• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Meli ya New Victoria Yatia Nanga Katika Bandari ya Bukoba Wananchi Wajitokeza Kwa Wingi Kuipokea Meli Yao

Imewekwa : June 28th, 2020

Meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu imetia nanga katika Bandari ya Bukoba  leo Juni 28, 2020 majira ya saa 10 jioni ikitokea mkoani Mwanza  ikifanya safari yake ya kwanza mra baada ya ukarabati kukamilika na kupokelewa na umati wa wananchi wa  Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini.

Akiongea mara baada ya meli hiyo kuwasili Mkuu wa Mkoa Gaguti  alisema kuwa ni takribani miaka sita tangu MV Victoria isitishe safari zake kutoka Bukoba kwenda Mwanza ambapo safari ya mwisho ilikuwa tarehe 18 Desemba 2014 na wakati huo Meli hiyo ikitegemewa na  wananchi wa Kagera kwa usafiri na usafirishaji wa mizigo ambapo tani moja ya ndizi ilisafishwa  kwa shilingi 27,000/=ukilinganisha  sasa malori yanasafirisha tani moja ya ndizi kwa gharama ya shilingi 100,000/= hadi shilingi 120,000/=

Aidha, Mkuu wa Mkoa alisema kuwa Meli hiyo sasa imeufungua tena mkoa wa Kagera kiuchumi kwa njia ya maji kuelekea katika nchi za jirani za Uganda na Kenya. Pia alisema kuwa meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu ni mkombozi wa wananchi wote wa Kagera Bodaboda, Mama lishe na wengineo sasa wamejipatia ajira rasmi.

Naye Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Bw. Humphrey Polepole akiongea mara baada ya kuwasili ana meli hiyo alisema kuwa Meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu ipo vizuri na wataaalam wamethibitisha kuwa hakuna hitirafu yoyote kwani  imefungwa mitambo mipya ambayo ina nguvu mara mbili ya ile ya awali iliyokuwemo jambo ambalo litapelekea meli hiyo kufanya safari zake kutoka mwanza kuja Bukoba kwa saa sita tu.

Meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu ina uwezo wa kupakia tani 200 za mizigo na abiria 1200 aidha, imekarabatiwa kwa gharama ya shilingi bilioni 22.8 na Kampuni ya JV of Gas Entec Company Limited, Kang Nam  Corporetion wakishirikiana na SUMA JKT. Pia Meli hiyo imefungwa mfumo mpya wa kidigitali ambapo mfumo wote wa analojia uliondolewa.

Meli ya New Victoria Hapa Kazi Tu baada ya kutia nanga katika Bandari ya Bukoba itaendelea kufanyiwa majaribio mbalimbali ya kitaalam ikiwa ni pamoja na kwenda katika bandari ndogo ya Kemondo kabla ya kurejea Jijini Mwanza na kubeba mizigo ya wanachi bule zaidi ya tani 100.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa