- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ikiwa ni siku ya pili Agosti 24, 2022 tangu kuanza kwa zoezi la kuhesabu watu, la Sensa ya Watu na Makazi, Mkoa wa Kagera umepokea magari matano kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa kwa ajili ya kusaidia katika zoezi hilo kwa kurahisisha kufika kwa urahisi na kwa wakatimaeneo yenye changamoto
Akizungumza mara baada ya kupokea magari hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Albert Chalamila alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu na kupokea hitaji la Wanakagera kuhusu uhaba wa magari katika kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa zoezi la Sensa na kuupa kipaumbele Mkoa wa Kagera kwa kutoa magari hayo matano yanayokwenda kwenye Wilaya kwa ajili ya shughuli za ufuatiliaji wa zoezi hilo
“Tumeomba magari haya ili zoezi la sensa lisikwame pale inapotokea changamoto katika Halmashauri, tunazo Halmashauri nane na Wilaya saba,leo tunakabidhi magari haya matano ambayo yatakwenda kwenye Wilaya kufanya kazi ya ufuatiliaji ili Mkoa wetu upate takwimu sahihi kuhusiana na Watu na Makazi itakayowezesha kupanga mipango sahihi ya Maendeleo”, alieleza Mhe. Chalamila
Mkuu wa Mkoa Mheshmiiwa Chalamila aliendelea kueleza kuwa siku ya Agosti 23, 2022 wananchi walionesha mwitikio mzuri kuhusu kuhesabiwa aidha, rai kwa wale ambao wanafanya mizaha kwenye mitandao ya kijamii kuwa zoezi hilo si zoezi la utani bali ni zoezi lenye manufaa makubwa kwa Taifa la Tanzania kupata takwimu sahihi. Pia alisisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kuhesabiwa kwani inawezekana Mkoa wa Kagera hauna miundombinu ya kijamii mizuri kutokana na kutokuwa na takwimu sahihi ,hivyo kwa kuhesabiwa Serikali inaenda kupata takwimu sahihi na kuleta maendeleo yanayostahili Kagera.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Ndg. Toba Nguvila alieleza kuwa kutokana na jografia ya Mkoa wa Kagera, yapo baadhi ya maeneo ni magumu kufikika kirahisi. Hivyo magari yaliyotolewa yatasaidia kufikaka kirahisi na kwa wakati. Pia alimshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliona hitaji hilo ambalo liliwasilishwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuomba magari 15 kwa ajili ya kusaidia kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ili zoezi hilo liweze kufanikiwa kwa ufanisi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa