinzi na Usalama kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence Collage) ukiwakilisha nchi 11 tofauti wautembelea Mkoa wa Kagera Januari 7, 2019 kujifunza na kubadilishana ujuzi na Uongozi wa Mkoa hasa katika masuala ya Ulinzi na Usalama na kutumia fursa hiyo kushauriana namna bora ya kukuza uchumi wa Mkoa wa Kagera.

Ujumbe huo wa Maafisa 16 kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa ukiwa na Maafisa kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Nigeria na China mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera ulipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ofisini kwake na Kiongozi wa Ujumbe huo Balozi Peter Kallage alisema lengo kubwa ni kuja Kagera Kujifunza na kubadilisha mawazo hasa katika Nyanja za Ulinzi Kimataifa na kuona namna bora ya kuendeleza fursa mbalimbali za kukuza uchumi.

“Chuo cha Ulinzi cha Tanifa (NDC) ni chuo ambacho kipo chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na kinaendesha kozi mbali mbali za Kimataifa kama unavyoona hapa tuna Maafisa kutoka nchi nne kama nilivyozitaja hapo awali lakini kwa kozi hii ambayo imetuleta hapa Kagera ina Maafisa kutoka nchi 11 tofauti na tumewagawanyika katika makundi 4 na Maafisa wengine wamekwenda katika mikoa mingine sisi tumechagua kuja Kagera .” Alifafanua Balozi Peter Kallage

Aidha, Ujumbe huo kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa  ulipitishwa kwenye Wasifu wa Mkoa wa Kagera wa Kiuchumi na Kijamii ili kuonesha maendeleo ya Mkoa, Fursa mbalimbali za uwekezaji na changamoto ambazo mkoa unazipitia katika kuendelea kukuza uchumi wake na uchumi wa wananchi kwa ujumla. Katika wasilisho hilo Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa pamoja na Mkoa wa Kagera kufanya vizuri kiuchumi lakini chamoto kubwa ni Wahamaiaji Haramu, na Biashara ya magendo ya Mazao.

“Pamoja na Mkoa wetu kuwa na fursa nzuri za kiuchumi kwa kupakana na nchi tatu za Rwanda, Burundi na Uganda na kuwa kitovu cha biashara cha Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini bado tunakabiliwa na Changamoto ya Wahamiaji haramu na Bishara ya Magendo ya mazao. Tunaendelea kushirikiana na Viongozi wenzetu wa nchi jirani kukomesha uhamiaji haramu, pia uongozi wa Mkoa umeanzisha Mkakati wa Nyumba Kumi bora kuhakikisha biashara hiyo inakoma.” Alieleza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Maafisa hao mara baada ya kupitishwa kwenye Wasifu wa Mkoa walishauri namna mbalimbali za kuimarisha Ulinzi na Usalaama katika Mkoa, namna bora za kufanyia kazi fursa za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Kagera ili kuinua uchumi wa mkoa pamoja na uchumi wa wananchi na kuchangia pato la Taifa kwa ujumla.

Mara baada ya kupitishwa katika Wasifu wa Kiuchumi na Kijamii wa Mkoa wa Kagera Kiongozi wa ujumbe huo wa Maafisa kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa aliushukuru Uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa kukubali ombi la chuo hicho kuualeta ujumbe wa Maafisa hao kuja Mkoani Kagera kujifunza hasa katika fursa mbalimbali za Kiuchumi, Ulinzi na Usalama pia na kuona fursa za uwekezaeji zilizopo Mkoani humo.

Pamoja na kupitishwa katika wasifu wa Kiuchumi na Kijamii wa Mkoa wa Kagera Ujumbe wa Maafisa hao 16 kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa pia utakuwepo Mkoani Kagera kwa ziara ya siku saba ili kutembelea maeneo mbalimbali ya uwekezaji, maeneo ya utalii, viwanda pia na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa