• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mgogoro Kati ya Wafugaji na Wakaulima Kijiji Kashanda Wilayani Karagwe Sasa Kupatiwa Mwarobaini Wake – RC Gaguti

Imewekwa : September 4th, 2019

Mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu zaidi ya miaka kumi na kusababisha uvunjifu wa amani kati ya pande mbili za wananchi ambao ni  wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Kashanda Kata Bugene Wilayani Karagwe sasa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu mara baada ya Mkuu wa Mkoa kuingilia kati ili kurejesha amani ya kudumu katika eneo hilo.

Baada ya kuwa anapokea malalamiko mengi kwa muda mrefu kuhusu Kijiji Kashanda Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti aliamua kufika eneo la kijiji hicho cha Kashanda Septemba 4, 2019 pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ili kujionea mwenyewe jinsi mgogoro ulivyo  ili uweze kuutolewa maamuzi sahihi.

Mhe. Gaguti alipofika katika eneo hilo la Kashanda alikuta ni eneo ambalo halina wananchi ambao wanaishi kama kijiji bali aliwakuta baadhi ya vijana kutoka Wilayani Ngara wakiwa wanafyeka miti na vichaka wakiendelea kulima katika maeneo mbalimbali wakidai kuwa nao wameajiriwa kulima na wamiliki wa maeneo hayo.

Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti hakukuta mifugo ya aina yoyote ile katika eneo hilo bali baadhi ya wakulima ambao walikuwa wamefyeka miti na vichaka ndani ya eneo hilo wakiendelea kulima kwa ajili ya msimu wa kupanda maharage na mahindi na mazao mengiyo.

Kwa maelezo kutoka katika uongozi wa Wilaya ya Karagwe wakiuelezea mgogoro huo walimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa baada ya kutokea uvunjifu  wa amani mara kwa mara wakulima wakijihami na siraha za jadi kama mapanga, mikuki na upinde na wakiwashambulia wafugaji, wafugaji waliamua kuondoa mifugo yao katika eneo hilo ambalo walitengewa kwa kwaajili ya kulishia mifugo yao hasa ng’ombe.

Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya kutembelea eneo la kijiji hicho cha Kashanda na kuona hali halisi alisema kuwa amelielewa eneo lenyewe la mgogoro, pili ndani ya muda mfupi sana ataitisha kikao cha pamoja uongozi wa kijiji hicho cha Kashanda, uongozi wa Wilaya ya Karagwe pamoja na wataalam wote wa ardhi wanaohusika na atatoa maamuzi yenye maslahi mapana ya wananchi, Wilaya na Taifa kwa ujumla.

Kijiji cha Kashanda kipo Kata Nyakahanga Tarafa Bugene Wilayani Karagwe na kina hekta za mraba 3,370.319 na kiliandikishwa kwa hati namba KAG/KIJ 507 chini ya kifungu namba 22 cha sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya mwaka 1982 na hati hiyo ilitolewa tarehe 23 Mei, 1989.

Pamoja na kijiji cha Kashanda kuandiskishwa na kusajiliwa na Serikali hakikutajwa kama kijiji cha wafugaji bali kinatajwa kama vijiji vinginevyo vilivyosajiliwa na Serikali. Aidha, kwa maelezo ya wananchi wa eneo hilo pamoja na Wilaya ni kwamba kijiji Kashanda kilianzishwa kwa kumega maeneo ya vijiji vya Bishehe, Omulusimbi, Chonyonyo na Chabalisa ili wafugaji wapate sehemu ya kulishia mifugo yao lakini baadae eneo hilo lilianza kuvamiwa na wakulima.

Kutokana na mgogogo huo kusababisa uvunjifu wa amani wa mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima wanaolivamia eneo hilo Mkuu wa Mkoa Gaguti amesema kuwa sasa basi lazima mgogoro huo ufike mwisho na ijulikane wazi ni shughuli zipi zinatakiwa kuendelea kufanyika katika eneo hilo ufugaji au kilimo. “Nataka Mkoa wa Kagera migogoro ya ardhi ikomeshwe kabisha na uwe mkoa wa mfano.” Alimaliza kwa kusisitiza Mhe. Gaguti

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa