• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Mkurugenzi Mkuu Mpya wa Takukuru Nchini Aweka Wazi Namna Atakavyoiendesha Taasisi Hiyo Nyeti ya Kupambana na Wala Rushwa Nchini

Imewekwa : October 1st, 2018
  • Awaaga Rasmi Watumishi na Wananchi wa Mkoa wa Kagera Kama Katibu Tawala wa Mkoa 

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani aongea rasmi na Vyombo vya Habari nchini kwa mara ya kwanza akiwa Mkoani Kagera na kutaja vipaumbele vyake katika kuiongoza TAKUKURU ili iweze kufanya kazi kwa kasi na ufanisi katika mapambano dhidi ya rushwa.

Mkurugenzi Mkuu Diwani Athumani akitaja vipaumbele hivyo Oktoba Mosi, 2018 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwenye hafla fupi ya kuongea na kuwaaga rasmi Watumishi wa Serikali kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera alisema kuwa vipaumbele hivyo vimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambapo kuna vipaumbele vya muda mfupi na vya muda mrefu ili kuifanya TAKUKURU kutekeleza majukumu yake kulingana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Vipaumbele vya Muda Mfupi; Kwanza ni kuwasimamia watumishi walio chini ya TAKUKURU kuchapa kazi kwa bidii na kuachana na utendaji wa mazoea. Pili, atahakikisha anachukua hatua stahiki na kwa wakati kwa watumishi wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa. Tatu, Kupeleka Kesi zote za masuala ya rushwa  Mahakamani na kufuatilia mienendo ya kesi hizo. Nne, kufuatilia miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa kama inatekelezwa kwa thamani stahiki kulingana na fedha iliyotolewa na

Serikali.

Vipaumbele vya Muda Mrefu: Kwanza, Kufanya uchunguzi katika mfumo wa mapato ili kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali. Katika kipaumbele hiki Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani alitolea mfano wa Wafanybiashara wanaotoa risiti za (EFD) zenye gharama pungufu ya kiwango cha fedha tofauti na thamani halisi ya bidhaa ilyonunuliwa kutoka katika maduka yao.

Kipaumbele cha Pili ni kufuatilia kesi zote za rushwa  zilizopo Mahakani na kuhakikisha kesi hizo zinafika mwisho kwa kutolewa hukumu. Tatu, Kutoa elimu kwa umma kuhusu athari za rushwa na kuelimisha wananchi kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani madhara yake ni makubwa. Nne, Kuweka mfumo mzuri wa kuhakikisha wananchi wanatoa taarifa za wala rushwa lakini pia kuhakikisha wananchi hao wanalindwa mara baada ya kutoa taarifa za kweli. Tano, ni kuongeza ushirikiano kati ya TAKUKURU na wadau wote katika mapambano dhidi ya wala rushwa nchini.

 

Mkurugenzi Mkuu mpya wa (TAKUKURU) nchini Kamishina wa Polisi Diwani Athumani alisema kuwa ameweka vipaumbele hivyo katika kutekeleza majukumu yake akiwa Mkurugenzi Mkuu lengo kuu likiwa ni kumsaidia Rais John Pombe Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa nchini. Lakini pia kuhakikisha anashirikiana na wadau wote wapinga rushwa kuhakikisha kaulimbiu ya “Tanzania Bila Rushwa Inawezekana”  inatimia.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu Diwani Athumani alisema kuwa tayari maelekezo yote aliyopewa na Rais John Pombe Magufuli wakati akimuapisha Chamwino Jijini Dodoma  Septemba 12, 2018 tayari ameanza kuyafanyia kazi yote ili kuhakikisha TAKUKURU inatimiza wajibu wake kwa wakati na kupambana kisawasawa na wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa nchini.

Kamishina wa Polisi Diwani Athumani aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera tangu Novemba 2016 na kuteuliwa rasmi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Septemba 2018 alitoa wito kwa watumishi wote na wananchi kusoma alama za nyakati hasa wakati huu wa Serikali ya Awamu ya Tano kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani si salaam sana kwa wala rushwa nakusisistiza kuwa kesi ya rushwa haiozi hata kama ikipita miaka ishirini mhusika atafikishwa Mahakamani na kufirisiwa mali zake zote.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akitoa neno katika hafla hiyo fupi alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani kwa kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuiongoza Taasisi hiyo nyeti. Pili aliwapongeza watumishi na wananchi wa Mkoa wa Kagera kwa kutoa ushirikiano kwa Diwani Athumani katika majukumu yake akiwa Kagera mpaka Rais akamuona na kumteua kuiongoza Taasisi nyeti nchini.

Pili, Mkuu wa Mkoa Gaguti alimshukuru Diwani Athumani kwa kusimamia vizuri raslimali za Serikali na kusimamia utekelezaji wa miradi ya Serikali Mkoani Kagera hasa mara baada ya Tetemeko la Ardhi lililotokea Septemba 10, 2016. Na miradi hiyo imekamilika kikamilifu na thamani ya fedha inaonekana katika miradi hiyo ambapo alitoa mfano wa Shule za Sekondari za Ihungo na Nyakato kuwa kuwa za kisasa baada ya kujengwa upya.

Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti alimuhaidi Mkurugenzi Mkuu mpya wa TAKUKURU kuwa Mkoa wa Kagera utampa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake kwenye Taasisi mpya kwake ili kuhakikish rushwa inakomeshwa nchini ukiwemo na Mkoa wa Kagera. Pia Mkuu wa Mkoa Gaguti alimshukuru Diwani Athumani kuona umuhimu wa kutoa msimamo wake wa kuiendesha TAKUKURU akiwa Mkoani Kagera kuwa ameupa Mkuo huo heshima kubwa.

Mwisho naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Nesphory Chacha Bwana aliyekabidhiwa Majukumu ya Katibu Tawala wa Mkoa Kagera na Kamishina wa Polisi Diwani Athumani alihaidi kuendeleza kusimamia majukumu aliyoachiwa kuyasimamia kikamilifu ikiwemo kuendelea na utatuzi wa migogoro ya wananchi, Kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za Serikali, Kushirikiana na watumishi katika kutekeleza majukumu ya Serikali na mwisho kufuatilia mifumo ya Serikali.

Matangazo

  • Online Content - inception report for CSA training programme in Kagera region August 19, 2022
  • Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kuhitimishwa Mkoani Kagera Oktoba 14, 2022 August 23, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkoa wa Kagera Wapokea Magari Matano Kusaidi Kufanikisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

    August 24, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Chamila Akagua Miradi na Kuongea na Makarani Wa Sensa ya Watu na Makazi Kagera

    August 23, 2022
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Wanakagera Wakumbushwa Kuendelea Kuilinda Amani ya Tanzania Ili Kufikia Miaka 100 ya Uhuru

    December 08, 2021
  • Tazama zote

Video

Kijue Chuo Kipya cha Kisasa cha Ufundi Stadi VETA Mkoani Kagera Kazi Inaendelea.....
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa